Headlines News :
Showing posts with label VICHEKESHO. Show all posts
Showing posts with label VICHEKESHO. Show all posts

Wednesday, March 4, 2015

AKILI ZA USIKU: SIMULIZI YA MAPENZI

Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati (City Center), nikaipenda suruali moja ya shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya Postal.
Nimefika pale sikukuta mtu hivyo niliingia moja kwa moja, nimefika mle ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika pale kwenye kitundu cha kutolea pesa, ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike iliyoonekana kutuna vilivyo.

Kwa woga mimi huku nikitetemeka mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka nikatizama nyuma yangu sikuona mtu, nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM na ile pochi.

Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata uoga nikamuuliza “Samahani dada, kuna kitu umesahau humu”, yule dada hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela mi nikaondoka zangu fasta kuelekea home.

Nimefika home nikajifungia ndani na kuzibwaga zile pesa kitandani, nikafungua wallet nikakuta imejaa dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia kidogo cha tochi, ATM Card mbili za Benki tofauti ambazo zilikuwa zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na namba za siri za ATM zote, moyo ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora Nipumzike kwanza kitandani!!

Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita, nilipoangalia halikutokea jina nikaona bora nipokee nimsikilize anasemaje, ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa huzuni kwa kubembeleza huku akilia na alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza nilipo aje kuchukua...

Hakuchukua muda akawa amefika nami nikamkabidhi vitu vyote naye akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni 3 za Kibongo na Dollar 500. Dada kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya kibongo mi nikazikataa kwasababu ni mali yake na alizisahau tu.

Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu, mi kama binadamu mwenyezi Mungu atanilipa, nikakataa... Mwishowe akaomba namba yangu na kuondoka zake, akawa ameniacha ndani huku njaa sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku mbili nikaenda kula viepe kavu na soda nikawa powa.

Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka akaenda kunionyesha kwake kisha tukaelekea kwenye nyumba nyingine iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa akaniambia hii itakuwa yako akanikabidhi baadhi ya nyaraka na funguo zote sikuamini...!!

Akanisindikiza kwangu, kufika home ananiambia hiyo gari (Prado) nayo ananiachia ni kwa mema tu niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa na brifcase iliyokuwa na pesa akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya kuanzia maisha, na kumbe yule dada alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!! umasikini baibai...

Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi juu ya kifua changu nikahisi mtu akinishika begani na  kuniita kwa sauti.
“Anko ankoo we ankoo... amka rafiki yako Salim anakuita!!!”.

“ALIKUWA MTOTO WA SISTA ALIKUWA ANANIAMSHA !!”.
Kumbe muda wote nilikuwa nikiota Dah...!!

Thursday, September 25, 2014

Mambo ya Johnny Haya!!!


Mambo ya bwana John Haya 

JOHN alikuwa analala darasani wakati mwalimu anafundisha!
MWALIMU: We John kwanini unalala wakati mi nafundisha?
JOHN: Unajua mwalimu sauti yako nzuri ndio maana nikalala!
MWALIMU: Sasa mbona wenzako hawajalala?
JOHN: Kwa sababu wao hawakusikilizi!!
MWALIMU: Haya nitajie mifano ya wanyama kumi wa pori...
JOHN: Aaaah! uliza swali lingine bhana hilo siwezi kujibu ni rahisi mno!
MWALIMU: Jibu kwanza hilo kama ni rahisi!
JOHN: Simba saba na Chui watatu...!!!
KWA STORI ZAIDI LIKE HAPA https://www.facebook.com/mzukatz
JOHNNY alikuwa analala darasani wakati mwalimu anafundisha!
MWALIMU: We John kwanini unalala wakati mi nafundisha?
JOHNNY: Unajua mwalimu sauti yako nzuri ndio maana nikalala!
MWALIMU: Sasa mbona wenzako hawajalala?
JOHNNY: Kwa sababu wao hawakusikilizi!!
MWALIMU: Haya nitajie mifano ya wanyama kumi wa pori...
JOHNNY: Aaaah! uliza swali lingine bhana hilo siwezi kujibu ni rahisi mno!
MWALIMU: Jibu kwanza hilo kama ni rahisi!
JOHNNY: Simba saba na Chui watatu...!!!

Sunday, March 2, 2014

KITUKO : HOUSE BOY

 


Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.

Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.

Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.

Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss:Bakariiii!
Bakari:Naam boss!
Boss:nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss:Bakariiiii !
Bakari:naam boss!
Boss:nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.

Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari:boss huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno mengine husikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.

Bakari:Boss!
Boss: naam Bakari!
Bakari:Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss kimyaaaa!

Bakari:Bosss!
Boss: ndio Bakari!
Bakari:Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss kimyaaaaaaa!
Bakari:Boss!

Boss: naam Bakari!
Bakari:Nani aliyempachika mimba house girl?
Boss kimyaaaa!

Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!!

Friday, February 21, 2014

SOMA HIKI KISTORI KUONDOA STRESS NA MACHOFU YA MCHANA KUTWA

Kucheki mpira na wanawake ni stresi tupu kwa maswali yao:

Mwanamke: Baby yule jamaa ni Chris Brown?
Jamaa: Hapana anaitwa Theo Walcott.
Mwanamke: Hee.. Ile kadi ya njano ni ya nini?
Jamaa: Ni onyo tu kwamba kafanya kitendo kibaya, akipewa nyekundu anatoka!
Mwanamke: Na ya kijani je?
Jamaa: Hamna kitu kama hicho! Hamna za kijani!
Mwanamke: Nataka Arsenal washinde Kombe la Dunia.
Jamaa: (kimya)
Binti: Yule mzee ni nani?
Jamaa: Arsene Wenger.
Binti: Okay! Kwa hiyo na yule mwingine ni Manchester Wenger?!


USIKU MWEMA 

INGEKUA HIVI , INGEKUA VIPI?

 

"Ingekuwa ni mimi ningeclear mabweni mawili matatu UDOM, Wabunge Bunge la Katiba (wawili wawe wanashea room moja) wangepata pakulala na msosi cafeteria na posho 50,000 kwa siku, usafiri wa to and from bungeni wakati wa session za vikao utatolewa. 
Option ya pili ni familia 600 za Dodoma kuadopt Mbunge mmoja mmoja kukaa nao kwa miezi mitatu. Familia kuwezeshwa posho ya 500,000 kwa mwezi na Mbunge kupata 80,000/ a day. Anayekataa namkodia helikopta mpaka kijijini kwake anashushwa uwanja wa shule ya msingi ya kijiji wananchi watambue kwanini karudishwa."

Sunday, February 9, 2014

CHEKA NA HII

Binti alisafiri kwenda china muda wa miaka 10, alipofka akawatumia wazaz wake kichupa cha dawa wanywe tone 1 moja wasizeeke, baada ya miaka 20 aliporudi alimkuta mama yake kawa bint huku kabeba katoto ka kiume akafurahi kumkuta mama yake kawa binti kigori, akamuuliza mama baba yuko wapi? Mama akamjibu mwanangu baba yako alivyoniona nimekua binti yeye akanywa kichupa chote ndo huyu nimembeba mgongoni. 
Wachina noma!!!!

JERO v/s BUKU KUMI

Masoud Mussa's photo.
JERO anamuuliza Elfu kumi; ulikuwa wapi ndugu yangu mbona huonekani?
ELFU KUMI; Daah! Ndugu yangu mambo mengi, nazunguka sana kwenye ma-wallet na ma-ATM, mara nimeingia bar, mara casino, juzi nilikuwa Airport nikakaa sana pale kisha nikaenda Mlimani city nikatoka nikaenda Serena Inn, Kisha nikachukuliwa nikapelekwa Masaki. Wewe vipi, pande zipi?
JERO; Oooh, mwenzio kila siku kwa mama ntilie, nikibadilisha kiwanja kilabuni, stoo ya mkaa mwenzio sina usafiri wa wallet huku ni mifundo ya kanga na vibubu. Si unaona nilivyozeeka, yaani utadhani mi ndo mkubwa kumbe wewe ndio mkubwa mh!
Masoud Mussa's photo.

Thursday, January 2, 2014

Baba na Mwana

 


Huku akionyesha katika ramani ya dunia iliyobandikwa ukutani,mtoto wa miaka mitano alimuuliza baba yake;
MTOTO: Baba, eti Brazil iko wapi?
BABA: Muulize mamako kwa maana yeye ndo mwenye tabia ya kufichaficha vitu humu ndani!

Wednesday, December 18, 2013

NANI MJANJA?

NANI MJANJA? BABA 1 Mlevi Nyumba yake ina shimo kubwa uani lenye maji Machafu ila halina mfuniko. Siku moja BABA karudi saa 8 usiku toka Ulevini mambo yakawa hivi;
BABA: Funguaa!!
MKE: Leo sifungui, Nimechoshwa na tabia yako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisaa.
MKE. Kufa tu huna faida duniani!.
MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo pwaaa!!
MKE kusikia akajifunga kanga fasta akafungua mlango.
Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.
MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Piga sana 2 wakija uwambie unatoka wapi usiku huu tena na kanga moja!?

Go Slow - School Ahead

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=120363&d=1383939751

Wednesday, October 23, 2013

MAAJABU: KOBE ANAYEVUTA SIGARA

Meet-A-Turtle-That-Smokes-10-Cigarettes-A-Day.jpg2
Maajabu hayaishi duniani na kila siku yanajitokeza maajabu mapya ambayo hukuwahi kutarajia kuyashuhudia maishani mwako . Nchini Japan kuna kobe ambaye amejiingiza kwenye tabia ya uvutaji wa sigara na mpaka sasa anavuta sigara kumi kwa siku.
Kobe huyu alianza tabia ya kuvuta sigara wakati mmiliki wake Bwana Tang alipojaribu kuutoa mfupa wa kuku uliokuwa umekwama tumboni mwa kobe huyo .
Snapping turtle addicted to smoking smokes 10 cigarettes a day, Changchun, Jilin Province, China - 28 Jun 2013
Kobe alimg’ata wakati jamaa alipojaribu kuingiza mkono wake kinywani mwa kobe , Mr Tang aliamua kuiweka sigara aliokuwa akiivuta yeye mwenyewe mdomoni mwa kobe ili kumziba asimng’ate tena . Kobe aliivuta sigara ile huku akiutoa moshi mdomoni kama kawaida na ndani ya dakika tatu ilikuwa imeisha na mpaka sasa imekuwa tabia na kobe huyo anavuta mpaka sigara kumi kwa siku moja . Mr Tang anatafuta njia ya kumuachisha kobe tabia hiyo ya uvutaji sigara.

Use Facebook to Comment on this Post

Tuesday, October 15, 2013

FUNNY STORY ILA SIKUSHAURI KUISOMA

NOT CENSORED
Bibi kizee mmoja alikwenda benki moja maarufu sana hapa nchini ili kuweka fedha zake. Alipofika mapokezi aliuliza.
"Naomba kumuona meneja mkuu wa benki hii"
Mfanyakazi wa mapokezi akamuuliza,"Unataka kumuona kwa shida gani?"
"Nataka kufungua akaunti" akajibu bibi
"Akaunti inafunguliwa hapa hapa mapokezi, sio kwa meneja" akajibu mtu wa
mapokezi.
"Mimi nataka kufungua akaunti ofisini kwa meneja maana nina pesa nyingi sana hapa" akasisitiza yule bibi kizee
"Hata hapa unaweza kufungua kwa pesa hizo zote na zitakuwa kwenye usalama
tu"
" Kama hutaki kunuruhusu kufungulia kwa meneja, basi nakwenda kufungua kwenye benki nyingine" akasema bibi huku akiwa amechukia.
Kuona hivyo, mfanyakazi wa mapokezi akaamua kumpeleka kwa meneja.
"Kwa nini mmeshindwa kumfungulia akaunti huko mapokezi" akauliza meneja
"Amesema lazima afungulie kwako na nilipomsisitiza afungulie mapokezi alitaka
kuondoka"
Basi meneja akaamua amfungulie yeye akaunti. Bibi akazitoa pesa, zilikuwa shilingi milioni kumi taslimu! Hadi meneja akashangaa nakumuuliza,
"Bibi inaonekana pesa hizi umezidundukiza kwa mudamrefu sana eeh?"
"Hapana,nimezipata juzi juzi tu"
"Umezipataje?"
"Kwa kupinga na mtu"
"Kweli? kupinga tu hadi ukapata pesa zote hizo?"
"Yaah, nimepinga tu. Tena hata na wewe tunaweza kupinga
tu"
Meneja: "Ehe,tunaweza kupinga vipi" (akauliza meneja kwa udadisi).
Bibi: "Kwa mfano, tunaweza kupinga kuwa kesho saa kama hizi, pumbu zako zitakuwa za square yaani pembe nne. Kama zikiwa hivyo, wewe utanipa milioni kumi na zisipobadilika mimi nitakupa hizo zangu"
Meneja kusikia hivyo, akakubali mara moja na wakapinga.
Bibi kizee akaondoka. Meneja alibaki akiwa na wasiwasi
sana , hadi alipotoka ofisini kila mara alikuwa anazishika pumbu zake kuona kama zimebadilika. Hadi siku iliyofuata asubuhi bado pumbu zake zilikuwa kama
kawaida. Saa nne asubuhi bibi kizee alifika benki kwa meneja akiwa ameongozana na jamaa mmoja nyuma yake.
Meeneja: "Enhe naona bibi umekuja" (meneja akasema huku akiwa na wasiwasi mwingi).
Ghafla akatoka kwenda chooni kuhakikisha kama pumbu zake ziko sawasawa.
Akakuta hazijabadilika, akarudi mara moja ofisini kwake.
Meneja: "Haya bibi, pumbu zangu hazijabadilika, enhe, si unaona ziko sawasawa? nimekushinda!" (akasema
meneja kwa kutamba).
Bibi kizee akamsogelea meneja na kumwambia kwa sauti ya chini chini.
Bibi: "Sawa baba lakini mimi nitahakikishaje?"
Meneja: "Njoo tu uzishike" akasema meneja.
Bibi;"Sawa lakini lazima uvue suruali nizishike pumbu zako nihakikishe"
Meneja akavua suruali na bibi kizee akaanza kuzichezea pumbu zake. Wakati akiendelea kuzichezea (zilikuwa hazijabadilika) Yule mtu aliyeongozana na bibi alikuwa anajibamiza ukutani
kwa nyuma. Meneja akashangaa na kumuuliza bibi.
"Mbona huyo jamaa uliyekuja naye anajibamiza ukutani?
haoni ataumia?"
"Heh he heee! huyo AMELIWAA!!" alisema bibi na kuendelea,
"Nilipinga naye jana kuwa leo hii saa nne nitakuwa nazichezea pumbu za meneja
wa benki kubwa hapa nchini, akakataa eti siwezi. Tulipinga shilingi MILIONI ISHIRINI! Hivi anakwenda kuzitoa baba!"
Meneja akachukua milioni kumi
na bibi akapata milioni ishirini!

Thursday, May 16, 2013

SIMU L A KICHINA



Utajua kama unasimu ya KICHINA
kama_________
1. Battery inajaa baada ya dk 3 ....
2. Simu ina Tv, microwave, torch, kikata kucha, mswaki, kiberiti cha sigara 
3. Unaweza andika sms hata kwa tooth pick
4. Kuna matatizo ya kimaandishi mfano Nokla, Blackderry, Samvang
5. Ndege ikipita , simu inaandika 1 missed call 
6. Ukiwa karibu na lorry likawashwa kitu kinaandika "Charger Connected"

7. Lazma iwe na Simu card Mbili na bettry mbili 
8. Kukiwa hamna umeme inaandika "insert sim card"
9. Ukipost status facebook ina post 10 nyingine bila wewe mwenyewe  kujua
10. Ukipita karibu na mchina huku bluetooth ikiwa ON , simu inaonesha new hardware found, please enter pairing code

Monday, March 18, 2013

TODAY'S JOKE - DOGO


Wakati wa msosi dingi anamlazimisha dogo aombee chakula, dogo akawa hataki lakini baada ya kulazimishwa sana akaanza kuombea chakula ili wale. Akaanza: "Ee Mungu nakushukuru kwa kutubariki na kumuwezesha baba kupata hela na kutuletea chakula. Naomba umbariki na baba yake Joni mlafi ili Joni aache kuja kudowea chakula kwetu. Naomba pia umbariki Tino ambaye ni kaka yake Joni aache kuja kila siku kumvua dada nguo na

Thursday, March 7, 2013

UKWELI WA MAMBO UKO HIVI. . .

UKILAZIMISHA PENZI KWA MTU AMBAYE HAKUPENDI.
♥ Muda mwingi Unakuwa na stress sababu kila wakati unamuwaza yeye.

♥ Unaweza ukawa kila siku unagombana na marafiki zako wa karibu kisa tu mpenzi wako umemtumia meseji saa nzima hajakujibu na yupo Online aidha kwenye Facebook, BBM , Nimbuzz, Whatsapp n.k.

♥ Ukitaka kumtumia msg au kumpigia Simu Unajistukia sanaa sababu kila siku wewe ndio wa kwanza kumtafuta.

♥ Kila siku  Ku-post status za kuchukia MAPENZI.

♥ Maswali ya kujiuliza kama "kwani Mimi nina kasoro gani"? huwa Hayaishi kichwani mwako kila muda kazima ukae katika KIOO ukijitathmini.

-Haahaa Unaumizwa kichwa yoote hayo kumbee UMESAHAU kuwa  MAPENZI NI HISIA..!!

-Labda Huyo Hana Hisia Na wewe...Acha kujikondesha na mawazo ya ki mapenziii ACHANA NAE Fanya mambo yako ya ki maendeleo.

#KUPENDA USIPO PENDWA NI SAWA NA KUSUBIRIA MELI AIRPORT #


(C) Critical Thinking.

Thursday, May 10, 2012

TODAY's JOKE


Jamaa mmoja kijasho kikimtoka na panga kali mkononi akaingia msikitini, akaanza kuwauliza, "hapa nani muislam?" wote wakawa kimya, akauliza tena, jamani hapa nani muislamu? " watu wakaendelea kuuchuna, akamchukua mmoja wao aliyekuwa amekaa mlangoni akatoka nae nje, kufika nje akamwambia, samahani mkuu wangu kwa kukusumbua, naomba unichinjie mbuzi wangu, jamaa akakubali akamchinja yule mbuzi, kisha akamwambia mie kuchuna siwezi (alikua mzee kidogo) labda urudi tena msikitini, Jamaa akaingia tena msikitini huku panga likiwa limejaa damu , Akaenda kuwauliza tena" jamani nani muislam hapa? " wakamuonyeshea kwa Imamu, Imamu akaanza kujitetea," Aah jamani yaani mie kuswalisha leo tuu  ndo nimeshakuwa muislamu!!!?"
HAHAHA!!!
  • World News

     
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger