Headlines News :

NEWS


\

Ngeleja arudisha milioni 40 za Escrow

Written By Kakytee Media.Inc. on Wednesday, July 12, 2017 | 6:39 AM

Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza,  William Ngeleja amesema kuwa  amerudisha Serikalini kiasi cha shilingi milioni 40.4 ambazo zinatokana na kashfa maarufu ya Escrow.

Ngeleja amesema kuwa alipokea fedha hizo kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemalira anayehushishwa na kashfa hiyo ya Escrow.

Waziri huyo wa zamani wa nishati na madini katika Serikali ya awamu ya nne, amesema kuwa alipokea fedha hizo kwa nia njema hapo mwaka 2014 kupitia akaunti yake ya Benki ya Mkombozi na hakujua  kama zilikuwa na utata.

“Fedha hizo nilizipokea kwa nia njema, kama msaada/ mchango kutoka kwa ndugu Rugemalira ili zinisaidie katika kutimiza majukumu yangu ya kibunge, hususani, kusaidiana na wananchi wa jimbo langu la Sengerema na taifa kwa jumla,” alisema Ngeleja.

Ngeleja aliongeza kuwa fedha hizo alizipokea ili kutimiza shughuli za kijamii za ujenzi wa makanisa, Misikiti, kusaidia kulipia karo wanafunzi na watu wasiojiweza.

Pia Ngeleja amesema licha ya kupokea fedha hizo, alizilipia kodi kwa Mamlaka ya Mapato Nchini(TRA), kiasi cha shilingi milioni 13, (asilimia 30) ila kwa sasa ameamua kurudisha fedha hizo zote licha ya kuwa alizilipia kodi.

Akiongea na waandishi wa habari, Ngeleja amesema amechukua uamuzi huo ili kulinda maslahi mapana ya nchi na chama chake cha Mapinduzi (CCM).

Kashfa ya Escrow iliibuliwa mwaka 2014 kwa baadhi ya viongozi wa Serikali, viongozi wa dini na wafanyabiashara kudaiwa kuhusika kuchota zaidi ya shilingi bilioni 300, fedha zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye akaunti maalumu ijulikanayo kama Tegeta Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Fedha hizo zilihifadhiwa huko ili kusubiri kuamuliwa kwa mgogoro baina ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco).

Kwa sasa baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani ambapo ni mfanyabiashara na mmiliki wa IPTL, Harbinder Sethi Singh na mfanyabiashara, James Rugemalira wa Kampuni ya Engineering and Marketing LTD.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

World News

Text Widget
Sport

 
Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
Template Modified by KakyteeMedia
Proudly powered by Blogger