NDOA YANGU INANITESA
Katika
maisha yangu yote nilitegemea sana na nilihitaji kuwa na mwenzi wa
kuishi naye, kama vile familia nyingine bora ambazo kila siku zina
furaha na ridhaa. Kwa kila mmoja kuwa mwanandani wa mwenzake. Pia
nilimuomba mungu kwa kila hali si kanisani na hata nikiwa katika
mapumziko yangu, anipatie mwanamke ambaye angenifaa katika maisha
yangu.Kila siku palipokucha,niliamka nikiwa na wazo la kumpata
nimpendaye na anipendaye.Niliamini hivyo japo sikuwa na uhakika kama
kweli ningepata mtu kama huyo maishani mwangu.
Siku
zote nilijibidisha kuwa mfano bora ili niweze kupata mchumba, nilikuwa
mtiifu, nikiwa heshimu wenzangu na kushirikiana nao vema kujenga
Taifa.Kujaribu kuwa na marafiki wengi wa jinsia tofauti. Nilijitahidi
nikihisi pengine wale marafiki wangenifaa kumbahatisha wa ubani wangu.
Pamoja na yote hayo sikuweza kubahatika kupata
niliyempenda kutoka moyoni, na aliyenipenda. Nilizidi kumuomba Mungu
anishushie neema ya kumpata wa ubani wangu. Ikafikia wakati nikaomba
ushauri, lakini wale niliowaomba ushauri walionekana kuwa fukara wa
mawazo.Walinishauri wakisema kuoa ni kuoa.Eti mwanamke ningemfunza kama
angekuwa na tabia mbaya.Nikafikiri mara mia mia ushauri wao nikaona
haukuwa na maana zaidi ya upofu.
“Bw.
Kachenje inamaana uwingi wa wanawake ulimwenguni umekosa
umpendaye?”Lilikuwa swali nililoulizwa na rafiki yangu.Hatahivyo
nilishinda kumjibu na hatimaye nikamdharau.
“Inamaana
kuchagua mke wa kuishinae ni sawa na kuokota fungu la samaki sokoni ama
vipi?”Nilijiuliza bila kujijibu kwa wakati huo.
Nilishindwa
kuokota mke ilimradi mke kama vile mtu anavyookota nyanya sokoni na
kulipa pesa, nafikiri hata anayeokota nyanya nae huchagua. Japo kuna
usemi usemao mchagua nazi hupata koroma usemi huo niliupinga na
kuutupilia mbali. Niliamini usemi wa kuoa ni kuoa pengine ningefanya
hivyo basi ndoa yangu isinge kuwa na ladha ya unyumba na isingedumu
maishani.
Nilijawa
na imani kuwa mke mwema hupewa na Mungu, niliishi kwa matumaini ya
Mungu na nilitegemea msaada mkubwa kutoka kwake. Wazazi wangu Mungu
aliwapa baraka walikuwa hai wakinisubiri nioe wamuone mkwe na wajukuu
wao kabla ya kufa. Kwa bahati mbaya sikuweza
kupewa upeo wa kuona mchumba mwema ambaye angekuwa mke wangu, japo
nilikuwa na kazi nzuri na nafasi yangu kazini ilinifanya nionekane
maridadi saa zote.
Watu
wengi walioniona walinishangaa sana, kwani sikuwahi kuonekana na
mwanamke yoyote niliyeongozana naye katika maisha yangu. Si kwamba
nilikuwa na hitilafu yoyote mwilini!. Hapana nilikuwa mwanaume rijali,
na sikupenda kujihusisha na ngono,kwani magonjwa yamezagaa kama inzi
kwenye mzoga.Licha ya magonjwa, ni dhambi kubwa kuzini nje ya
ndoa.Nilitambua kwamba jambo hilo halimfurahishi muumba hata kidogo.Siku
zote nilikuwa nikijilaumu,ikafikia wakati nikitaka kuokota mwanamke
hata baa, moyo ukasita ukinitaka niwe na subira zaidi.Lakini subira gani
huumiza matumbo. Je subira hii itazaa matunda ama nikunizidishia bala
uzeeni?.Nikayatupilia mbali mawazo potofu. Nilihitaji kuwa na subira
nikihisi pengine ningempata atakaye nipenda na mimi kumpenda.
Umri
wangu ulisogea kufikia miaka arobaini. Hali ambayo iliwaogopesha sana
wazazi wangu, waliokuwa wazee wa kujikongoja. Nilizaliwa mtoto pekee wa
kiume na dada zangu watatu.
Wazazi
wangu walichoka na maneno yangu. “Bado umri wa kuona. Nitaoa Mungu
akipenda, mke mwema hupewa na Mungu” Miaka yote huwa nilikuwa najitetea
hivyo .
Ulifika
wakati baba na mama walitaka kuniachia laana baada ya kuwadanganya
zaidi ya miaka kumi toka nipate pesa na kuwajengea nyumba. Walitaka
wawaone wajukuu wao kabla ya kufariki, walijua umri walio kuwa
nao,wasingeishi miaka mitano ama saba mbeleni wangepoteza maisha.
Kwa
kuwaridhisha na kukwepa radhi za wazazi niliwaomba wanitafutie Mke.
Niliamini mke ambaye ningepewa na wazazi angenifaa maishani. “Baba
akimpenda binti, hata mimi sina budi kumpenda” nilijisemea mwenyewe
baada ya kuwapa kazi ya kunichagulia msichana mwenye
sifa zote zile mwanamke anatakiwa kuwa nazo. Ni miongoni mwa nidhamu
kwa mume. Nilikuwa na furaha kidogo, kwani nilijiona niliyejaa Ukungu wa
kutopendwa na kutopenda.
Kwa
ujumla sikujua ilikuwa ni mitihani ya Mungu kwani mimi ni miongoni mwa
vijana waliokuwa wakicheka vijana waliochaguliwa wachumba na wazazi wao,
hakuna kitendo nilichokichukia kama kuchaguliwa msichana na wazazi.
Nilikuwa na imani ya kijana akichaguliwa mke basi hata ndoa ingejaa
migogoro isiyoisha na pengine ikavunjika.
**********
Kampuni
yetu iliitwa JOPHU MINING TRANSPORT CO LTD, mwenye Kampuni yetu,
alijulikana kwa jina la Mzee Jophu Kundy . Ndiye alikuwa Mkurugenzi na
mmiliki wa Kampuni.
Kipindi
cha miaka ya sabini kulikuwa hakuna gonjwa la Ukimwi, kama lilikuwepo
basi ilikuwa halijajulikana kama sasa. Nilikuwa nikienda Nchi Thailand
kila wiki kuuza madini aina ya Tanzanite. Siku zote nilikuwa na urafiki wa karibu na mmiliki wetu Mzee Jophu. Hakuna hata mtu mmoja aliyethubutu kuongea na mzee Jophu aliyeonekana mwenye uso wa ukali saa zote. Haikuwahi kupita siku bila mzee Jophu kuita “Sweedy njoo” nk.Alikuwa kazoea jina langu , pia alinipenda kama mwanae.
Siku
moja niliondoka katika uwanja wa Kia (Kilimanjaro International
Airport) nikielekea Nchini Thailand, Bang kok.Vaaa yangu toshani
kielelezo kwa mtu asiyenifahamu,kusema mimi ni
mtu mwenye pesa za kunifanya niitwe tajiri. Nilivaa suti ya kijivu,chini
nilivalia viatu vya mchongoko,vijana wa sasa huviita ‘Mkuki
moyoni’,mkono wa kushoto nilishikilia ‘breefcase’lililojaa madini ya
Tanzanite.Pia nilivalia miwani ya jua,iliyosababisha vigumu kuona macho
yangu.
Nilikuwa
nimebeba madini gram 5000gm. Sawa sawa na kilo tano Kg 5. Kilo mbili
ilikuwa ni rangi ya blue colour A na kilo tatu (3kg) yalikuwa ni rangi
ya mkojo, kwa wale wakazi wa Mererani wanajua vizuri wakiona na rangi ya
coke ile maji ya kunywa ilikuwa (gm 50).
Ndege
iliacha aridhi ya Tanzania mnamo saa nne unusu asubuhi, ambako
ilichanja mawimbi angani saa mbili na sekunde ya kumi iltua uwanja wa
kimataifa Bang kok.Nilifanikiwa kushuka salama nikiwa mtu wa tano.
Sikuweza kwenda kwenye soko siku hiyo, nilielekea kwenye maegesho ya
gari za kukodi amabako nilikodi gari.
“Halo.kutoka hapa hadi Care lodge ni kiasi gani cha pesa?”
“Dola tano.Karibu”
“Sikuweza
kubishana sana kwani niliamini kauli ya ‘nipunguzie bwana’ ni huku
kwetu.Alinifungulia mlango wa mbele, nilivuta mguu wangu wa kulia na
kuingia ndani mlango wa mbele kulia mwa dereva.Gari hilo lilikuwa ‘Left
hand’.Nilienda moja kwa moja kwenye hoteli iliyoitwa CARE LODRGE .Dereva
alitumia kama dakika nne kuingia lango la hoteli hiyo.Nilipofika,
nilimlipa ujira wake, nikaelekea ofisi za kupokelea wageni(Mapokezi).
Sikutaka kwenda kufanya biashara kwa wakati huo. Niliamua kujipumzisha
kutokana na uchovu wa safari, jambo la kushangaza nilichokiona mbele ya
macho yangu sikuweza kuamini macho yangu kama
yalikuwa sawa sawa ama vipi, nilijaribu kupikicha macho pengine ni ule
ukungu wa kutokuwahi kupenda. Lakini cha ajabu moyo wangu ulisimama kama
sekunde kadhaa, kisha ukaendelea mapigo yake yakawa ya taratibu mno,
ambayo sikuweza hata kuyasikia. Nilihisi jasho jepesi likitiririka,
kwanza nilijitazama kisha nikamtazama mtu huyo, hata hivyo sikuamini kwamba kwa uzuri wake kamwe ningependwa mtu mweusi tena Mtanzania?.
Niliona
mwanadada mmoja aliyekuwa amekaa karibu na muhudumu wa mapokezi katika
hoteli hiyo, msichana huyo alikuwa Mzungu si mzungu, muhindi si muhindi,
mwarabu si mwarabu hata kwenye weusi hakuwepo. Baada ya dakika tano,
nikiwa nimemtumbulia jicho la matamanio, alinisalimia .
“Kaka habari yako”
“Nzuri,
sijui nyie”nilijibu salamu kwa wote,nikiwa bado sijabandua jicho usoni
mwake.Sikushughulika na huyu mwingine,macho yangu tayari yalishapata
chakula.Nilimtizama hamu haikuniisha nikatabani abaki pale pale macho
yangu ya shibe.
“Mimi mzima”aliitikia msichana huyo na aliyefuata ni wamapokezi.
“Hata mimi mzima pia” walinisalimia.
Sikupenda
kukaa na ule mzigo wenye thamani kubwa niliandikisha jina langu na
kuchukua chumba namba kumi.Kila nilipotaka kuondoka kuelekea chumba
nilicholipia ,nilisita na kubakia mdomo wazi,mwili ulibweteka nikitamani
kufahamiana zaidi na mwanadada yule.Niliamua kujilazimiza kuondoka
ingawa nafisi ilitukutika,nilipofungua mlango wangu,niligeuka kumtizama
yule mlimbwendekama vile nikihakikisha kama atakuwa pale.Nilimuona nae
akinitizama.
“Mtoto
mtoto,Duu!.Tembea uone mengi”Niliongea akilini nikiwa nafungua
mlango,katika kuzungusha funguo mlango ukatii sheria ,ukanipa nafasi ya
kuingia.Nilihifadhi Breefcase yangu haraka na kufungua mlango kutoka
nje.Nilikuwa nimeshikilia funguo,nikajikuta nikiziachia bila
kujijua.Yote ni baada ya kumwona yule binti akiwa ametoka chumba
kilichokuwa mkabala na changu.
“Kumbe
chumba nilichochukua kilikuwa karibu na chumba cha Binti yule
niliyesalimiana nae muda mfupi tangu nifike pale.”Nilijisemea moyoni
kiwa nimeacha mdomo wazi ,nikimtizama ,alikuwa kajifunga taulo nyepesi
kabisa.Tayari kwa sasa alikuwa kanipa mgongo,kila alipovuta hatua ,
makalio yake yalitikisikia kama mawimbi ya maji baharini.Miguu yake
minene iliyobeba umbile la wastani lilijivuta kwa madaha.Nilijikuta
nikimtizama hadi alipoishia.
Kwa
kweli nilimpenda na niliamini angenifaa kuwa mwezi wangu na pambo la
ndani. Hata hivyo niliumia moyoni je kama akinikubali nitafanya nini
kama baba na mama watakuwa wamenipatia mchumba wa kumuoa?.Wazo hilo
lilinijia na nikaamua kulitupilia mbali. Lakini ngoja nisiumize kichwa
sijui nitakubaliwa au laa! Kwani nitese nafsi yangu? Nilizidi kuwaza
wakati namalizia kufunga chumba. Pasipo kutegemea mara nambona tena
akiwa kashikilia mafuta ya lotion. Safari hii alikuwa anakuja kwa
mbele,niliweza kufaidi kuisawiri sura yake vema, ilioonyesha umahiri wa
muumba.Tembe yake ungeweza kudhania kachoka vile,lakini hapana ukweli
halisi.Ule ndio mwendo wake halisi,ikafikia hatua nikadhani hakanyagi
chini, kwa jinsi alivyotembea utafikiri anaionea aridhi huruma.
Nikajikuta moyo ukinipasuka “paaa” nikiwa na mshangaa nae alinitolea
tabasamu nono! lililoshamiri usoni mwake.Tena likiwa limeambatana na
mwanya mzuri.Nilishikwa na butwaa kama dakika kadhaa, nikajikuta ubongo
ukifa ganzi. Tulibaki macho pima, hapo nilijua dhahiri kama kunapimana
hivi.Nikajitizama na kumtizama kwa mara ya pili. Mapigo y a moyo
yakaanza kupungua.Hata hivyo nilishindwa kuvumilia yote niliyoyaona kwa
safari hii.
“Samahani dada naweza kujua jina lako”alikuwa kesha nikaribia.
“Yaa!. Jina langu ni Jeniffer John”
“Sawa . Ahsante unajina zuri. Naitwa Sweedy Kachenje” nilijitambulisha nikilamba midomo yangu kuua aibu flani iliyochomoza kama mshale wa sekunde na kupotea.
Tuliongea
mengi na Jeniffer nae hakuwa mvivu wa kujibu maswali na chochote
nilichomuelezea, niliamini ndoto yangu ilitimia, yule mwanamke
niliyempata angeweza kufunika pengo kubwa maishani mwangu. Hata hivyo
katika mazungumzo yetu alinitamkia kwa kinywa chake kuwa nae ananipenda
sana, kuliko hata mimi ninavyompenda. Ni binti aliyeukonga moyo wangu na
kuuteka kila sehemu ya viungo vya mwili wangu, “Kweli subira huvuta
heri” niliongea kimya kimya kwenye mtiririko wa mawazo.
Jennifer
alikuwa ni mchanganyiko wa Mzungu na mwafrika (chotara) na ni msichana
aliyetoka Bara la Africa kama mimi, tofauti ni kwamba yeye alitokea
Africa ya kusini, na mimi nilitokea Tanzania. Wala hakujali Nchi
niliyotoka kuwa ilikuwa ya kimaskini, inamaana alinipenda na umasikini
wangu. Tuliongea na kujikuta mawazo yetu yakiwa sawa, kwa kutaka
kunionyesha upendo alikubali ombi langu la kutaka anisindikize
kuupitisha usiku uliojaa raha za kila aina. Alidiriki kuacha chumba
chake na kuja kulala na mimi, nilimgusia suala la ndoa nalo alilikubali
alikuwa tayari kubadili uraia kuwa Mtanzania. Lakini kama angekuwa
Mtanzania aliyekuwa Afrika ya Kusini umwambie arudi aolewe Tanzania,
angeruka hata futi mia.
Kwa
upande wa mapenzi nilikoga na penzi motomoto, hakuwa mvivu wa
kujishughulisha, tulisaidiana kupitisha usiku huo mwanana uliojaa mahaba
ya kila aina, si mlimani tulipanda vichochoroni tulipita kwa nia imara
ya kumridhisha Jeniffer aliyeonekana mgeni kwenye ulimwengu huo. Asubuhi
kulipopambazuka nilimuaga Jennifer na kuelekea soko la madini ya
Tanzanite, lililoitwa King Life. Kabla ya kuondoka nilimuachia namba ya
simu email address yangu kwa mawasiliano. Na niliamua kufanya hivyo ili
kuwahi na kuwaeleza wazazi habari mpya, wasihangaike kunitafutia mchumba
kwani nilishampata mrembo. Nilifanikiwa kuuza madini yote kwa bei nzuri
na kurudi Tanzania.
************
Nilipofika kazini, nilikabidhi pesa kwa Tajiri yangu Mzee Jophu tukiwa katika maongezi ya mabadiliko ya
kibiashara. Tulisikia mlango ukigongwa kwa nje, bila kujali wala kujua
ni nani mtu huyo, Mzee Jophu aliamuru aingie, Aliingia na alikuwa
sekretari wa Mzee Jophu.
“Boss, samahani kuna wageni wa Sweedy wanamuhitaji” sekretari aliongea akijikanyaga kanyaga na kuuma vidole.Alionekana kumuogopa sana bosi wake.
“Sawa waambie wasubiri kidogo” Mzee Jophu alijibu kwa kifupi na kuendelea na mazungumzo nami.
Tuliongea
na kumaliza, Mzee Jophu alikuwa wa kwanza kutoka kinyume na mashariti
yake, tuliongozana kujua nani alikuwa ananiita. Kwenye viti vya mapokezi
ya wageni, nilimuona baba na mama, mama mwingine wa makamo ambaye
simfahamu, pembeni ya yule mama nisiye mfahamu nilimuona binti mwingine
mrembo. Kwa haraka ubongo ulifanya kazi yake kwa bidii na kukumbuka kuwa
niliwapa kazi wazazi wangu kunitafutia mchumba baada ya kuzunguka kila
kona ya dunia bila mafanikio. Kumbukumbu hiyo iliutesa moyo wangu kwani
nilishapata mchumba mwingine, tena mzuri kuliko yule niliyeletewa na
wazazi, japo nae alikuwa mzuri lakini kamwe asingefurukuta kwa
Jennifer.Ndivyo nilivyo hisi moyoni na wasiwasi ukawa umejidhatiti
akilini.
“Baba
shikamoo, mama shikamoo!, Mama shikamoo!, Dada habari yako!
Niliwasalimia wote nikipita kwa mstari huku nikiwashika mikono. Pia mzee
Jophu naye alifanya hivyo hivyo nilivyofanya mimi. Lakini cha ajabu
aliposhikana mkono na binti yule akabaki amemshika muda
mrefu, macho ya upendo yakiwa yanatambaa usoni mwake. Nilishtuka pale
yule binti alipovuta kujinasua mikononi mwa Mzee Jophu.
Baba hakupenda kufanya mambo kwa siri, alizungumza yote mbele ya mzee Jophu mama na yule mama mwingine na binti yule.
“Mwanangu
unayemuona pembeni ya mama yako ni mama mkweo na msichana unae muona
hapo ni mkeo kazi uliyotutuma tumeikamilisha. Sidhani kuna la ziada zaidi ya kuhitimisha ndoa kanisani” Baba alizungumza na alitegemea kuona furaha, lakini furaha yangu ilifunikwa na uzuri wa Jennifer niliyeonja penzi lake Nchini Thailand.
“Mbona huongei wala huonyeshi furaha” Baba aliniuliza kwa mshangao.
“Baba
ningeomba tuzungumze faragha kidogo. Kuna mambo mengine hayafai
kuzungumza mbele ya mama na watu wengine, nilipoongea hivyo baba alikiri
na kujikuta akitikisa kichwa kuafiki yale niliyoyasema.
Tuliondoka eneo lile na kulizunguka nyuma ya jengo la kazini. “Baba nimekuita mazungumzo ya pembeni nina jipya lililojitokeza”
“Jipya lipi zaidi ya hili nililo kuletea? Baba alizidi kunikazia macho ya ukali.
“Ndio
hilo ni jipya ulilolileta wewe nashukuru. Lakini hata mimi nina jipya
nililopata nikiwa Nchini Thailand kikazi”Baba alionekana mwenye furaha
iliyotoka moyoni, alihisi pengine nimemletea zawadi, kumbe asijue ni
ujumbe wa kumkataa binti walionitafutia.
“Umeniletea suti nini mwanangu Sweedy?” Baba aliuliza huku akiwa ametoa tabasamu zito la kupokea zawadi.
“Hapana baba, ila ninaomba radhi kwa usumbufu.”
“Usumbufu gani?. Sema”
“Nimewasumbua
kunitafuti mchumba. Baba nikiwa Bangkok Nchini Thailand nimebahatika
kupata mchumba ninayetegemea kufunga naye ndoa.”
“Eti
nini”? usinichezee naona unataka radhi ya wazazi, hatuelewi kila kitu
tumemaliza. Mahari tumeshalipa tunachosubiri ni ndoa tu. Halina mjadala”
Baba aliongea kwa ukali, mishipa ya shingoni ilimtoka, ghafla macho
yake yalibadilika rangi na kuwa mekundu.
“Naomba uniambie sasa hivi. Unamuoa yule binti au laa! Sitaki uniambie nikupe muda” Baba alizidi kufoka kwa sauti. Sauti yake
ilienda mpaka alipokuwa mama na mama wa yule binti na binti. “Baba
nisamehe sauti hiyo inasafiri naomba yaishe”Mara anakuja mama akikimbia
huku kanga zikimdondoka alikwapua kanga na kufika pale nilipokuwa na
baba.
“Baba Sweedy kuna nini? Mama aliuliza kwa kudadisi .
“Mwanao anataka kututia aibu.”Baba alisema akinikazia jicho la ghadhabu.
“Aibu gani tena?”Mama akauliza akiwa anamtumbulia macho Baba.
“Mwanao
hataki tena kuoa.Anasema binti tuliyemtafutia hajampenda.Na ameshapata
mchumba huko alikotoka” Baba aliongea kwa sauti ya taratibu iliyojaa
uchungu.
“Hakuna
pingamizi lazima aoe la sivyo atazunguka hii dunia wakumwoa hatamuona.
Hata huyo anayesema amempata pia atamkataa. Kama sisi sio…… nilimkatisha
mama aliyekuwa anaongea kama kuniachia radhi.
“Mama
sasa naona mnaniachia laana, basi nitamuoa binti huyo.” Muda mfupi
niliona maneno hayo yalirudisha furaha zao. Hawakupenda nichelewe kuoa,
mipango ya harusi ilifanyika na tarehe ya harusi ilipangwa.
Wiki
tatu kabla ya kusafiri kwenda nchini Thailand. Nilipokubali wazazi wote
walirudi kule tulipowaacha mama wa binti, binti mwenyewe ambaye ndiye
mke wangu mtarajiwa na mzee Jophu. Lakini tukiwa katika mazungumzo mimi
na wazazi wangu, huku nyuma Mzee Jophu alikuwa akiongea na mama wa binti
aliongea kuwa anamuhitaji yule binti amuoe yeye na sio mimi tena mambo
hayo yalifanyika haraka na kwa siri, si tu kwa maneno bali Mzee Jophu
alimpatia hela nyingi kuliko zile za wazazi wangu walizolipa.
“Mama
kamata laki tano hizi ni zako bado nitakuongeza” kwa shida ya mwanamama
yule alizipokea na kuziweka kibindoni kwa haraka huku akimuahidi
kuvunja ndoa isifungwe, aliniamini angetumia njia yoyote ya kukwamisha
ndoa. Ni mambo ya kusikitisha, mzee Jophu pamoja na kuwa baba wa familia
ya watoto watatu, bado alihitaji mke wa pembeni aliamini kwa pesa zake
nisingeweza kufurukuta “Pesa inazungumza. Pesa ni kila kitu.Haki pasipo
haki kwa tajiri ni haki” mzee Jophu alizidi kuzungumza.
Tuliporudi
pale nilishangaa kumuona Mzee Jophu akiwa na hasira alikunja ndita
aliponiona tofauti na mwanzoni. Nilijiuliza nina kosa gani, kama ni
mazungumzo yetu yalikuwa mazuri nimemfanya nini boss mbona ananitupia
jicho la ukali, nilishindwa kujua kilichoendelea kwa wakati huo.Mama
mkwe mtarajiwa nae alipindua midomo yake na kuibetua kama iliyoteguka
jicho la dharau lilinitizama kuanzia chini ya unyayo hadi juu ya nywele,
kisha kabla ya yote nilisikia akisema “Kijana wenu hana hadhi ya kumuoa
mwanangu. Kwa jinsi ninavyomuona” nilistaajabu kusikia sauti
iliyoambatana na kusonywa.
“Kwa nini mama Getu?. Amefanya nini mwanangu?” Mama alimuliza kwa sauti ya chini.
“Mwanao
hana nidhamu. Uso wake umetawaliwa na dharau. Hawezi kumuoa mwanngu”
aliongea kama kawaida alinitupia macho ya kunitazama kama mtu
aliyejinyea japo maneno yake niliona na niliyasikia yakinichoma moyoni
mwangu. Nilikabwa na fundo kali la ghadhabu nikaamua kumuheshimu tu,
kama si heshima basi ningeropoka neno lolote baya nae limkere moyoni.
Mzee Jophu alikuwa kimya pembeni , macho yakipepesa kwa kuibia na furaha iliyojificha ilionekana usoni mwake, lakini sikuweza kugundua kwanini mama yule alibadilika yeye na Mzee Jophu.
Mama
na baba walimuomba radhi awasamehe kuzaa mtoto asiye na nidhamu na
anisamehe, walijua pengine hasira ile ni kile kitendo cha mimi kumuambia
baba siko tayari kumuoa mwanae kwani nilipata mchumba Thailand. Lakini
mama mkwe mtarajiwa msimamo wake ulikuwa pale pale, hakutaka nimuoe
mwanae, na alitaka arudishe mahari, kwa kile kitendo cha kusema
“Mtoto wenu hana nidhamu” hata alipoulizwa nidhamu gani alishindwa na kubaki akisema.
“Sitaki
nasema basi. Chukueni hela zenu na ng’ombe zenu nne, sikotayari
kumuozesha mwanangu” Aliendelea kuwa na msimamo wake. Kwa maneno ya mama
yule yalikuwa ni furaha kwangu, kwani ningemkosa basi ningeenda kumuoa
Jennifer na kwa upande mwingine yalinikera sana, hasa alipozidi kusema
sina hadhi ya kumuoa mwanae. Eti nina dharau, nilishindwa kumuelewa
alikuwa na maana gani?.
Baba
na mama yangu walinivuta pembeni na kuzungumza kama dakika takribani
tatu, kisha wakarudi na kuomba waondoke wakayazungumze nyumbani.
Waliondoka wote, baba, mama, mama Getruda na Getruda. Hawakutaka
kuyazungumza pale kwani ilikuwa sio sehemu yake. Tulibaki mimi na mzee
Jophu, lakini sikumuona akiwa na furaha kama nilivyomzoea, hakutaka
kuongea na mimi.
“Boss
mbona unaonekana una hasira nini hasa nilichokukosea. Nimeona
umebadilika” kimya kilitanda sikupata jibu lolote zaidi ya kunitazama na
kuondoka zake.
Kesho
asubuhi nilipowasili kazini, nilifanya kazi vizuri kama kawaida nikiwa
naongea na baba na mama kwenye simu. Mara Boss Mzee Jophu anaingia na
wakati huo nilimaliza maongezi na kukata simu, nilipomsalimia hakuitikia
salamu yangu, bali alinitupia barua mezani, na kusema “Sina shida na
salamu yako. Barua hiyo na unijibu haraka iwezekanavyo.Nakupa nusu saa”
aliondoka na kufunga mlango kwa kishindo kikubwa.
Nilishindwa
kumuelewa, lakini kwa matendo yake nilihisi na kuamini barua ile
ilikuwa ya kufukuzwa kazi, lakini nilishindwa kuelewa kosa hasa lilikuwa
lipi?. Homa ya kufukuzwa kazi ikaniingia, nilishindwa kuisoma ile
barua, niliinamisha kichwa nikiwaza.
“Hivi
kama nitakuwa nimefukuzwa kazi nitaenda wapi? Nitamuonaje Jennifer
tena? Nauli sina ya kwenda Bangkok” Ghafla mawazo yakanijia nilikumbuka
kuwa boss alinipa muda wa nusu saa kuijibu barua yake. Ndipo nilipoanza
kuifungua barua huku mikono na vidole vyote kwa
pamoja vikitetemeka kama mgonjwa wa degedege. Nilifanikiwa kufungua
Barua. Kitu cha kwanza kukutana nacho ni maneno yaliyoandikwa kwa herufi
kubwa.
YAH: UPIMAJI WA AFYA KWA AFISA MAUZO, JOPHU MINING TRANSPORT CO.LTD.
Moyo
wangu ulipasuka kwa furaha “nilihisi ni ridandasi kumbe ni kupima afya
hilo halina shida. Ngoja niendelee kusoma” nilijisemea kimoyomoyo.
HUSIKA
NA KICHWA CHA HABARI HAPO JUU, TUMEPATA BARUA KUWA WAFANYAKAZI WA
KAMPUNI YETU WANAHITAJIKA KUPIMA AFYA ZAO, HASA UKIMWI NA AFISA MAUZO
AWE WA KWANZA . BODI ILIPANGA KIKAO CHA SIRI.
MKURUGENZI WA KAMPUNI
JOPHU KUNDY.
Nilimaliza
kusoma barua, lakini hata hivyo moyoni nilijiuliza “Kwanini Mzee Jophu
na msalimia haniitikii, halafu akanipa barua ya kwenda kupima afya
yangu, au anahisi nina virusi nini?. Ama anataka kunitafutia kosa ili
anifukuze kazi nini?. Kwanini ananikasirikia, ni kwa vile wazazi wangu
wamekuja kuongelea maswala ya kuoa hapa kazini au ni nini?.” Nilizidi
kutumbukia kwenye kisima cha mawazo kem kem, bila kupata jibu muafaka.
Kwa ujumla nilishindwa kuelewa wazo halisi la Boss kunitaka nikapime
afya yangu, na nikiwa mtu wa kwanza kazini kupima virusi na kwa nini
alinikasirikia. Muda niliopewa na Mzee Jophu ulitimia, hakupenda
kupoteza muda, aliingia ofisini kwangu na kuniuliza,
“Sweedy umeisoma barua niliyokupatia?. Naomba majibu. Utaenda kupima au hutakwenda?”
“Nitakwenda boss, lakini kwani ni lazima kupima?”
“Ndio, ni lazima hasa wewe” Mzee Jophu alinijibu kwa uhakika.
“Kwa
nini mimi iwe lazima, asiwe mfanyakazi mwingine. Boss unanitisha sana
hasa unaposema ni lazima mimi, na cha kushangaza boss hutaki kuitikia
salamu zangu. Nimekukosea nini, naomba uniambie, ndipo nami nikujibu
kuhusu jibu la kupima” Niliongea nikilalamika kidhaifu kwa boss,
niliogopa mabadiliko ya boss.
“Ok,
usihofu kuhusu kutoitikia salamu yako. Nilijaribu kukutingisha tu
unajua Sweedy mimi na wewe dam dam. Pia watu wanatufananisha kama mtu na
mdogo wake, wengine wanajua dhahiri kuwa wewe ni mdogo wangu wa toka
nitoke. Nilikuwa nakupima imani yako, hivi wewe hushangai toka nikuajiri
kazi hatujawahi kukasirikiana iwe sasa? Wewe ndiye ninaye kuamini
katika kampuni yangu, hata nikifa leo, wewe ndiye utakaye shikilia mali
mpaka watoto wangu watakapokomaa kiakili. Umenielewa Sweedy? Ondoa shaka
yale yote ni matani.” Mzee Jophu aliamua kuficha ukweli uliopo moyoni mwake,
alinichukia mno! kwa muda mfupi tu toka amuone Getruda, binti mrembo,
hakutaka nijue nini kilichotaka kuendelea, alizidi kunifumba kwa maneno
ya uwongo na kunifanya nimuamini kuliko siku za nyuma.
Nilipandisha
pumzi na kushusha kwa nguvu “oophhhh!” “Ni kweli boss lakini ilinifanya
niwe na alama ya kuuliza ndani ya ubongo wangu, hata hivyo sikuamini
kuwa ni wewe ulinibadilikia kiasi hicho. Kuhusu kupima nani kakupa wazo
hili?”.
“Ok,
swali zuri, nilipata barua kutoka mamlaka ya Uhamiaji, kwamba si ruhusa
mtu kutoka nje ya Nchi bila kupima afya, hivyo wewe kama Afisa mauzo
bila kupima hutaenda Nchini Thailand lakini utakapopima utaendelea na
kazi yako kama kawaida.”
“Hakuna
shida boss mimi nitapima virusi najiamini sina kitu, mimi sio mkware”
Nilimjibu. Furaha yangu nikutaka kwenda nchini Thailand nikaonane na
Jennifer .
“Kesho
asubuhi watakuja Daktari kukutoa damu. Hutaenda huko hospitalini, cheo
chako kinakulinda na sitaki uhangaike. Watakuja na kukupima na wiki ya
tatu utaenda Nchini Thailand kama hutakuwa na virusi. Sio sheria yangu
hapana ni serikali”Akasema Boss akizunguka zunguka pale
ofisini.Alionekana mwenye furahabaada yakukubali kuopimwa.
“Nitakuongezea mshaharaasilimia hamsini wa mwanzoni”Alizidi kunipa motisha.
“Nitafurahi Bossi” .
Tukiwa
kwenye maongezi nilisikia simu ikiita. Nilipoitoa mfukoni niliona namba
za baba juu ya kio cha simu. Niliipokea na kuanza kuongea .
“Shikamoo baba.Mama hajambo?”
“Marahaba!.
Wote wazima wanakusalimu. Jiandae kwa harusi yule mama amekubali umuoe
mwanae. Ni baada ya kwenda kwenye mila na desturi, amepewa faini ya
kutaka kurudisha mahari. Umenielewa mwanangu?”
“Ndio baba. Kweli amekubali nimuoe mwanae?. Hata siamini nitajitahidi kukusanya mchango wa harusi”
“Sawa jitahidi mwanangu” Tulimaliza maongezi na kukata simu.
Nilipomtizama
Mzee Jophu alinitupia macho ya lawama, lakini hata hivyo nilichukulia
usemi wa kupima imani kumbe yeye maneno ya yule mama kukubali nimuoe
mwanae yalimuumiza roho sana, na alikiri kumuua mama Getruda
kwa kumsaliti na kumchukulia laki zake tano, lakini kwa upande wa mama
Getruda hakula wala hakuzitumia hata senti tano yoyote, alipanga
kumrudishia baada ya kushindwa kuzuia ndoa isifanyike.
*************
Kesho
yake ilikuwa siku ya mimi kupimwa afya ikiwemo na kupimwa virusi vya
Ukimwi, sikuwa na wasiwasi nilisubiri waje kunipima kwani nilijiamini
sikuwa na virusi, japo nilifanya mapenzi na Jennifer kule Thailand bila
kutumia kinga yoyote.Na hata mapenzi niliyofanya yenyewe yalimfurahisha
na kumridhisha Jennifer na kukiri mimi ni miongoni mwa wanaume wanaojua
mapenzi. Sikupenda Jennifer anidharau kwa upande wa kutomridhisha
kimapenzi.
Waliingia
Daktari waliovaa magwanda meupe wakiwa na vipimo vyao. Waliongozana
moja kwa moja ofisini kwangu, cha ajabu baada ya kusalimiana nao
walitaka nivue nguo nibaki na kaptula, jambo hilo nilipinga.
“Kama kunipima damu ninatolewa damu kwenye mkono sio karibu na uume wangu. Nyie ni daktari kweli?”
“Ndio sisi ni daktari unataka vitambulisho?”.
“Sina
shida na vitambulisho vyenu. Nyie chukueni damu mkaipime, mkileta
majibu mabaya nitarudia hospitali nyingine niliwaeleza waziwazi bila
kuwaficha kitu.”Nikiwa nimeketi kitini,wao walikuwa wamesimama.
Haraka
haraka daktari mmoja alitoa sindano iliyokuwa na kitu kama maji, sijui
ilikuwa sumu au ilikuwa nini!. Maji hiyo ilikuwa ndani ya bomba la
sindano. Kama cc 200. Sikuweza kuona nilikuwa nimegeuka kwa upande
mwingine ili nisione sindano inavyopenya na kuingia kwenye nyama za
mwili wangu. Kwa kifupi nilikuwa muoga wa sindano japo nilikuwa mtu
mzima.
Wakati
sindano ipo kwenye mshipa wa damu nilisikia kitu kama maji yenye
uchungu wa dawa, nilipata maumivu makali nilipogeuka ndipo niliona
akigandamiza bomba la sindano kwa haraka ili nisione kitu, lakini
niliona kitu kilichoingizwa kwenye mshipa wa damu. Nilishindwa kujua
kilikuwa ni kitu cha kuniletea matatizo ama kunijenga ndani ya mwili
wangu.
“Dakitari
wewe unanipiga sindano au umekuja kunitoa damu ili upime Virusi vya
Ukimwi?. Iweje unipige sindano?”. Nilimuuliza daktari kwa hasira baada
ya kusikia ile sindano mwili mzima, nilihisi kizunguzungu mwili ukakosa
nguvu. Tofauti na kabla ya kuingiza sindano yao, halafu walikuwa bado
hawajatoa damu.
“Usijali Sweedy sijakupiga sindano, nataka kutoa damu” alisema huku
akivuta damu kwenye bomba la sindano. Na muda mfupi waliniaga,
alionekana nesi mmoja kati ya wale waliokuja kunitoa damu mwenye
majonzi. Alinitazama kama mtu aliyenionea huruma sana, machozi
yalimlenga lenga lakini hakutaka niyaone aligeuka upande wa pili na
kujifuta na kitambaa alichokuwa nacho mkononi. Nahisi alikuwa anajua
kila kitu kilichotendeka kwa muda ule na sura yake ilikuwa sio ngeni
machoni mwangu, lakini nilishindwa kumkumbuka vizuri. Alijua mipango
yangu yote hasa ile ya kufunga pingu za maisha. Alijaribu kuwa wa mwisho
kuniaga.
Nilisikia
akiniambia “Pole sana Sweedy, moyo unaniuma Mungu akubariki maishani.
Nenda kanywe maziwa mengi yatakusaidia”. Nesi huyo aliondoka taratibu,
huku akigeuka nyuma na kunitazama kwa macho ya huruma. Nilishindwa
kumjibu, nilibaki nikiyaganga maumivu ya sindano niliyochomwa mara ya
kwanza, ambayo sikuweza kuielewa ilikuwa ya nini mwilini mwangu.
Robo
saa baada ya wale daktari kuondoka mkono niliopigwa sindano na kutolewa
damu nilihisi unakufa ganzi, kila nilipotafakari yale maneno ya yule
nesi na kilio chake nilishindwa kumuelewa zaidi ya kujilaumu kwa nini
nimekubali kupimwa pengine wamenipiga sindano yenye sumu ambayo
itanidhuru. Kwa upande mwingine sikuamini niliona yule nesi alinipenda
bure, na Mzee Jophu asingeweza kuwatuma watu wanipige sindano yenye sumu
. Nilimuamini sana tajiri yangu.
****************
Wiki
tatu zilitimia na siku ile ya harusi iliwadia. Kila mtu aliisubiri kwa
hamu sana siku hiyo hasa wazazi wangu kwani walijisikia furaha kwa mtoto
wao wa kiume pekee kufunga pingu za maisha. Nadhani moyoni mwao
walijisemea, sasa ule wakati wa kuwaona wajukuu toka kwa mtoto wetu
Sweedy umewadia. Mzee Jophu ndiye alikuwa mtu wa kwanza kwa watu
walionichangia mchango mkubwa katika kuifanikisha harusi yangu. Sherehe
ilipendeza sana, watu walikula na kunywa hadi wakasaza. Namshukuru Mungu
sikupata lawama yoyote ya kuhusu sherehe yangu.
Getruda
ambaye ndiye ubavu wangu sasa aligubikwa na furaha isiyo kifani.
Sherehe iliyopendeza kwa shamrashamra na vifijo, DJ alitumbuiza kwa
muziki wa taratibu wa wapendanao hasa kibao kilichopigwa na mwanamuziki
Bob rudala nadhani msomaji unaupatapata ule wimbo vilivyo . Utajisikia
vipi ukipigwa siku ya harusi yako? “NIMEKUCHAGUA WEWE” nakumbuka baadhi
ya maneno yake, “Nimekuchagua wewe uwe wangu, wangu wa maisha wa kufa na
kuzikana”msomaji sitaki nikumalizie uhondo tafuta wako na wewe awe wa
maisha ili ujiepushe na mengi hasa janga la Ukimwi. MC au Msema chochote
watu wa mjini wanavyoita alikuwa anaitwa MR.Kicheche ni kicheche kweli
si mchezo ukumbi haukuruhusiwa kukaa kimya siku hiyo watu wote walikuwa
wakicheka na kutabasamu kwa wale wasio na bandama. Kwa ufupi sherehe
ilipendaza mno, hatukuwa matajiri lakini watu wailiridhika na kila idara
ya sherehe.
Sherehe
ilipoisha, tulichukuliwa na gari maalumu siku hiyo kwa bwana na bibi
harusi na tukaelekea kwenye hotel moja iliyoitwa NGORONGORO HOTEL
kujipumzisha. Tulipofika tulikwisha andaliwa kila kitu, chumba kilinukia
harufu nzuri za manukato, choo na bafu ndani kwa ndani ilipendeza kwa
kweli. Washenga waliondoka tukabaki mimi na mke wangu Getruda Kimario.
Nilikuwa
na shauku kubwa ya kukabiliana na binti ambaye alikuwa kigoli, ambaye
hakuwahi kuguswa, nilitamani kupata ukweli wa maneno ya baba
aliyenieleza kuwa mke niliyeoa alikuwa bikira, na mimi nilitamani kumtoa
mwenyewe yaani kama ni gari lilikuwa jipya ‘New model’ na sio mtumba.
Tuliongozana
bibi mbele bwana nyuma, wote tukiwa tumefunga taulo tuliingia bafuni na
kuanza kuoga. Kweli uzuri wa mke wangu niliufananisha na lulu au tunda
Apple. Alikuwa na umbo dogo lenye figa, ambalo lilinifanya nimtamani
zaidi na zaidi. Si kifuani, usoni na umbo lote lilinivutia sana.
Nilimuogesha nae aliniogesha, tulipomaliza tulijifuta na taulo na
kuelekea chumbani.
Tulijitupa kitandani, “Samahani mpenzi nikumbatie, nahisi baridi…nahitaji…..” Ilikuwa sauti ya Getruda iliyojaa mahaba na iliyonisisimua mwili na kuhisi joto .
“Usihofu
kila kitu kitakuwa shwari, nitakupa kila kitu unachokitaka” nilimjibu
kwa sauti nzito iliyomuingiza kwenye ulimwengu wa mahaba.
“Lakini mpenzi unajua nakupenda sana” Getruda aliongea macho ya udadisi yakiwa yametuwa usoni mwangu.
“Naamini
unanipenda mke wangu ndio maana ukaamua tuoane, lakini nahisi mimi
ndiye nimezimika kwako zaidi” nilimweleza na hapo hapo tulikumbatiana na
mabusu motomoto yalishamiri, si mashavuni, mdomoni na kwenye paji la
uso kote tulipeana mabusu ya upendo.
Niliyasikia
mapigo ya moyo wake yakienda kwa kasi jasho jepesi lilimchuruzika
taratibu nilishindwa kuelewa kwani AC au ‘kipupwe’Kiyoyozi kwa jina letu
la kiswahili kilikuwa kinafanya kazi yake kama kawaida. Kila
nilipomshika kwenye kona za mapenzi nilimsikia akizizima kwa sauti za
mahaba, si kwikwi wala kuweweseka zote zilimburudisha. Niliamua kutulia
kidogo baada ya kuona mambo yote nilikuwa namfanyia uume wangu
hausisimka hata kidogo, tofauti na siku za nyuma busu moja kila kitu
kimesisimka, leo mambo yote sikuona hata dalili.
“Oooh.!!! Sweedy unajua mimi sijawahi kuguswa kabisa!”
“Eti!, samahani sijakuelewa mke wangu”
“
Sijawahi kufanya mapenzi toka kuzaliwa. Naomba unifundishe” sauti
nyororo na ya simanzi ya Getruda ilinifanya nilie mwenyewe, sikuwa na
nguvu za kiume, bali nilitamana kumkabili mke wangu nilishindwa kujua
Ugonjwa wa kupooza kwa uume wangu ulitoka wapi na nitamuambia nini mke
wangu, na je atanielewa na wakati nishamchezea kila sehemu, nilizidi kulia sikuwa na la kufanya.
“Unalia
nini tena mume wangu?” Getruda aliniuliza akiwa kalala chali, kama
mgonjwa aliye mahututi . Mweupe mwili wake ulipendeza na kuzidi kung’ara
kila nilipomtazama usiku ule, kwa ufupi alikamilika kila
idara,nilitamani nimrukie lakini jogoo wangu hakutaka kuwika kabisa.
Nilidanganya “Mke wangu nimeshikwa na kichomi cha tumbo sijui ni hiyo AC
“kipupwe” niliongea kidhaifu nikiwa nimeshika tumbo, machozi
yakiendelea kuchuruzika taratibu, niliamini kwa maneno ya kusema
“Naumwa” Getruda angeridhika na kunionea huruma, aliniangalia kwa huruma
na kusema
“Basi mume wangu tuzime usije ukapata matatizo zaidi”. Nikaona duh! Acha nizidi kujitetea “Labda upunguze kidogo”Nilisema nikiwa nimekunja sura na kushika maeneo ya tumbo.
“Pole mpenzi” mke wangu alisema kwa sauti ya utulivu.
“Usiku huu tutapata wapi dawa?. Jikaze usilie”Mke wangu alinionea huruma.
“Usijali mama watoto.Huwa natokewa na tatizo la kichomi ninapofikia hatua ya kufanya tendo la ndoa”
“Kwa hiyo utafanya je?”
“Daktari aliniambia tatizo hili litaisha baada ya kuzoea mwanamke”
“Mwanamke gani, mbona sikuelewi?”
“Wewe,
Usijali tatizo hili litaisha”Nilizidi kumpa motisha mke wangu.Lakini
moyoni bado wasiwasi ulitanda kuhusu jambo hili geni kabisa mwilini
mwangu.
Maneno
hayo ndio yaliyomfanya Getruda, mke wangu ainamishe kichwa magotini
mwangu kama mtu aliyekuwa akisujudu. Sikujua aliwaza nini akilini mwake,
lakini nikahisi yote yalikuwa juu ya matatizo niliyonayo.Muda wa dakika
takribani tano nilihisi kitu kama maji maji angali yenye uvuguvu
yakidondoka gotini kwa tone moja na moja.Matone hayo nilihisi ni machozi
,nikaamua kuinua uso wake kutizama kwamba ni
nini hasa.Kila nilipojaribu kumuinua alikaza shingo.Wazo ambalo nilihisi
kwamba alikuwa akilia likajidhatiti akilini na kuhisi sikukosea.Pia
nilijaribu kwa mara nyingine kumuinua uso wake, safari hii akanisemesha
akionekana kukasirika.
“Mume
wangu umeamua kunitesa angali unajua unamatatizo. Kwanini usingenieleza
kabla, umenitesa naunaendelea kunitesa. Utafanya nini ilikunisaidia,
najisikia vibaya sana mwenzio” aliongea kwa sauti ya chini akiwa
anadondosha machozi, mwili wake ulikuwa umelegea, macho mekundu na ya
kurembua, hakuweza kuvumilia zaidi ya kulia kwa kwikwi, alitamani
niondoe hali ya ubikira na kumpeleka kwenye utu uzima. Maneno ya Getruda
yaliniumiza moyo wangu, nilimuonea huruma alivyokuwa akijigaragaza
kitandani. Machozi yalichuruzika kwa kasi nilizidi kuwaza.
“Au
ni kwa vile ndio mara ya kwanza kukutana naye nini?. Lakini hapana
sijapaniki” labda ni uzuri wake unanichanganya nini? . Au ni chango la
tumbo limesababisha nini?.Sasa tatizo hili litaniumbua” Nilijiuliza bila
kupata muafaka wala sikuweza kuhisi kitu chochote zaidi ya ugonjwa wa
kawaida. Tuliupitisha usiku huo usio na ladha ya mapenzi, si mimi wala
Getruda wote tulihuzunika.
************
Kwa
ujumla maisha ya ndoa niliyaona machungu kama shubiri na pengine
machungu kama mitishamba. Nilishindwa kuelewa ugonjwa huo ulitokea wapi
na umesababishwa na nini? Nyumbani kwangu nilipaona kama jehanamu,
sikuona raha kuwa nyumbani kwani mke wangu alikuwa ananilalamikia kila
siku , kila dakika kuhusu ndoa yetu. Tofauti na ndoa nyingine zikiwa
changa, watu huwa wanatamani wapate hata likizo ya miezi kadhaa ili wawe
pamoja na wandani wao, hapo nasemea kwa wale wafanyakazi kama mimi.Mimi
Sweedy kama mtu mwenye uwezo wa kutunga uongo
basi nilijitahidi kumridhisha kwa maneno matamu niliyoamini
yangemfariji. Uwongo una mwisho wake kumbuka hapo. Lakini hata hivyo ni
mtu gani atasikiliza uwongo kila siku. “Kuumwa kuumwa ni kuumwa gani hukokusikoisha?”.
Nilikuwa
natoka kazini saa kumi jioni, lakini cha ajabu nilikuwa nikitafuta
sehemu ya kupoteza muda ili mradi nirudi nyumbani usiku. Nikiamini mke
wangu atakuwa amelala. Siku zote nilitumia njia hiyo, hata kunywa pombe
nikajifunza ilimradi nikwepe kugungulika udhaifu wangu.Si mitishamba
wala hospitali za kawaida kote nilienda bado ikawa si kitu.
Siku moja mke wangu aliamua kuelekea kazini kuuliza kuhusu ratiba ya kazi zangu. Alimkuta Mzee Jophu mwenyewe.
“Shikamoo baba” Mke wangu akamsalimu pale alipofungua mlango wa Mzee Jophu.
“Marahabaa mchumba mzuri”Mzee Jophu akaitikia salamu kamavile anamuona mke wangu mtoto mdogo.
Hata hivo Getruda ,mke wangu hakujali aliona ni utani tu kwani anajua dhahiri ni shemeji yake.
“Shemeji
nimekuja ninashida”Getruda akasema na kusubiri kitu ambacho angeelezwa.
Mzee Jophu alionekana kutingwa na shughuli nyingi pale ofisini.
Aliinua kichwa chake na kumtizama Getruda kwa macho ya huba.
“Shida gani shemeji?”
“Wala usishituke ni shida ndogo tu”Getruda akasema akiweka pete yake ya ndoa vema.
“Shemu sema kama ni pesa. Nikupatia au nimambo ya familia unataka kunieleza?”
“Ndio, ulijua je?”
“Najua maana nyie wanawake mmeumbwa na aibu sana. Jambo dogo unaweza ukaogopa kumueleza mwanaume”
“Nijambo dogo kwa kulitizama lakini kwa undani nijambo kubwa”
“Sawa ulitaka tukalizungumzie faragha kidogo?”
“Hapana shem. Naomba nikueleze hapa hapa”
“Sawa
nimekuruhusu. Lakini nilipendelea tutoke tukazungumze nje ya ofisi
kwani mambo ambayo haya husiani na ofisi tunayazungumzia nje ya ofisi”
“Naomba nizungumzie hapa , ni kwamba sitatumia hata dakika tatu”
“Ok, sema”
“Naomba unieleze, mume wangu anatoka kazini saa ngapi?”
“Wewe
kwani kakuambia anatoka saa ngapi?”Mzee Jophu hakujibu swali kama
alivyoulizwa bali nae aliligeuza swali upande wa Mke wangu.
“Anasema saa tano usiku”
“Basi inawezekana, kwani mama unaweza kuniambia, maana ya kazi?”
Mzee Jophu alimuuliza swali kwa mtego wa kasa
“Kazi kama ninavyoifahamu ni kitu au ni shuhuli inayoniletea kipato,”
“Ahaa kumbe unajua, mama nenda nitakuambia, maana yake siku nyingine ukiwa na muda.”
“Lakini bado hujanijibu mume wangu hutoka saa ngapi kazi kwako?”
“Saa kumi jioni?”
“Kaaa!. Saa kumi jioni halafu hufika nyumbani saa sita usiku?”
“Inamaana
Sweedy hurudi nyumbani usiku?”Mzee Jophu alimtolea Getruda macho ya
mshangao, huku akishika kiuno kana kwamba haamini maneno ya Getruda.
“Ndio shemeji”
“Siamini
kabisa. Siku zingine huwa na mruhusu saa tisa na siku za jumamosi
anatoka saa sita mchana”Mzee Jophu alizidi kuongezea chumvi.Nia yake ni
kuvunja ndoa yangu ili afaidi yeye.Alipania kuvuruga ndoa yangu.Siku jua
hata nguvu zangu ya kiume zilipoisha ni kwasababu yake.Yeye ndiye
alituma watu ambao walivaa kama Daktari kuja kunipiga sindano ya kuua
nguvu ya kiume.
“Shemeji inamaana maneno yako niyakweli kabisa”
“Shem
nikudanganye iliiweje?.Sitaki kukuvunjia ndoa yako lakini ukweli mumeo
hakupendi. Anasema sana kila siku hapa kazini kwamba mpaka sasa hajawahi
kufanya tendo la ndoa na wewe.Eti mke gani wa kutafutiwa na
wazazi.Anampango wa kukufanya kijakazi pale nyumbani kwake….”
“Eti
nini?.Shemeji naweza kuyaamini maneno yako kwani ni miezi miwili sasa
hajanigusa kabisa. Kila siku anasingizia kuchoka na kuumwa.Raha ya ndoa
iko wapi shem?.Naomba unipe ushauri nimechoka kuvumilia na mateso haya”
“Usichoke
shemeji vumilia tabia itabadilika. Yule bwana anapenda watoto wa shule
sana na mshahara wake mwingi huishia huko.Juzi tu kashikwa ugoni na
mtoto wa shulwe ambapo alitolea faini laki saba, huwezi kuamini lakini
ndivyo ilivyotokea. Mumeo ni mkware kweli…Naomab ausije ukamueleza
maneno haya naomba ufanye siri, nitakueleza mengi siwezi kuvumilia
ukateseka bure binti wa watu”
“Ahsante sana. Leo atanikoma nyumbani”Getruda
aliondoka akiwa na mawazo chungu zima.Machozi yalimlenga lenga
machoni.Moyo uliuuma sana. Waliagana na Getruda, lakini moyoni Mzee
Jophu alibaki na sononeko la upendo kwa mke wangu, Na aliamini kumpata,
kwa jinsi alivyo nitumia Daktari wanipige sindano ya kuuwa nguvu za
kiume, aliamini njia hiyo aliyotumia ya kuuwa nguvu za uume,wangu
ungeshindika kumpata Mke wangu basi angeniuwa kabisa
“Yaani
Sweedy ndivyo alivyo?.Nimemtunzia boma langu iliawe wa kwanza kulibomoa
lakini hataki, anapambana na watoto wa shule?.Haipiti hata siku moja
haachi kusema naumwa sijui kichomi mara nimechoka kumbe anachoshwa na
hao makahaba wa shule?”Getruda alizidi kuwaza njia nzima .Hakuwa
anaelewa sehemu alipokuwa alisha pita nyumba yetu.
Ilikuwa
siku ya juma mosi siku hii aliyotokea kazini,hakuweza kuzungumza
chochote na mimi.Alionekana mwenye ghadhabu kali . Hakutaka hata
kunikaribia, alikwenda kujipumzisha kitandani.Macho yake fika
yalinijulisha kwamba alikasirika sana. Nami niliogopa kumuuliza kwani
nilijua lazima alichukia kutokana na matatizo yangu.Sikuwa nalingine
kichwani.Wakati wa kulala ulipofika ,nilitoka sebleni ambako nilikuwa
nikitizama mkanda wa dini, na kuelekea chumbani.Nilijawa na wasiwasi
kwamba usiku huo kungekuwa na kitimtim kikali, dalili niliiona toka
mapema kabisa.Sikuwa na amani na maisha yangu, hofu kubwa ilikuwa kwa
mke wangu ambaye hakuwa na raha kila aliponiona.Sasa hasira yake ikawa
kubwa pale alipopewa maneno ya uchochezi na tajiri yangu.Nilitembea kwa
kunyata ilitu asisikie kwamba naelekea kitandani.Kwa sasa nikajongea na
kukifikia kitanda.Nilipandisha mguu wa kushoto kwa hadhari sana
asishituke. Pia nilihakikisha kitanda hakichezi, jambo hilo nililifanya
kwa makini zaidi.Wakati huu napandisha mguu macho yangu yalitizama usoni
kwamba mke wangu angeshituka ama vipi. Nilifanikiwa kupandisha mguu wa
kwanza, sasa nikajaribu wa pili kuupandisha kitandani. Laiti ningekuwa
na uwezo ningejitafutia kitanda changu.Ukweli ndoa yangu niliiona chungu
na iliyojaa mateso makubwa sana. Nilikuwa mtu wa wasiwasi tupu.Kitu
kingine, nilijiona nisiye na dhamani duniani, nilitamani nife kuliko
kuishi kwa shida lakini wasiwasi wangu ukawa huko ahera nikukimbiliako
je? Ni kwema aba ndio nitakimbilia mateso mengine?.Nilizidi kuzama
kwenye dimbi la mawazo.
Nikafanikiwa
kupanda kitandani bila mkewangu kushituka,nilihisi angeshituka angetaka
tendo la ndoa wakati huo huo.Sikutaka kulala zaidi ya kulala macho
wazi, nilijua nikishikwa na usingizi ningeweza kukoroma ambapo mke wangu
angeamka, kwani nilijijua toka niliwa shuleni kwamba nimkoromaji mkubwa
hata mtu nyumba ya jirani angesikia.
Sikulala
kabisa, nilihakikisha simgusi hata kwa shuka ambapo angeamka na
kunisumbua.Saa kumi na robo nilisikia jooo za jirani zikiwika nikajua
kwamba kunakaribia kupambazuka. Nikiwa kitandani nilishuhudia miale ya
mwanga ikiingia kupitia dirishani.Nikajua tayari palisha kucha.Mpaka
wakati huo mke wangu hajazugumza kitu chochote na mimi.
Ilikuwa
siku ya Jumapili,siku ya mapumziko,nilikuwa nyumbani na Mke wangu
lakini maongezi yetu yalikuwa juu ya unyumba wetu,si kuhusu maendeleo.
“Hivi
mume wangu umenioa ili niwe pambo lako au kama TV unitizame tu au
laa!.Naomba unieleze nimevumilia vya kutosha”Getruda alisema kwa hasira
baada ya kunitengea chai mezani.
Nilishindwa
hata kuokota kikombe nikabaki nimeduwaa. Nikanyamaza kimya, nilishindwa
niongee uwongo gani,kwani kila siku nilikuwa muongo wa kupindukia,mara
naumwa, mara nimechoka kazini, mara sijisikii,zote hizo zilikuwa njia za
kukwepa aibu.
“Sema”Mke wangu alifoka kwa kunihimiza.
“Kwani baada ya ndoa ni haki kunitendea hivi?Kila siku hupandi kitandani mpaka mimi nishikwe na usingizi………”
Nilinyamaza
kwa muda dakika tatu, kichwa nikiwa nimekiinamisha kama kondoo, kisha
nikameza mate na kulamba mdomo, kila nilipotaka kuongea nilijikuta
machozi yakitiririka kwa kasi,nilihisi labda nililogwa na
walimwengu,kweli imani ya kishirikina ilitawala ndani ya ubongo.Niliamua
kujikaza na kuanza kuongoa uwongo.
“Mke wangu shughuli zangu nzito sana, halafu ni za usiku mno!huwa nachoka nashindwa kufanya tendo la ndoa na wewe”.
“Eti
nini? kwa hiyo kuna wengine unaofanya nao?. Si ndio, hao machangu wa
shule ndio wanakusababishia unione kama mboga zilizochacha eee!.Eti
nashindwa kufanya tendo la ndoa na wewe”.Mke wangu aliongea kwa kufoka
huku akibana sauti na pua akiniigiza nilivyo sema.
“Hapana
mke wangu” nilimjibu kwa sauti ya kidhaifu iliojaa uwoga na simanzi.
Nilikuwa niiingia baa na kunywa, niliporejea nyumbani uliku usiku wa
manane nikiwa chakari. Mke wangu hakuweza kugundua mapema, hata mimi
mwenyewe sikujua ugonjwa huu niliupata wapi.
“Mume wangu”
“Naam mke wangu”Nilimwitikia nikiwa nimeangalia chini,kwa mbali mapigo ya moyo yalinidunda.
“Eti unasubutu kuniitikia.Wewe mwanaume kweli?”
Sikutegemea maneno hayo.Nikahisi mwili kufa ganzi.Nilijiona ninaye dhalilisha hapa ulimwenguni.
“Unafurahia nikuite mume wangu,sivyo?”
“Ndio”Nikaitikia kwa sauti ambayo hata mimi mwenyewe sikuisikia vizuri.
Nikanyamaza,nilijikuta machozi yakinitoka.Kwa kweli moyo uliniuma lakini sikuwa na lakufanya.
“Sasa unataka nikuite mume wangu wakati huwezi?”
“Getruda siwezi nini?”
“Kwani umenioa ilinikupikie tu?”
“Hapana”Nilijibu kwa hofu.
“Sasa unategemea mimi nitaishi vipi?”Safari hii Getruda alishika kiuno.
“Mke wangu vuta subira,nitapona”
“Kwani unaumwa?”
“Ndio, sin’shakuambia naumwa?”Nilikuwa na kila sababu ya kumnyenyekea.
“Hivi
Sweedy unataka kunifanya mtoto.Kwa taarifa yako nimeshajua siri
zako.Juzi umeshikwa ugoni na mwanafunzi ukatozwa laki saba.Na nimepata
tetesi kwamba unapenda hawa wa kusoma”Getruda alinishikia kibwebwe.
“Huu ni uzushi wa watu wasipenda niwe nawe.Naomba usisikilize maneno ya wafitini”
“Sio wafitini.Niwatu wanaokujua kwa ukaribu tabia yako”
Zogo lilikuwa kubwa ambalo lilichukua masaa sita.Baada ya hapo mke wangu akaondoka kwenda mjini.
Hakuwa
na safari bali aliamua kwenda mjini kununua gazeti la Mwanasport,
lililoandikwa mwongozo wa kumridhisha mwenzi kiunyumba, na kuliweka
kwenye meza makusudi ilinilione.
“Haya nakuuliza umesoma gazeti nililokuwekea kwenye meza?”
“Gazeti lipi mke wangu?” nilimuuliza kwa sauti ya chini.
“Hili hapa” mke wangu alinionyesha huku akinipatia nisome.
“Mwongozo wa njia za kumridhisha mwenzi kiunyumba”
“Aaaaa! Gazeti hili, kipengele hiki nisha soma….” Nilijaribu kuchangamka kijanja, lakini huzuni ilibaki pale pale.
“Uongo” Getruda alinishupalia
“Haki
ya Mungu, nimesoma kipengele hicho tena kinasisitiza swala la unyumba,
mume amtendee haki mkewe na mkewe amtendee mume haki yake, tena hii
hapa….” Nilijaribu kujitetea kwa unafiki.
Nilichukuwa
gazeti lile na kupitisha macho juu juu kwa haraka na kumwambia nimesoma
ndani vizuri. Nilifahamu sana nia yake haswa ilikuwa ni nini?
Nilimtizama mke wangu kwa masikitiko na kumuonea huruma, lakini
ningefanya nini ili kumridhisha, nae aridhike japo mara moja.
“Samahani mke wangu siku hizi na choka kwa shughuli nzito si mchana wala usiku, hata nimesahau kufanya mapenzi nawe”
“Hivi wewe unavyosema siku hivi, ina maana toka tufunge ndoa, tumeshafanya chochote na sasa karibu miezi miwili na nusu?”
“Basi ni samehe mke wangu”
“Nikusamehe kwa lipi?. Usinipotezee muda ninachoomba ni haki yangu bwana”
“Naomba unipe muda wa wiki nzima”
“Sitaki,
ninacholilia ni haki yangu.Kwani kanisani uliapa kwamba utanitendea
hivi. Ulinioa wanini kama hukunipenda, naomba talaka yangu haraka…”
“Umeenda mbali sana mke wangu…”
“Mimi
sio mkeo kuanzia sasa. Naomba uelewe. We mwanaume gani?”Getruda
alionekana mwenye hasira ,nikaamua kutulia kama niliyenyeshewa na mvua.
Akrabu
za saa zilionyesha saa tisa na robo usiku, mke wangu alijawa na
fukutiko la moyo lililokuwa zito, japo alikuwa na hasira lakini
alijitahidi kuiondoa ili kunitamanisha. Muda mfupi aliingia chumbani na
kufuata kabati lake lenye makorokoro yote ambayo yanampendezesha
mwanamke kuwa kivutio mumewe au mchumba au mwanaume rijali. Alichukua
muda kidogo akijipodoa na kujipara, mafuta sijui lotion, cream,
manukato, wanjaa lipshine nk. Hakuishia hapo alivaa sketi fupo, ambayo
wanaita kimini kilichoonyesha mapaja yaliyonona, na kibilauzi kifupi,
wengi huita “kitopu” chenye kuonyesha kitovu kilichoumbika sawia, usoni
alipaka poda kwa mbali na kujipulizia manukato yenye harufu ya mahaba.
Mke mwenye sura mufti, nyororo kwa macho ya kuita japo mke wangu
alijitahidi kwa vitu vyote hivyo lakini ilikuwa sawa na kupiga kinyago
ukwenzi, nilibaki kama zoba na mbege.
Juhudi
zote za kujipara manukato, tabasamum nono! Nilibaki kuwa sikuuwona
uzuri ule, kumbe ni kwasababu nilikuwa siyawezi. Uzalendo nae
ulimshinda, ndipo alipaanza kuuliza.
“Mume wangu urembo wote nilonao bado hunitamani? niambie unanipenda au hunipendi” “Nakupenda”
“Sasa kama unanipenda mbona hunifa…” alizidi kulalama kila siku, kila dakika, kila sekunde.
“Nisamehe
mke wangu ongea taratibu jirani watasikia”. Niliongea kwa sauti ya
chini nikiwa nimempigia magoti mke wangu, sikupenda jirani watambue
udhaifu nilionao.
“Nirahisi
kupata msamaha wangu, lakini nataka ufanye ninachokuambia, umenielewa
mume wangu” mke wangu alipunguza ukali kidogo na kuanza kupitisha mkono
wake wa kushoto akipapasa kifuani mwangu.
“Haya
twende tukatizame mkanda wa X kwenye video ya chumbani” mke wangu
aliongea kwa kunibembeleza, aliamini yeye kama mwanamke lazima
ambembeleze mumewe,amfanyie vile vitu anavyopenda ili penzi likomaa na
kufika kileleni.
Tulifika
chumbani nilijitupa kitandani kigoigoi, roho ikiniuma “Ugonjwa huo wa
kuuwa nguvu za kiume niliupata wapi? Au huyu mke ni jini nini? Mbona
nimemuoa na uume wangu kukosa nguvu, kwanini? Mbona jenifer
nilimridhisha vya kutosha. Mama mkwe kaniloga nini?. Hataki niwe na
mwanae” Alitoa mkanda kwenye droo za kanda kisha akasema “Mkanda huu
nimeaununua kwa ajili yako. Najitahidi kila namana kukuvuta jirani nami
mpenzi” Getruda aliongea huku akitoa tabasamu nono.
“Halafu baada ya kuangalia nini kiendeleee?” niliongea kwa wasi wasi mkubwa tena kwa kuropoka, nilihisi kuchanganyikiwa.
“Kwani wewe umenioa niwe nani kwako, au nifanye nini. Niambie sio kuropoka maneno yasiona maana” Getruda alizidi kufoka.
“Vitu vingine vinaleta kero, sijui huyu ni mzigo, au nini?” Getruda alijisemea kimoyo moyo.
“Basi yaishe mpenzi, punguza hasira”
“Ooo! Kumbe ulikuwa unataka tujifunze kitu”
“Ndio, ili tujifunze wazungu wanavyoridhishana”. Getruda alipunguza hasira kidogo yote hayo ni kunifanya nisisimke.
“Kaaa!
Pamoja nami?” Kwa kweli nilichanganyikiwa kabisa, nilikkuwa nikiropoka
maneno yasiona msingi, hata nilivyomjibu aliniona limbukeni.
“Kwani
ajabu, ndio nikae nawe!” Getruda alizidi kushikwa na hasira usiku mzima
hatuku lala ni kukoromeana, maneno ya lawama na mengine ya kuomba
msamaha.
“Nikae
na wewe tu?” nilizidi kumyumbisha kwa maneno ya ajabu ilimradi
papambazuke niondoke mikononi mwake. Nilitamani pakuche niondoke niende
kazini.
“Hukubali eee!, niambie hutaki?”
“Aaaaa! Na kubali kabisa bila hofu” jibu hilo lilimfurahisha Getruda mke wangu aliamini ningefanya mapenzi muda mfupi.
“Basi
vizuri, nitashukuru mume wangu, na nitakupa unachotaka, japo sijawahi
kufanya ngono lakini nitakuachia ufanye utakavyo taka.” Mara moja
alianza kuimba
“Basi mume wangu Sweedy, wewe ni wewe
sina mwingine, kama ni kundi la ndege msituni basi wewe ndio chaguo
langu, wengine sioni, nakupenda peke yako naomba uangaze pendo letu
ling’are giza,…” Alitunga wimbo wa muda mfupi.
Getruda,
mke wangu alinifuata kitandani baada ya kuweka mkanda wa mapenzi,
alinikumbatiam tukaanza kuviringishana huku na kule. Lakini wasi wasi
ulinijaa pale nilipo kumbuka mapenzi na mke wangu, niliamini hakuna
chochote kingeendelea zaidi ya kumtesa Getruda. Wala sikuwa tayari ajue
udhaifu wangu, nilihofu pindi angejua basi angeomba talaka, hata hivyo
siri ingekuwa hadharani, kila kona ya dunia.
Baada ya kuchoka mabusu, alilala kwa chali akiwa ananitizama, kwa hofu nilitizama pembeni, sikuweza kumuangalia usoni.
“Niangalie
basi nijue unanipenda” nilipomtizama kwa kujikaza, nilisikia akisema
(Ooooohhh! Honey you look at me, without uttering any word”) “Ooooohhh!
Mpenzi unanitizama bila kunena neno!” Nilituliza macho uso mwa Getruda,
uso ulijaa ubembe. Ingawa nilifahamu shauku ya
mke wangu lakini nilishindwa nimfanyie nini ili nionekane kidume na mume
hodari, sio sifa ya kuoa tu ndoa Kanisani. Lakini lazima nimburudishe
mke wangu hata kwa kumshika shika maungo yake, ili kumtuliza asionekane
mwenye sikitiko moyoni.
Hata
hivyo mke wangu hakuchoka na vitimbi vyangu, aliendelea kunishika
shika, ili kuniondoa uchovu. Aliona muhimu na dawa ni kwenda na mimi
bafuni kuoga, tulienda bafuni na kuanza kuoga pamoja, lakini hakuona
uume wangu ukisisimka hata kidogo. Hofu ilianza kumuingia hakuamini
alivyonihisi aliona ni uchovu tu wa kawaida. Hakuwa na roho ya kukata
tamaa, kule bafuni alijitahidi kuushika na kupapasa maungo yangu,
sikuonyesha dalili yeyote ile.
Getruda akaniogesha nami nikamuogesha.Tulipomaliza akachukua sabuni na bush la kuogea tukaelekea chumbani tukiwa tumefunga taulo. Getruda alionekana kuwa na hasira kali moyoni.
“Mume
wangu naona hunipendi kutoka rohoni, Bali ulilazimishwa na wazazi wako
sio hivi hivi ni miezi miwili sasa inatimia toka unioe hutaki kufanya
tendo la ndoa. Heshima ya ndoa iko wapi? Naomba unieleze kama hinitaki
niondoke au nini kimekusibu?”
Wakati
ananielezea machozi yalikuwa yanambubujika, aliamini kulia sio
suluhisho, taratibu alifuta machozi kwa lesso, alinisogelea karibu na
kunizungushia mikono kiunoni, huku akininong’oneza “Sweedy kuna kitu
chochote nisichokuridhisha mume wangu. Naomba unieleze niweze
kujirekebisha. “Tafadhali niambie sasa hivi. Nahitaji kujua, nitaishi
vipi bila mapenzi yako?”
“Kila
kitu unaniridhisha ila ni…ni…nina…ni….” nilikokoteza maneno
yaliyochanganyikanana kigugumizi, nilishindwa kutamka vizuri nilihisi
homa kali, nilijua ndoa ingeingia dosari.
“Ila una nini?. Sema mbona humaliziii?” alinikaripia kwa sauti.
“Unaumwa?” aliniuliza.
“Aaaa!, hata kidogo,” nilimjibu kwa sauti ya chini,
“Au…..penginenimekuudhi
bila mimi kufahamu…., maana mama husema mimi ni mkaidi na sijui namna
ya kumtunza mtu, ni kweli?” Getruda alizidi kunidadisi.
“Hapana” niliitikia kwa sauti ya majonzi.
“Oke, hivi ni kusema kwa sababu ya kazi ndio umenisogeza pembeni?”
“Hivyo ni vibaya mke wangu, nakuahidi nitajitahidi kukupa penzi nono!, ambalo litafuta kumbukumbu zote nilizo kukera”
“Kama sivyo, basi naomba unibusu, nijisikie furaha moyoni” mke wangu aliongea huku akinisogelea karibu zaidi.
Nilisita
kidogo kisha nikainamisha kichwa na uso kutokeza upande wa midomo yake
na kumbus kwa uvivu uvivu (Kigoigoi). Nilipomgusa tu midomo yake, mara
alinikumbatia vilivyo, kwa mikono yake na kuning’ang’ania na mabusu ya
mfululizo na muda mrefu na hata aliponiachia hilihisi joto lenye
uvuguvugu nikilikosa. Mwanzoni nilimbusu kwa wasi wasi na shingo upande,
lakini baadae nikaadhiriwa na mabusu motomoto ya Getruda nikajikuta
ashiki zikiwa zimesisimua mwili mzima, nilijibu mashambulizi kwa mabusu
ya nguvu huku nikihema roho juu juu.
Baada
ya mabusu yaliotuweka hali ya mapenzi, kwani ashiki zilimpanda na
kutaka penzi wakati huo huo bila kucheleweshwa. Akrabu ya saa ya ukutani
ilionyesha saa kumi na moja na nusu, karibu na kupambazuka. Majogoo
yalikuwa yakiwika kila kona ya wafugaji wa kuku.
“Mume wangu sikiliza” Getruda aliniambia, usoni macho yalikuwa yamelegea na kurembua rembua.
“Eee! Sema mama watoto” nilikohoa kinafiki na kusema.
“Karibu
kunapambazuka. Nataka uondoe mawazo ya biashara, madeni, sijue kazi
mawazo yako yote weka kuhusu penzi langu na wewe, naomba uniridhishe kwa
penzi motomoto.Kwani siku sitini sasa toka unioe
hujafanya tendo la ndoa na mimi. Hivyo leo ni mwisho, usipofanya tendo
la ndoa, talaka yangu naomba, siwezi kukaa kama pambo, katuni ndani ya
nyumba yako. Sijaja kukupikia hapa tumbo liende mbele, mimi sio kijakazi
wako, uelewe leo, mimi ni mkeo tena wa ndoa” Getruda alibadilika ghafla
na hakutaka kucheka na mimi, alikua anahitaji haki yake.
“Hayo
yote uliyosema nimeyatia akilini ila naomba unipe mu….” Kabla
sijamalizia maneno, nilikatishwana sauti ya ukali ya Getruda.
“Nikupe nini?, mbona sikuelewi?”
“Fahamu
kwamba ninahitaji kuwa na mtoto . Nataka nami niitwe mama Fulani, si
jina langu Getruda” Getruda alizidi kunifokea, nilishindwa kuelewa
ninani aliyekuwa ananitesa kiasi hicho.Niliwafikiria wabaya wangu wote
akilini sikupata aliyenitendea ushenzi huo.
“Ndio…”
niliitikia kwa sauti ndogo na ya huruma hata mimi mwenyewe sikuamini
ilitoka kwenye kinywa changu, wasi wasi ulinijaa moyoni, nilihisi
kuumbuka niliwalaumu wazazi walionitafutia mke. Laiti ningelijua kuwa
nina matatizo hayo nisinge Kubali kuoa.
“Haya
nenda ukazime taa basi basi mpenzi” Getruda alizidi kunifanya miguu
ilegee na kukosa nguvu ya kutembea, nafsi ilinyauka kama jani la tumbaku
lililosubiri kusagwa, jasho la woga lilinichuruzika. Sehemu ya kuzima
taa ilikuwa karibu kama hatua tatu lakini niliona umbali wa kilometer
ishirini.
Nilijikamua kikakamavu na kuinuka kwenye kitanda, kwa uvivu nikajongea kwenye
swichi ya taa. Kilikuwa kitendo cha sekunde tano lakini nilifanya
dakika saba.nilipofika kwenye swichi nilizima taa, mwili ulikuwa
ukitetemeka sio kwa baridi bali ni hofu juu ya kufanya tendo la mapenzi
na Mke wangu.
Nilitamani
kumfukuza mke wangu kwa kero nilizopata si usiku wala mchana, lakini
nilishindwa nianzie wapi na niishie wapi?. Licha ya kushindwa
kumfukuza,niliogopa siri ingefichuka na kila mwanadamu angenitupia jicho la lawama.
Nilibuni
haraka haraka mbinu za kuinusuru ndoa yangu,ili Mke wangu asigundue
matatizo niliyo nayo,nilirudi kitandani na kijisogeza ukutani mwa
kitanda,taratibu niliingiza vidole vya mkono wa kulia kwenye mkono
wangu,mwisho wa kinywa karibu na koromeo,na hazikupita sekunde
nane,nilitapika mfululizo. Sehemu ile ya ubavu wangu kwenye
kitanda.Niliamini kwa kufanya hivyo mke wangu angeanini kuwa mimi ni
mgonjwa. Lakini cha ajabu alianza kunivua nguo zangu badala ya kufikiri
njia ya kuondoa matapishi kitandani, alianza kunivua suruali. Alichoka
na maneno yangu ya kila siku nikilalamika, kuumwa,mara tumbo, kichomi,
kutapika, kichwa nk.
Baada
ya kunivua nguo, alivua na za kwake pia. “Maji ukiyavulia nguo huna
budi kuyaoga”alisema kwa sauti iliojaa hasira na mahaba. Mapigo ya moyo
wa Getruda yalianza kwenda kasi na mwili mzima ulisisimka baada ya
kunivua nguo zote.
“Leo
lazima, sijali kuumwa kwako au laa!,Kila siku unalalamika, tumbo,
kichomi, kutapika, mara uchovu, leo ni leo”. Taratibu alianza kunitomasa
wakati huo nilikuwa nimetulia kama yule mdudu kifaulongo na minong’ono
ya kuweweseka kama mgojwa niliendelea kuitoa.
“Mume wangu amka basi tufanye.” Getruda alinihimiza huku akiwa amenishika mkono wangu kidogo akininyanyua .
“Subiri kidogo naumwa na homa”
“Imekuwa homa leo” kwa kweli mke wangu alichoka na idadi ya magonjwa niliokuwa nikimtajia kila leo.
“Eti
homa, utashaa leo, sikusikilizi ninachotaka ni penzi tu, usiniletee
hadithi za riwaya, zile hadithi ndefu za kubuni, sizihitaji kabisa!,
wewe mwanaume gani? Hivyooo!” Getruda mke wangu alianza kunidharau baada
ya kuona sina lolote. Nilianza kulia nikilaumu ugonjwa ulioniingia
nikiwa na ndoa yangu, niliulaani ugonjwa huo nilitamani nikatwe vidole
kuliko kuwa na udhaifu wa nguvu za kiume. Kilio changu kilikuwa chungu
mwenye na roho yangu. Pamoja na kunywa dawa za mitishamba kutoka kwa wamasai aina ya mchuma mbele bado nizidi kupata mateso ya unyumba.
“Mke
wangu unadiriki kunikashifu. Kunitukana mtusi ya nguoni!, kweli
umenichoka” nilijaribu kumlaumu mke wangu, lakini haikusaidia kitu.
“Ndio,
nimekuchoka, naomba talaka yangu asubuhi hii hii, longolongo sitaki”
mke wangu alibadilika ghafla na kunitizama kwa hasira kali, kama
kungekuwa na uwezekano wa kuniadhibu basi angeniadhibu ipasavyo. Niliona
bila kuwa mpole ndoa ingekuwa ndoano, ingesambaratika na ningekuwa
mseja.
“Mke
wangu naomba upunguze jazba nikueleze…” niliongea kwa sauti ya unyonge
iliyona lengelenge la machozi kunitoka, nikiwa na wasiwasi mkubwa wa
kumkosa Getruda. Sikupenda niachane na Getruda mke niliyepewa na wazazi,
mke mwenye hali ya ubikira, ambaye hajawahi kuguswa.
“Nimeshachoka na mambo yako ya ajabu, unataka kunieleza nini?”
“Najua
utanichukia nikikueleza kilichonisibu pia hutaamini yaliyonikuta
mwenzio”. Niliongea machozi yakinilengalenga machoni, roho iliniuma na
kujiona nisiye na faida wala umuhimu kuishi duniani, nilitamani kufa
ilinisiendelee na mateso. Kilio changu kilikuwa cha huzuni mno!, moyo wa
huruma ukamuingia mke wangu, masikini akaniomba nimuelezee.
“Mume
wangu haya nielezee kilicho kusibu, usiogope kuwa wazi usinifiche
chochote kama kuna uwezekano nitakusaidia mpenzi” sauti ya mke wangu
niliisikia na kuifananisha na sauti ya malaika wa neema. Nikajikaza huku
nikiwa na churuzika machozi yaliyolowanisha kope machoni.
“Mke
wangu hujafa hujaumbika, nisikilize kama mtu asikilizavyo maneno ya
Mungu, nilikuwa kiwandani kwenye uchanganyaji wake Kemikali, bahati
mbaya kemikali yatindikali ilinidondokea kwenye ngozi karibu na uume
wangu na kunisababishia udhaifu mwilini, naomba usiniache mpenzi, naomba
unisamehe kama nimekukosea mpenzi, naamini nimekukosea. Sikuyataka bali
yametokea bahati mbaya” Niliongea uwongo uliofanana na ukweli, kadri
nilivyozungumza ndivyo nilivyozidi kulia, sikupenda kuongea uwongo bali
ilinibidi niongee uwongo mtupu ilikuinusuru ndoa na aibu yangu ,
sikumwangikiwa na tindikali, ni ugonjwa ulionitokea ambao sikujua
ulitokea wapi na nani aliyeniletea ugonjwa huo, je ni Jenipher au ni
nani?”
“Sasa
kama ulikuwa unajua unamatatizo kwanini ulinioa mpenzi?, unanitesa,
umepoteza muda wangu bure” Getruda alizidi kulalamika japo alinionea
huruma.
“Kumbe ndio maana kila siku ana lalamika na kunitajia magonjwa mengi yote hayo ni kukwepa…” Getruda aliwaza akilini.
“Mke
wangu matatizo yalitokea siku tatu kabla ya ndoa, wala sikujua
nimeadhirika na tindikali hiyo, ningejua ningehairisha kufunga ndoa ili
upate mume rijali” maneno yangu yalimuingia Getruda mke wangu na kuamini
kuwa ni kweli nilipata ajali ya kumwagikiwa na tindikali.
“Nitaishi
vipi bila kupata matunda ya ndoa, naomba uniambie nitaishi vipi?,
nitaishi hivi mpaka lini, sijawahi kukutana na mwanaume, nilitegemea
wewe ndiye ungevunja boma langu, sasa itakuwa vipi? Naomba mawazo yako”
macho ya huruma yalitua usoni mwangu, niliyekuwa nimetulia kama
mtuhumiwa aliyesubiri hukumu ya kunyongwa.
“Mke wangu hilo usitie shaka. Hakuna kinachoharibika nivumilie kidogo”
“Siwezi kukuvumilia tena mume wangu. Naomba talaka haraka”Nilitamani kuondoka , ikiwezekana kuihama nyumba yangu,nikifikiri jambo hilo lingenisaidia lakini nikajikuta nikikatisha mawazo na nafsi.Nilitulia kama sekunde kadhaa hivi nikijaribu kuganga maumivu.
“Uliapa
mbele ya mchungaji kwamba utaishi na mimi kwa uvumilivu…”Kabla
sijamalizia maneno yangu , nikakatishwa na sauti ya ukali .
“Ndio. Nimevumilia nimechoka, naomba uelewa kwamba namimi nina homoni”Getruda akasema akinitizama kama mtu alieniandalia tusi.
“Nataka niende nchi za nje kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi”
“Nchi gani?”
“Uingereza….” Nilipumua
kidogo kisha nikaendelea kumweleza, wakati huu nikimueleza, nilikuwa
siamini kwamba angeweza kulielewa lile nililotaka alifahamu na kulitii
“Getruda nakupenda na kiliwaahidi wazazi wangu nitaishi na wewe hadi
mungu atakapo chukua roho zetu”
“Sweedy unajua maana ya ndoa kweli?”Getruda akaniuliza akiwa amenitumbulia macho.
“Ndio”Nikajibu kwa sauti ndogo na ya upole kabisa,nikiwa nimeinamisha kicha kama kondoo.
“Kama
unajua maana yake.Mbona sioni nini maana ya ndoa kati yangu na
wewe?”Hapo nikavuta pumzi ndefu na kuziachia kwa nguvu,
“Ooooopphhhh”.Ikafikia wakati mwingine hata kujionea mwenyewe huruma.
“Si nishakuambia tatizo langu?”Nilizidi kutukutika moyoni.
“Basi kama unataka nisivunje ndoa yetu nitafutie ndugu yako aniridhishe kimapenzi mpaka utakapo pona”
“Sina ndugu yangu wakiume mke wangu.Kwa nini usiwe na subira?”Machozi sasa yakaanza kunidondoka kama maji ya dripu, nilihisi kudhulumiwa haki yangu , ingawa nilitaka njia ya amani kati yangu na mke wangu.
“Ngoja
ngoja yaumiza matumbo”nilimtizama Getruda, mke wangu nikagungua hakuwa
na nafasi tena ya kunisubiri. Macho yake tu, yalikuwa jawabu tosha
kwamba angeondoka kwenda kutafuta mume mwingine.
“Nasubiri
unijibu upesi, sitaki mzaha tena. Ushanipotezea muda mwingi sana
Sweedy”Sauti ya kupaza niliisikia ikigonga ngoma za masikio yangu,
nilijaribu kumtupia macho ya huruma,kuwa pengine angepunguza maneno.
Sikuweza kumjibu chochote,badala yake nikabaki kimya kama niliyeletewa
habari ya msiba wa ndugu yangu wa karibu.
“Dharau
yako itakuponza. Wala sitaki talaka yako.Naondoka, narudi kwetu mwili
wangu bado unaniruhusu kuolewa.Kama ni bikra bado ninayo kama ni kuzaa
ndio kabisaa.Kwanini nikose mume.Uzuri wangu tosha nishahidi kwamba
sitokaa kwetu mwezi bila kuolewa”Getruda aliongea na kunyanyuka kitini
ambako alielekea chumbani. Nilibaki nikimtizama bila kunena neno juu yetu.Sikutarajia kuona kile kilichopo mbele yangu wakati huo.Nilimuona Getruda akiwa kabeba begi kubwa languo akitoka nalo nje varandani.
“Mke
wangu tafadhali naomba uweke begi chini tuongee.Unapochukua uamuzi huo
si suluhisho. Ni busara kusuluhisha mgogoro ili kuhuisha uhusiano mwema
,tangu kuumbwa kwa familia hakuna hata moja isiyopata ubishi na mgogoro
ndani ya nyumba…..”nilivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu ,ni
dhahiri nilichoka kuitetea ndoa yangu isianguke.Wakati huo Getruda
alinitupia jicho, begi lake akiwa kalishikilia mkononi.Nikavuta hatua na
kumfikia karibu, nilimshika mkono nikijaribu kumbembeleza, “Tafadhali
usinishike.Muda wa kuishi nawewe umeisha.Mume gani usiye…”Nilimkatisha
maneno yake, “Ni samehe mke wangu,nitaendelea kukuita mke wangu kwa
sababu nakupenda, naomba uwe na subira. Unyumba nikuvumiliana, kuna leo
na kesho, kumbuka hujafa hujaumbika, jambo hili linaweza kukukuta hata
wewe,pengine ukapata ajali.Sikupenda kuwa hivi mpenzi…. hili ni jambo la
kawaida, muhimu ni jinsi ya kutatua mikwaruzo hii.Mfano ungekuwa wewe
mwenye matatizo haya ungelifanya nini?”
Niliongea taratibu na kwa busara nikijaribu kumshauri Getruda , mke wangu. Alivuta pumzi na kuzishusha.
“Naomba unipe uhuru.Utakubali niwe naingiza mume mwenzio ndani?”
“Hapana.
Utakuwa ni unyanyapaa wakijinsia.Getruda unataka kuniumiza moyo
wangu.Nakupenda na nimekuomba uwe na subira,pengine nimajaribu ya
mungu”Nilivumilia kulia ikashindikana,machozi yalinitoka bila
kutegemea.Nilitamani nibaki peke yangu ,ingawa sikuweza kuamini kama
kweli Getruda angenihifadhia siri yangu.Angeenda kuwaeleza nini wazazi
wake.Kuna mtu anaweza kuvunja ndoa bila kufarakana, migogoro ya
kiunyumba?.Mawazo hayo yalizidi kuniumiza na kunikera moyoni.
“Chagua
moja….”Alitulia , akalamba midomo yake kisha kunitizama kwa
dharau.Dharau hiyo niliigundua kwamba nikwa vile aliniona si lolote si
chochote kwake.
“Unasema unanipenda sana?”
“Kwani hujui hilo?”
“Sijui kwa sababu wewe mwenyewe hujanionyeshea upendo wako kwangu”
“Hivi umesema unanipenda vile?”
“Ndio…najua umekuwa wimbo”
“Naomba unichagulie maisha nitakayoishi kuanzia sasa”
“Basi nitakuacha uchague unachotaka mpenzi bora usinidhalilishe.”
“Sina chaguo lingine zaidi ya kunitafutia ndugu yako yeyote”Alisema tena akionekana siriasi.
“Kuna
rafiki yangu mpenzi ambaye tupo karibu .Yeye ndie mwandani wangu, siri
zangu ni zake na zake ni zangu nitamueleza kilio changu. Naamini
atakisikiliza na kulichukulia kama kilio chake na atanisaidia shida
ndogo ndogo za unyumba wetu. Mtu huyo ni tajiri yangu anayeitwa Mzee
Jophu. Itakubidi unihifadhie aibu hii moyoni mwako. Ndiye ambaye siku
ile ulivyoletwa na Baba niliwaacheni nae nikiwa na maongezi ya faragha
na Baba.” Nilijaribu kumueleza mke wangu kuwa pengine angekubali
kutembea na rafiki yangu mkubwa badalaya ndugu , na aendelee kinitunzia
heshima yangu kama mumewe. Japo roho ilikuwa inauma kumkabidhi mwenzangu
boma langu. Wala sikuweza kugundua kuwa mzee Jophu ndiye aliye panga na
Daktari anipige sindano ya sumu.
“Kama
una matatizo ndoa ya nini?.Suluhisho ni kuivunja ndoa kwa amani sitaki
kujidhalilisha kwani wanaume wameisha duniani? Isitoshe nilishakutaarifu
kwamba sijawahi kuguswa, bado nina nafasi kubwa
ya kuolewa, wameolewa machangudoa sembuse mimi kigoli. Siwezi kukuelewa
kabisa ninachotaka ni talaka yangu. Kuishi na wewe ni sawa na
kulinganisha kifo na usingizi” Mke wangu alinibadilikia ghafla, sikuweza
kuamini maneno hayo yaliyotoka kinywani mwake . Hali hiyo ilininyima
amani na kijikuta nikilia kama mtoto mchanga aliye hitaji ziwa la mama
yake baada ya kulikosa kutwa nzima bila kunyonya.
“
Sijali kulia kwako kwani mimi ndiye niliye kumwagia tindikali? Mlaumu
aliye kumwagia na sio mimi.Kweli ving’aavyo vyote si dhahabu. Najuta
kuolewa na watu waliochelewa kuoa, huenda ni matatizo uliokuwa nayo toka
zamani”. Getruda alizidi kuniumiza moyo.
“Sawa
najua sina faida ya kuishi duniani,nitawaachia ninyi wenyewe umuhimu na
hii dunia, lazima nife …….sio muda mrefu utaniita marehemu sio Sweedy
tena ,” Nilijikuta shetani mbaya akiniingia kichwani na kuiteka akili
yangu, nikaamua kujiua tu, sikupenda kuishi na mateso. Niliondoka na
kuingia chumbani kwetu, nilijifungia kwandani na kutafuta kamba tayari
kutoa uhai wangu. Nilikusudia kujiua na niliamua kufanya kama mawazo
yalivyo nituma, sikupenda kuishi kwa manyanyaso, mateso ya unyumba.
Nilikuwa
chumbani na tafuta kamba ya kujinyonga, Getruda, mke wangu muda mfupi
tu, angeniita marehemu badala ya Sweedy. Getruda akiwa kwenye mtiririko
wa mawazo alisikia sauti yangu, (LORD YOU KNOW MY TRIBLES)” “Mungu
unajua mateso yangu”Wakati nasema maneno yale ,nilishafunga kitanzi juu
ya paa la numba.Nilikuwa nimepanga stuli mbili zikiwa
zimebebana,nikaanza kuingiza shingo kitanzini,
nilihakikisha kamba haitakatika. Iliyofuatiwa sauti nyingine nikimuaga.
“Getuuuuu! Kwa heri niagie ndugu wote, nimeamua kufa sipotayari
kunyanyaswa na udhaifu wangu, hata mungu anajua”. Taratibu nilianza
kusukuma stuli nilioikanyaga ili idondoke na nijinyonge, Muomba kifo
hakosi basi stuli ilidondoka kamba ikaninyonga.
“Ahiiiii”nilitoa sauti moja kwa shida sana.Kutoa neno la zaidi,nilijijigeuza na nikawa natapatapa kama mfa maji.
“Haraka
Getu aliamka na kuekekea sauti ilipotoka, aliamini nilikuwa nianajiua
akajuta na kujilaumu kwanini alinipa maneno ya ukali badala ya
kunifariji.
“Dhambi zote ni mimi, isingekuwa mimi asingejiua, yanipasa nijitahidi kumnusuru na kifo,” Getu alianza kuniita
kwa sauti ya huruma, “Sweedy…Sweedy… naomba unisikilize mkeo naongea.
Niwie radhi nilikuwa na kutania nimekubali kuwa na rafiki yako. Naomba
unielewe mpenzi nitalitunza penzi lako na siri yako. Kama nikujiua basi
nisubiri tuongee nitakuacha uendelee kujiua.” Getu aliendelea kuniita
bila ya kupata kujibiwa. Kilikuwa kitendo cha haraka alichukua uamuzi wa
kuvunja mlango na kuingia ndani, alinikuta nikiwa nimeningia mapovu ya
kitoka puani.Aliona kisu kilichokuwa mezani,Hakupendakupoteza muda ,kwa
mwendo wa umeme alikata kamba na nikadondoka chini kama
gunia la maharage, aliponigusa alipeleka mkono kifuani kuona kama
nilikuwa hai. Ajabu ni kwamba hakusikia mapigo ya moyo ya kienda. Miguu
ndio ilikuwa nikiitupatupa huku na kule, ulimi ukiwa nje kama wa kenge.
Hali iliyomfanya asijidanganye kuwepo hai tena na kuamini zisingepita dakika kumi ningepoteza uhai.
Uzito
wangu haukuwa kigezo kikubwa cha kumfanya Getruda ashindwe kunibeba,
alijitahidi alivyo weza kunitoa nje ambako alipiga simu kwa dereva teksi
aliyemfahamu. Dakika takribani mbili ,alisikia gari likiegeshwa nje ya
jengo letu.
“Vipi shem. Imekuwa je?”Dereva teksi aliuliza.
“Wee achatu.Hebu tumuwahishe hospitali mazungumzo baadaye”
Walinibeba
juu juu hadi kwenye gari, dereva akafungua mlango wa nyuma ambako
walinilaza chali na kufunga mlango.Hawakukawia kufika hospitali ya rufaa
Mount meru kwa matibabu zaidi.Getruda aliniingiza ofisi ya dakitari wa zamu.
“Anasumbuliwa hasa na nini?”
“Amevamiwa
na majambazi ambao walimnyonga kwa kutumia kamba”Getruda alidanganya
wazi wazi.Huku akiuma mdomo wa chini kana kwamba alijawa na dhahabu
kali.
“Sasa umeripoti polisi?”
“Daktari mbona unaniuliza maswali ya sio na msingi kabisa.Wewe unataka ripoti ama kumtibu mgonjwa?”
“Hatuwezi kutibu bila kupokea karatasi ya PF3 kutoka polisi”
“Dokta kipi bora .Kuokoa maisha ya mgonjwa ama kumwacha afe kwa sababu ya PF3?”
“Kuokoa maisha yake”Dokta akajibu akichukua vipimo vyake.
“Basi kumbe unajua. PF3 baadae, nisamehe kama nimekuudhi”Getruda alimwomba radhi Dokta.
Dokta
alinishughulikia kwa haraka.Nilitibiwa kwa makini na baada ya saa nzima
nilipata ahuen.Ila kooni nilihisi maumivu kwa ndani.
**********
Zikawa zimepita Siku mbili toka nilipookolewa na Mke wangu,Getruda pale nilipokuwa najiua kifo cha taabu.
“Mume
wangu nilikuwa nikikutania . Tafadhali usijaribu kujiua tena.
Nimekubali mlete huyo rafiki yako leo nimuone kama sura yake ina tapisha
au laa!” Getruda hakupenda kufanya hivyo aliamua kukubali ili
kuninusuru kifo. Sauti ya Getruda ilipenyeza kwenye ngoma ya masikio
yangu fundo kali la sononeko liliingia moyoni.Nikajivuia kulia kwa nguvu
zote lakini nilijikuta machozi yakichuruzika taratibu bila kujua.
“Sawa mke wangu utamuona nitakapomleta jioni,” Ilikuwa asubuhi na mapema, majira ya saa moja na nusu.
“Mmmm! Lakini Getruda unanipenda.Isingekuwa wewe basi nilikuwa mfu”Nilimweleza Getruda.
“Kumbe unalijua.Mkojo ulishaanza kukutoka”
“Masihara hayo.Inamaana nilikikojolea kama mtoto”
“Ndio”Getruda alinijibu akainuka kitini na kuelekea kwenye jokofu ambako alilifungua na kunipatia Juisi baridi ya machungwa.
“Karibu mpenzi”
“Ahsante
mpenzi”Niliipokea na kumtolea tabasamu,lakini nilipokumbukla kwamaba
nahitajika kumtambulisha bosi wangu.Moyo ulisingaa na kunyauka kama jani
la tumbaku lililosubiri kusagwa.
“Mpenzi nataka kwenda kujipumzisha kidogo”
“Sawa,ila
usisahau kwenda kumleta rafiki yako jioni”Nilishituka na kutulia kama
sekunde kadhaa ,kisha nikageuka kumtizama mke wangu.
“Utaniamsha baada ya saa moja.
Ok,
bye”Nilijikaza kutoa tabasamu ambalo pengine lilionekana dhahiri la
kulazimisha, huku moyo ukiniuma kama kutu inavyokula chuma taratibu na
kukiozesha chote.
“Nije tujipumzishe wote?”Getruda alinieleza wakati nikiwa nimempa mgongo.
“Poa. Ukipenda”Nilimjibu damu zikienda mbio ,ungeweza kuhisi nimekimbia umbali mrefu bila kupumzika.
Getruda alinifuata chumbani kama alivyoomba.Nilijitupa
kitandani kiuvivu uvivu nae akajibweteka kwenye sofa moja lililomo
chumbani.Ingawa nilifumba macho lakini sikuwa hata na lepe la usingizi,
mawazo yangu yalimezwa na taswira ya maisha ya unyumba.Nilijiuliza bila
kupata jawabu sahihi kwamba ugonjwa huwa niliupata wapi na nani
aliyenipa?.
Nikiwa
nimelala nilihisi vidole laini zikitalii mwilini mwangu.Hata hivyo
sikushituka kwani nilihiosi alikuwa mke wangu.Vidole hivi vilizunguka
huku na kule bila kupumua,nilihisi kama kero ama mdudu fulani
akinitembelea akini kwarua. Sikuona raha zaidi za mateso tu.
“Hallo Sweedy”
“Na..a.amu”Nilikokoteza maneno,nikiwa nimetulia utadhani mbwa anayetolewa kupe.
“Unanipenda?”
“Saaana tu”
“Kwanini hunipi haki yangu kama kweli unanipenda?”
“Haki ipi?.Si una jua matatizo yangu sasa unataka nini tena”
Nilihisi Getruda akinitibua akili yangu.Niliinukla na kutoka nje.
“Getruda unanitesa. Tumepanga nini na wewe unataka nini?”
Nilitulia
kidogo nikaendelea, “Moyo wangu unasononeka sana. Laiti ningelijua
nisingeoa, maisha gani haya yananitesa kiasi hiki?”Nilijikuta nikilia
ovyo kama toto jinga lenye kudeka ovyo.Kilio changu lilikuwa rohoni.na
aliyejua alikuwa muumba pekee.Getruda alikuja kunibembeleza kwa hofu
kwamba ningechukua maamuzi ya kijinga tena. Aliniandalia chakula
mezani.Tulisali kisha tukala .
Saa
nane mchana baada ya kupata mlo wa mchana nilimuaga Getruda nikiwa
naelekea ofisini kumueleza Mzee Jophu yaliyosibu katika unyumba wangu.
Lakini cha kushangaza Mzee Jophu baada ya
kumueleza kila kitu,nilimuona uso ukiwa umejawa furaha badala ya
kunionea huruma. Hali hiyo aliisubiri kwa hamu hata hivyo alishanga kuona mimi kuchelewa kumuelezea shida zangu toka mwanzoni.Alijifanya kama hataki kuchangia mapenzi ilinimuone mtu mwema,
“Sasa Jophu unakataa nini na wakati nimekuambia mke wangu hajaguswa”
“Inamaana siku zote hizo mlikuwa mkilala tu?”
“Ndio”nilimjibu nikahisi machozi yakinilengalenga, hata hivyo nilijikaza kiume.
“Matatizo haya yalikupata muda gani?”
“Siku ya kwanza toka nifunge ndoa na mke wangu”
“Usinitanie Sweedy. Ulijaribu kwenda hospitali?”
“Ndio.Nilichunguzwa
kwa makini.Daktari alinieleza kwamba nilipigwa sindano yenye
sumu.Nilikataa kwani sijawahi kupigwa sindando yeyote toka uliponiajiri.
Na sasa ni miaka karibu ishirini na tano. Nakumbuka sindano ya mwisho
nilichomwa nikiwa na chuoni. Na siku nyingine niile nilipokuja kutolewa damu”
“Kutolewa damu si kupigwa sindano labda una matatizo mengine kiafya.Vipi kuhusu chango?”
“Sina chango,mzee”Nilimjibu nikiwa nimetizama chini.
“Mzee,
naomba unisaidie kuokoa jahazi la ndoa yangu”Nilimweleza nikimpigia
magoti.Sikuwa najua kwamba mzee Jophu ndiye aliyetuma watu wanipige
sindano ya kuua uume wangu.Wakidai wana nitoa damu ilinikapimwe virusi
vya ukimwi.Hata hivyo ilikuwa kazi kumgundua mbaya wangu,jinsi
alivyoonyesha kutokutaka kuchukua jukumu la kumridhisha mke wangu.
“Mkeo atakubali kwenda kupima damu zetu?”
“Sina uhakika kama atakubali au laa. Ni vizuri kimpigie simu”Nilitoa simu yangu ya kiganjani na kubonyeza namba za Getruda, mke wangu.
“Hallo, mpenzi”alipokea tu baada ya kuona namba zangu juu ya kioo cha simu yake.
“Oooo!, vipi upo salama.”
“Ndio. Sijui wewe”
“Shwari kabisa.Mmmm…utakubali kupima Virusi vya ukimwi?”
“Tangu lini kigori akawa na Ukimwi?”
“Sijambo la ajabu kwani ukimwi unaambukizwa kwa kujamiana tu?”Getruda aitafakari akajiona kweli alibugi sana.
“Sawa, nimekubali kupima afya kwa manufaa yetu sote”
“Ok, jiandae nakuja sasa hivi nyumbani”
“Ok, bye bye”Alinaga na kukatasimu.
“Nilimtizama mzee Jophu na kumwambia, “Amekubali kupima”
Kwambali niliona tabasamu la mzee Jophu lililonifanya nione meno yake ya rangi rangi, nafikiri kutokana kunywa maji ya Arusha tokea utotoni mwake.
“Sasa
Sweedy”Alitulia kidogo na kukohoa kinafiki,nilimtizama kwa makini
niwezekujua alichotaka kusema,aliendelea “Kwa vile wewe ni rafiki yangu
sina budi kukusaidia.Ila nakuomba usimweleze mtu yeyote ‘Especial my
wife’,Umenielewa. Narudia tena naomba iwe siri moyoni mwetu”
“Sawa, mzee.Usihofu kitu”nilimjibu kwa upole kabisa.
Mzee
Jophu aliongea moyoni akiwa amejawa furaha kubwa mno, “Kile
nilichokitaka kimekamilika. Sasa kazi kwangu kurina asali nitakavyo””
Mzee
Jophu kunajambo la muhimu nimelikumbuka. Nilimdanganya kuwa
nilimwagikiwa na tindikali. Akikuuleza mueleze ni kweli”Nilitulia
kidogo, ingawa alijaribu kuficha furaha niliiona , Nikatulia kama
niliyewaza kitu ,Machozi yakaniwakia pale nilipokumbuka nguvu zangu
nilipokuwa Nchini Thailand “Lakini boss na shindwa kujua ugonjwa huu
niliupata wapi na nani aliyeniletea”
“Usijali
muombe mungu akuondolee. Hatamimi ninafanya tu, kwa vile wewe rafiki
yangu wa damdam, lakini kwa maulana ni dhambi kuzini nje ya ndoa,” Mzee
Jophu aliongea ilinimuone mtu wa busara kama alivyoonekana kuwa
ni mtu wa busara kumbe ni muungwana wa ngozi tu, lakini rohoni ni
muuwaji. Maneno yake ilikuwa vigumu kumgundua kuwa yeye ndiye mbaya
wangu, aliyeamua kunitesa iliamfanye mke wangu wake.
Mazungumzo
yetu ya ofisi yalikuwa ya muda mrefu. Tulipo maliza jioni iliwadia
tuliongozana na Mzee Jophu moja kwa moja hadi nyumbani kwangu.
“Lakini Sweedy kama ameoa mke mwenye uso wa mbuzi mimi sitamkubali atakuwa wako mwenyewe”
“ Hakika mke wangu utamkubali. Amekamilika kila idara. Utamsahau mama Jacob nakuambia” Nilimueleza.
“Yote tisa, kumi tutaona. Nitaamini unajua kuchagua,”
“Lako
jicho, yanini ni kusifie?” Niliposema, nilitamani Mzee Jophu ardhike na
ombo la Getruda, lakini kitu kilichoniuma zaidi ni jinsi gani
ningemuunganisha mwanaume mwenzangu na mke wangu niliyemlipia mahari.
“Inawezekana huyu mshenzi akamkataa mke wangu. Midomo yake imejaa dharau”nilijisemea kimoyomoyo huku nikibonyeza kitufe cha geti.
Getruda
Kimario alifika getini na kufungua, mtu wa kwanza kuingia akiwa Mzee
Jophu.Shauku yake haikufichika ,alimtupia Getruda jicho la lilo jaa
ubembe.Ni hapo ndipo nilipohisi Mzee Jophu kumkubali mke wangu. Alikuwa
na shauku ya kumbusu Getruda, nikipindi kirefu toka wapoteane pale
ofisini kwake, na Getruda alimkumbuka kuwa yule alikuwa yule aliyempa
mama yake mzazi shilingi laki tano za kitanzania iliamuowe yeye.
Walitupiana macho yaliyojaa furaha macho ya matamanio ya Getruda
yalizidi kumchanganya Jophu. Aliyekuwa na shauku kuupitisha usiku
mwanana na binti aliyemlipia shilingi laki tano. Aliamini alikuwa na
haki yakujivinjari jasho lake.
Mwanzoni nilihisi hawakumbukani,kumbe kumbukumbu alikuwa nazo na alishuhudia mama yake akipokea hizo hela.
Ulifikia
muda muafaka wakuweka mambo hadharani ili nitatuliwe shidayangu. Kabla
sijazungumza chochote nilipandisha pumzi na kushusha kwa nguvu kama mtu
aliyechoka na pilika pilika za kutwa nzima
,”ooooooophhhh!”Kisha nikasema kwa sauti ya chini kama mgonjwa,ni kweli
niliyotaka kusema yaliniuma sana.
“
Nafikiri mke wangu nilisha wahi kukutajia jina la rafiki yangu kipenzi.
Ila ni vema nikalirudia leo ukiwa una muona . Aliye kaa hapa mbele
ndiye Mzee Jophu. Sio Mzee kweli ni kwaajili ya mali zake ndio maana
watu wanampa jina la heshima ya mzee. Huyu ndiye
mwa ndani wangu ukimuona yeye ndio umeniona mimi. Shida zake ni zangu,
zangu ni zake,”Nilikohoa kidogo ni kumgeukia mzee Jophu. Kijasho
kilizidi kuchuruzika kwa kasi kuliko mwanzoni, nilihisi midomo kufa
ganzi na kuwa mizito, nilijikuta sauti ikipotea ghafla pale
nilipofikiria kumuachia mzee Jophu mke wangu.Tena hajawahi kuguswa na
mtu yeyeto maishani. Kwa kweli inatia uchungu sana heri ningekuwa nimezaliwa na udhaifu huo kuliko kunikuta nikiwa mtu mzima.
“Mzee
Jophu huyu ni mke wangu, kwa upande mwingine naweza kusema ni mkeo.
Nina matatizo ya,,,,,,” hasira kali iliniingia moyo nikashindwa
kumaliza, nilijikuta nikiangua kilio. Moyo uliuma sana.
“Kweli
kweli na muachia Jophu kigoli wangu?”Nilimtizama Getruda kama vile
nikimuaga, sikuweza kukwepa jambo hilo tena.Kwa kuwa lilishakuwa kero
katika familia yetu.
“Naomba
uwe karibu na mke wangu, kama ulivyo karibu na mkeo,
lakini,,,,,,,,,,naomba unifichie siri yangu, heshima iwepo msije
mkachukulia muda huo kunidharau, nami sikupenda kuwa
hivi,,,”Nilikokoteza maneno kwa ujasiri .
“Ok,
nashukuru kumfahamu mkeo, na nitaendelea kumfahamu vizuri, zaidi kadri
siku zinavyo zidi kwenda” Mzee Jophu aliongea huku akinyanyuka kuelekea
alipo Getruda. Alinishika mkono na kuunyanyua usawa wa midomo yake,
hakuchelewa nilisikia sauti ya busu kwenye kiganja cha mke wake wangu.
Busu hilo lilimchanganya mke wangu na kujikuta mwili ukimsisimka,
vinyweleo na nywele zilisimama kwa shoti ya busu la mzee Jophu.Nilibaki
nimeduwa, midomo ikiwa wazi kama sekunde kadhaa.Bila hofu wala haya,
walijikuta wamekumbatiana na Mzee Jophu alisogeza midomo yake karibu
kabisa na sikio akimnong’oneza.
“Kweli
kwenye miti hakuna wajenzi, nitakutunza kama mlima Kilimanajaro
unavyotunza Seluji yake, nitakupa chochote unachotaka, ikiwezekana
nitakuoa kabisa, nakupenda siko tayari kukuacha, naamini unanipenda”
Sauti ya Mzee Jophu ilizidi kumtekenya Getruda, alijikuta akitikisa
kichwa ishara ya kukubali.Alishindwa kujizuia kutoa sauti za kizizima,
taratibu kwa jinsi maneno ya Jophu yaliyokuwa yakipenyeza sikioni angali yana uvuguvugu, kwa wimbi lenye joto nadhifu.Mzee Jophu alimwachia na kuketi karibu nae.
Mambo
yote niliyaona. Kwa jinsi roho ilivyoguguna niliondoka sehemu ile na
kuingi chumbani, nilimpenda sana mke wangu, sikupenda awe mke wa shirika
wala sikupenda kuona akishikwa shikwa na mtu zaidi yangu. Japo nilikuwa
na wivu lakini nilishindwa kwa sababu nilipata udhaifu, ikanilazimu
kuvumilia na kuhamisha macho, na kutizama pembeni.Pia hilo lilinishinda nikaamua kujiondokea kiunyonge kama kifaranga asiye na mama.
Kuondoka kwangu, ulikuwa mwanya wa Jophu na mke wangu kupanga mambo yao.
“Oke nimeamini umeumbika sawa, kama asingekuwa Sweedy basi ningekuoa mimi. Bado sija chelewa. Nina nafasi kubwa ya kukuoa”Huo ndio ulikuwa mwanzo wa usaliti wa ndoa.
“Hata mimi nakiri umbo lako ni zuri na lakuvutia. Najuta kuolewa na huyu mchovu asiye na umuhimu wowote ndani ya ndoa”
Mzee
Jophu alidakia “Ni kweli, sio vyote ving’aavyo dhahabu. Vingine
aluminiamu ama bati,”alitulia kidogo na kumkodolea macho yaliyojaa
ubembe, kisha akanyanyua mkono wa Getruda na kumbusu kiganjani, akakohoa
kidogo na kusema “Sawa, tupange tukutane wapi?”Ilikuwa ni sauti ya
nzito ya Jophu ikinguruma varandani kwangu.
“Mimi
naona tukutane Hoteli yake Sweedy mwenyewe, pale sea breez inn hotel
ili tuwaonyeshe watu na hata wafanyakazi wake kuwa Sweedy ni dhaifu”Mke
wangu alianza dharau akitaka wakutane kwenye hotel yangu, ili kunidhalilisha.
“Kesho
saa kumi jioni, nafikiri utakuwa muda muafaka wa kujipumzisha,”Getruda
alizungumza huku akimtolea Jophu macho ya kurembua na ya unyenyekevu.
“Aaaa!, kesho mbali. Ok kumbe saa hizo karibu giza. Sawa usikose mpenzi”Walipigana mabusu ya kuagana na Mzee Jophu alimalizia .
“Niote njozi njema usiku. Tena zilizo jaa mahaba”
“Usijali mpenzi, zote nzuri zitakuwa juu yako”Mzee Jophu alitoka na mke wangu alirudi na kunifuata kule chumbani, kwa kusema kweli moyo wangu ulipata sononeko la roho, nilibaki nikiyaganga maumivu ya moyoni.
Walipanga
sehemu ya kukutana bila ya kukosa, wote walikuwa na shauku moja.
Ilikuwa jioni tulivu watu walikuwa wana kunywa na kula. Alionekana Mzee
Jophu akiingia na mke wangu SEA BREEZ INN HOTEL. Waliongozana hadi
mapokezi, na kuandika jina la kunikashfu kwenye kitabu cha wageni, bila
aibu mbele ya wafanyakazi wangu. Hata kama walifanya hivyo wasingefanya
kwenye hoteli yangu, wangeenda sehemu wasio julikana.Yote walionifanyia ni kunidhalilisha.
“Jina
tuandike nani Mzee” muhudumu aliongea kwa wasiwasi, baada ya kumwona
mke wangu, ambaye alikuwa kama bosi wake.Mzee Jophu aligeuza shingo
kumtizama Getruda, Kabla hajajibu kitu mke wangu alidakia “Andika Sweedy
dhaifu”
“Hapana bosi, anatakiwa kuandika jina lake kamili .Hilo sio jina kamili” aliongea kwa sauti ya chini huku akitetemeka. Alihisi mawili, kupokea tusi ama kibao.
“Sio jina kamili.Unafahamu jina lake?”
“Sifahamu”
“Kama hufahamu , mbona unasema si jina lake kamili?”Yule kijana akaanza kutizama chini kwa hofu.
“Nimekuambia uandike jina nililokutajia,upesi”
“Mama .Siwezi kuandika jina hilo”
“Wee,
mpumbavu nini!.Nimekuambia andika, kama hutaki huna kazi. Fungasha
virago uondoke,”Getruda alizidi kumuamrisha sambamba na kidole
alichoelekeza jichoni.
Ilimbidi
akubaliane na matakwa ya bosi wake, kwa kuwa hakuwa na sauti na alijua
Getruda ni mke wangu, asingefanya hivyo kibarua kingeota nyasi
haraka.Walichukua chumba, kila aina ya vinywaji viliingizwa
chumbani humo bila ya aibu.Kijana alishindwa kuvumilia yote
aliyoyaona.Aliumia rohoni na kuona kama yaliyotendwa alitendewa
yeye.Hakupenda kuona mke wa tajiri yake akifanya mambo ya kishenzi, tena
ofisini kwake bila aibu.
Chumba
changu kilijaa utulivu uliovunjwa na muziki wa taratibu uliosikika
redioni.Nilikuwa nimejipumzisha kitandani chali, nikiwa nasikilisa
mwambao ambao uliniwezesha kusikia mtu ambaye angeponyeza kitufe cha
kengele getini. Mawazo yangu yalilenga matatizo yaliokabili mwilini
mwangu.Hasa gonjwa ambalo limenifanya nimruhusu mke wangu awe na bosi
wangu. Mara simu ilianza kuita,nilishituka na kutizama mahala
nilipoiweka.Nilipoiona, nikanyoosha mkono kwenye droo ya kitanda na
kuiokota upesi.Sikutizama hata kwenye kioo kuona namba za
aliyepiga,niliipokea mara moja na kuipeleka sikioni.
“Hallo Sweedy hapa. Nani mwenzangu?”
Nilisikia
upande wa pili ukijibu kwa kuhemea juu juu.“Mimi John naongea, Mzee
nimemuona mama amechukua chumba yupo na Mzee mmoja, ameandika jina la
mgeni Sweedy dhaifu” sauti ya John iliingia lakini hata hivyo nilihisi
masikio kuchuja herufi.Nilishituka na kubaki mdomo wazi nikiwa nimetoa
macho kwa mshangaa mkubwa.Nilihisi mapigo ya moyo yakienda kasi zaidi.
“Umesema umemuona mke wangu wapi?”
Sikuamini nilirudia kwa ukali kidogo.
“Hapa hotelini kwako,mzee”
“Khaa,nisubiri nakuja.Wala usiwashitue”
“Sawa,mzee”
Nilikata
simu kwa ghadhabu kali.Sikupenda kupoteza muda, nilichukua bastola na
kuificha kibindoni. Nilifungua mlango kwa upesi na kutoka varandani,
nilionekana kuchanganyikiwa .Nilipofika varandani nikajikuta sikuwa
nimevaa viatu.Ndipo niliporudi kuvaa.Nikiwa nje ya jengo ,nilimpigia
simu dereva wa teksi niliyefahamiana nae aje kunichukua.Haikuchukua muda
, niliona gari jeupe lililo pigwa msitari mweusi katikati likiegeshwa
nje kwangu,nilitambua ni gari la bwana Jangala, yule dereva mashuhuri wa
teksi pale soko kuu Arusha.
“Bw.Jangala naomba unifikishe hotelini kwangu.Nimesahau kidogo,hivi nikiasi gani?”
“Mzee,umsahaulifu kweli.Unaonekana mwenye mawazo mengi.Kutoka hapa njiro mpaka pale Sakina ni sh,elfu tano tu,mzee”
“Hakuna tabu.Washagari twende.Samahani nina haraka,hivyo ikakupasa kutembea mwendo wa kasi”
“Sawa,
mteja kwangu ni mtukufu”Jangala alisema akikanyaga mafuta, wakati huo
gari likizunguka ‘Kiplefti’ ya kwanza kutoka kijenge juu.Nilielekea moja
kwa moja ilikushuhudia uzalilishaji.
“Ama
zangu ama zao, heri niwaue nami nife”Nilitulia kidogo nikitafakari
,nimbinu gani nitumie ilikuwa kuwanasa wote kwa mpigo.Yaani kumkabidhi
Jophu imekuwa nongwa.Ajabu ni kwamba hazijapita hata siku mbili
ananidhalilisha? Kweli rafiki mkia wa fisi.
***********
Nilionekana
kuchanganyikiwa badala ya kuingia chumbani nilijikuta naingia chooni
nilistuka ndipo akili ilipo rejea vema. Nilichomoa bastola yangu na
kuelekezea mbela tayari kwa vitachumba walichochukua kilikuwa cha mwisho
kabisa. Nilipokaribia chumba, nilisikia sauti za kilio kikubwa chumbani
humo.
“Oooooo! Jophu unaniumiza unaniua jamani!niachecheeeee!…nakufa!”Sauti ilikuwa nzito ilioitikia
“Tulia
mpenzi niku………kuku…….tengeneze.Unana……najua….wewe ..ni mzuri sana
lazima nikuoe”Mzee Jophu alikokoteza maneno kwa kigugumizi kikali akiwa
kifuani mwa Getruda.
Sauti
hiyo ilinilegeza viungo,nikajikuta kuishiwa na nguvu.Machozi yalianza
kuchururuzika kwa kasi nilijaribu kuyafuta kwa leso lakini bado haya
kukoma.Nilipitisha mkono kuhakikisha kwenye mpini wa bastola kuhakikisha
kwamba ipo.Nilipoigusa nikahisi ipo,nikaitoa na kuitizama kwa uchungu
sana.Nikasogeza risasi kwanye kifyatuo cha kuruhusu itoke,ilipoitikia
‘Katan’g..katan’g’Nilitikisa kichwa kwa fuhara ya kukusudia kufanya lile
nililofikiri kulifanya kwa wakati huo.Nilitembea kwa hadhari mpaka
dirishani walimo Getruda na Mzee Jophu.Nilijaribu kuchungulia lakini
sikufanikiwa kuona ndani kwakuwa kulikuwa na pazia nzito.Lakini kwa
kelele zile ,nilifikiri nikipiga risasi kwa kuhisi ningewaua kwa
pamoja.Nilipozidi kusikiliza kelele zao ,niligundua walikuwa karibu na
lile dirisha niliposimama.Niliuelekeza mdomo wa bastola yangu aina ya G3
rafles dirishani.Nikaingiza kidole ambacho nilitegemea kuwaulia .Kabla
sijafyatua risasi,nilishikwa mkono na mtu aliyekuwa nyuma yangu.
“Kaka usiwaue.Utajiingiza matatani bure.Nenda kapumzike nyumbani,hasira hasara kaka”
Mtu
huyo alinisihi akiwa ameing’ang’ania bastola.Kwanza aliniomba nitoe
risasi zote zilizomo ndani ya bastola.Nilipofikiri nikaona hakukuwa na
ulazima wa kubishana nae.Nilizitoa,akasema “Kaka naomba unipatie hizo
risasi .Najua unahasira unaweza kufanya lolote”Nilimpatia nikijua kama
ni kujiua basi naweza kutumia njia nyingine.Nilipompatia alizihifadhi
mfukloni mwake. Kila nilipofikiria, niliona kuwa sio suluhisho heri kufa
mimi kwa aibu niliondoka eneo lile, wahudumu walikusanyika wakinitazama
kwa huruma, wengine waliniomba niende niachane nao.
Waliendelea
kuvuta raha na wote waliyafurahia mapenzi yao, hasa Getruda aliamini
amepata mwanaume bora, ambaye asingemdhulumu haki ya unyumba. Alitumaini
na alitamani kuzaa na mzee Jophu ili kuondoa maneno ya mtaani kuwa ni
mgumba, alitegemea msaada mkubwa na juhudi za Mzee Jophu ili naye aitwe
mama.
Niliona Dunia chungu mithili ya shubira, kila nilipo kumbuka maneno ya Getruda na Mzee Jophu nilitamani nisitishe uhai wangu, sikuwa njia nyingine ya kuwepuka aibu ile, wakati na waza nafasi nyingine ilininyima kufanya uamuzi
huo na kunitaka niwe na subira. Niliamua kunywa pombe ili kupunguza
mawazo lakini mawazo yalizidi kutawala ubongo wangu kadri nilivyokunywa,
niliamua kusitisha kilevi, Sononeko liliendelea kunitawala, nikajiona
ni mtu dhaifu kuliko watu dhaifu wote duniani. Muda mwingine nilijaribu
kufariji kuwa ipo siku mungu atasikia kilio changu na kunipa nguvu za
ajabu,Maneno, “MUNGU UNAJUA MATESO YANGU” yakawa gumzo akilini kila
siku.
“Yaani
mke wangu ananidhalilisha kiasi hiki? Kweli yote haya ni kwasababu ya
udhaifu wangu,naamini mungu atasikia kilio cha mja wake na ataniponya
gonjwa hili na kunipa nguvu ili kuinusuru ndoa yangu
isivunjike”Niliongea huku nikiwa nimefumba macho, kichwa nikiwa
nimekiinamisha, kikiwa kina saidiwa kushikiliwa na viganja vya mikono.
Pamoja
na mawazo, hasira za kudhalilishwa. Bado nilikuwa na mpenda mke wangu,
nilimsubiri aje tukajipumzisha chumbani na kuongea utofauti
uliojitokeza. Kila nilipotizama saa ya ukutani,
niliona mshale kama unaenda mbele na kurudi nyuma, hali ile iliniadhiri
kisaikolojia. Nilikuwa nikiingia chumbani na kutoka, chooni na kutoka
bila kufanya chochote. Nilitamani kulala lakini sikupata hata tepe la
usingizi. Nilijikuta kutomlaumu tena mke wangu,kwani yote ni kwa sababu
sikuweza kumtimizia haki yake, nafsi nyingiune ilipinga na kusema
“Matendo aliyofanya ni ukosefu wa adabu na kutoheshimu unyumba, kwanini asifanye siri?”.Kila nilipokumbuka macho yalijaa machozi.
*****************
Ulikuwa
usiku wa saa sita na nusu, usiku mzito,Mwezi ukiwa umefunikwa na wingu
zito na ukungu mkubwa ukiwa mbele yake, mwili wake ulionekana kuchoka
mno!,akiwa anachechemea,mwendo ambao ulikuwa tofauti toka
kumuoa.Alinyanyua mkono sambamba na jiwe alilookota na kuanza kugonga
mlango kwa kishindo.Sikugonga tu pia kinywa chake kilipayuka maneno
machafu bila kujali alionitende.
“Wewe
mlinda nyumba umelala au upo macho?. Katika wasio na faida mmojawapo ni
wewe,wajanja wameondoa boma la mapenzi. Wewe unafananishwa na shoga,
mlinda nyumba. Funguaaaa”
Dharau
na maneno ya kashfa niliyasikia kwa usikivu wa masikio yote mawili,
maneno yalikuwa angali ya moto, nilihisi homa kali ikinitetemesha mwili,
nafsi ikakata tama ya kuishi kwa maisha ya manyanyaso, udhalilishaji na
matusi.
Nilifikiria
na kumfungulia mlango na kumuamuru aingie ndani, Getruda aliingia kwa
miondoko ya maringo huku akivumilia maumivu aliyoyasikia kwenye via vya
uzazi. Macho ya dharau yalinitizama kuanzia unyayo hadi kichwani na
kunipindulia midomo iliyojaa dharau kem! Kem!, hakuishia hapo alinisonya
na kutema mate pembeni, akijifanya anasikia kinyaa kunitizama.
“Mambo
baba wa nyumba”, akimaanisha mimi ni kama mlinzi wa kulinda nyumba,
sina mamlaka na penzi lake wala siwezi kutia neno kuhusu kuchelewa kwake
kufika nyumbani.
Niliitikia
salamu yake kwa shingo upande, sikupenda kumuudhi mke wangu, nilitambua
jinsi gani mtu anavyoumia pindi apatapo sononeko la roho. Kwa sauti ya
chini na ya upweke, hasira ikiwa imenikaba kooni.
“Mke
wangu umetoka wapi saa hizi, na ulikuwa unafanya nini?” Nilijizuia ili
mke wangu asijue kuwa nilikuwa na hasira, hata hivyo nilishindwa
kujizuia kulia, mwili mzima ulitetemeka, macho yakabadilika rangi kuwa
mekundu.
“Nimetoka
SEA BREEZ INN HOTEL kukagua mahesabu ya leo”. Getruda alijaribu kuongea
uwongo mtupu!, bila kupepesa macho, mboni wala kope za macho, macho
maangavu yasio na siri hata chembe.
“Nakubali
umetoka SEABREEZ INN, lakini sio kukagua mahesabu, bali umeenda kwa
mambo ya ufuska.” Hasira ilizidi kupanda kila nilipomtizama, mwili
ulizidi kutuna kwa hasira na jasho lilitoka kila sehemu yenye vitobo vya
vinyweleo mwilini.
“Hapana
mume wangu sikuwa nafanya ufuska” maneno yake yalinichanganya, nikaamua
kuchukua uamuzi ambao haukuwa akilini, niliamua kumuua mke wangu na
nilikuwa na sababu za kumuua, sikuwa tayari kutupiwa jicho na jamii kwa
udhaifu wangu.
Nilitoka
nilipokuwa, nikaingia ndani upesi, sikupenda kupoteza muda niliokota
jambia lenye makali kila upande, lenye kuwaka waka hata gizani,
nililitizama na kuamini kwamba ningelipitisha mara moja ningeachanisha
kichwa na kiwiliwili cha Getruda.
“Hakuna tena kumuuliza. Sio matangazo ya vifo.Nikifika ni kuachanisha kichwa chake”. Niliondoka nikimfuata alipo.
“Lazima nimuue Malaya huyu.Tukose wote, siwezi kujiua lazima nimuue leo leo”.
Nilipofungua
mlango, aliniona nikiwa na jambia lenye makali, aliamini kunusurika na
kifo ni asilimia mbili na zilobaki zilikuwa kifo, hapakuwa na upenyo
wowote wa kukimbilia kujinasua na mauti, “Haaaa!” Alihamaki na kujikuta anapiga kelele za kuomba msamaha.Ili nisitishe zoezi la kumuua bila mafanikio yoyote, sana sana niliongeza mwendo nikimfuata, jambia nikiwa nimeliinua juu tayari kutawanyisha shingo na kiwiliwili.
“Mume
wangu naomba unipe nafasi ya mwisho nikueleze yote yaliyotokea. Naomba
unisamehe usitoe uhai wangu, naamini utaridhika na matokeo. Kumbuka kuna
Mungu nae anayaona unayotaka kunifanyia” aliendelea kulia, akiomba
msamaha huku akirudi kinyume nyume taratibu.
Nilikusudia kumuua na sura yangu ilibadilika na kuonyesha dalili za kuua tu!, moyo wa huruma uliondoka; kwania ya
kumchinja kama kuku anavyochinjwa na kisu chenye makali. Nilizidi
kumfuata alivyokuwa anarudi nyuma, hasira ilitawala machoni. Ilikuwa si
rahisi kumsamehe kamwe!. Wakati Getruda anarudi
nyuma aliikwaa kwa nyuma na kudondoka chini kwa chali, hakuwa na njia
nyingine ya kujinasua na mauti, aliamua kusubiri mauti yamfike.
Nililikamata
jambia vizuri kwenye mpini wake kwa mikono miwili.Kitendo
chakutakakulishusha Getruda alishituka na kuzirai pale pale, aligeuza
macho, nilisitisha kumuua.Nilitaka kumuua akiwa na nguvu zake zote na
nilitaka afe kifo cha mateso.Nikaweka jambia pembeni na kuinama
kuhakikisha kama alizirai kweli ama ilikuwa janja ya
nyani.Niliposikilizia mapigo yake ya moyo yalikuwa mbali sana. Sikutaka kumpeleka hata hospitali nilitaka afe mwenyewe, si tena kumtibu, nilimchukia Getruda kwa mambo aliyonitendea.
Nililiokotajambia
langu nakulirudisha chumbani.Nilimuacha pale sakaruni akiwa kalala
chali.Nililitupa uvunguni kwa kitanda na kikajitupa kitandani kifudi
fudi. Muda mfupi usingizi ulinichukua, niliposhtuka ni ndege waliokuwa wakiimba
alifajiri. Niliamka na kufungua mlango waVarandani. Nilipochunguli
niliona bado Getruda alikuwa vile vile alivyodondoka usiku. Nilishindwa
kujua kuwa alikwisha kufa au laa!.Kwa vile nilikuwa mbali kidogo. Sikupenda hata kumsogelea, nilifunga mlango, nikakiendea kitanda kuendelea na usingizi.
Nikiwa
usingizini nilishituliwa na mlio wa simu, nilipoipokea nilisikia sauti
ya mwanaume na sauti hiyo haikuwa ngeni masikioni mwangu.
“ Hallo, vipi Bw. Sweedy?”alisema tu baada ya kusikianimepokea.
“Poa, nani unaongea”Nilimwuliza.
“Mimi Jophu, nauliza jana mkeo amerudi salama?”
Sikujibu kitu zaidi ya kuikata simu.
Baada ya saa moja hasira ilipungua, moyo wa huruma uliniingia, nilitoka na kumfuata Getruda alipo, hali
yake ilizidi kuwa mbaya, damu zilimtoka puani, mapovu mdomoni.
Nilimpigia simu mteja wangu Jangala aje nimpeleke Getruda hospitali,Kama
kawaida Jangala hachelewi alifika na tukampakiza Getruda.
“Vipi?.Mkeo ana matatizo gani?”Jangala aliniuliza wakati akifunga mlango wa nyuma alipo Getruda.
“Anasumbuliwa na shinikizo la damu”
“Oooo! Pole sana Bw, Kachenje”
“Nishapoa”
“Tunampeleka hospitali gani?”
“Naona tumpeleke Hospitali ya rufaa Mount Meru”
“Poa”Alijibu na kuondoa gari kwa kasi,huku likiwa limeacha vumbi zito nyuma.
Nilimfikisha
hospitali ya Mount Meru kwa matibabu. Aliingizwa chumba maalum cha
wagonjwa waliozidiwa ACU na muda mfupi aliwekewa mashine ya kumsaidia
kupumua. Walipomaliza walimtundikia maji ya mwili. Daktari walijitolea
kuokoa maisha ya Getruda kadri walivyoweza. Muda mfupi nikiwa kwenye
benchi, niliona mlango ukifunguliwa, alitoka nesi mmoja mwenye asili ya
kiarabu, kwa haraka nilijikuta moyo ukinipasuka. Nilimfananisha na
Jenifer niliyekutana nae nchini Thailand. Alinifuata pale nilipokuwa,
kitu kilichokuwa tofauti ni kwamba yeye alivaa magwanda meupe, “ Halo,
kaka wewe ndiye muuguzi wa Getruda Kimario?” nilishindwa kumjibu midomo
ilibaki wazi, niliamini kwa hali mbaya ya Getruda nesi aliniletea
taarifa mbaya.
“Kwani kuna nini nesi!…naomba unieleze!”niliongea mwili ukinitoka jasho pamoja na mambo mabaya Getruda aliyo nitendea lakini nilimpenda sana.
“Usiogope kaka. Niambie wewe ni muhusika?” Alisema tena kwa sauti ya chini.Nibaki nimeduwaa kama sekunde kadhaa.
“Ninani
kwako?”Aliuliza tena ,lakini safari hii alionekana kukasirika.
Nilishindwa kumwambi nilibaki machozi ya kinichuruzika, “Hata nikisema
ni mke wangu sijawahi kukutananae kimwili, sasa ni mwambie mimi ninani
wake?.Nikiwa nawaza, nikajikuta naropoka.
“Ni dada yangu” niliongopa
“Ok, pole sana mungu
amemsaidia. Sasa ananafuu”akatulia kidogo na kunitupia tabasamu pana
lililoshiba midomoni mwake.Kisha akasema “Tunategemea kumpa ruhusa
kesho. Mungu akipenda”Nilipandisha pumzi na kuishusha kwa
nguvu”oooophhhh!” nikajifuta jasho.
Kesho yake Getruda aliruhusiwa kurudi nyumbani.
*****************
Tukiwa
sebuleni nilianza kumueleza Getruda. Moyo uliniuma kila nilipo kumbuka
aliyonifanyia “Mke wangu kama ingenipasa kusema, nini kinacho ikera
nafsi yangu ni kuni dhalilisha ndani ya kadamnasi, sio wafanyakazi wangu
wa wageni, wote wanafahamu ulilolifanya, na isitoshe ile ni hotel yangu
unadiriki kufanya mapenzi ukitoa kashfa ili kuinufaisha jamii, kumbuka
aibu si yangu pekee, ni yetu wote.”
Sijui
ni mkate sikio au nimpe kilema kwenye via vya uzazi ni mchome na moto
wa umeme (hita)asiweze kufanya tendo la ndoa maisha?.Ndio itakuwa
fundisho,kiherehere kitamuisha”wakati na waza cha kumfanyia, nilikatishwa na sauti.
“Mume
wangu kumbuka wewe ndio uliyenitafutia mwanaume wa kuniridhisha
kimapenzi, ilinijisikie nina mume, basi kama ni hivyo nami sitaki penzi
la mtu mwingine wa nje. Nataka penzi lako nilikubali kwa kukuheshimu.
Mwanamke kawaida hatafutiwi mume, anatafuta mwenyewe, hisia zote
nilizoweka kama nipo na wewe, iweje useme na kudhalilisha, kama
utashindwa leo kesho nataka talaka yangu,asubuhi na mapema,
umenielewa?”Getrudaalinisemesha kwa ukali.
“Sio
nimekukataza usiwe naye, kinachonikera ni kunidhalilisha na kutoa siri
ya unyumba wetu, sina wivu na mapenzi yako.Ninachotaka unihifadhie siri
moyoni mwako”niliinamisha kichwa chini kama kobe.
“Mume wangu nakutunzia heshima kuliko mtu yeyote duniani, nashangaa!unapo sema nainfaisha jamii.
Kama angekuwa msichana mwingine asinge vumilia hata wiki moja, na
washukuru wazazi kunifundisha uvumilivu ndani ya nyumba”Aliendelea
kuongea,asijue nina mawazo nini moyoni.
Tukiwa
kwenye mazungumzo,nilisikia simu ikiita,nilijipapasa kama ilikuwa simu
yangu.Nilipotizama pembeni nilimuona Getruda akitoa simu yake kwenye
pochi ndogo ya rangi nyeusi iliyojaa nakishi nyingi.
“Hallo,
uko wapi?”Getruda alipokea tu,baada ya kuona jina juu ya kioo cha
simu.Niligutuka nikahisi mtu huyo anamfahamu,ndio maana alimuuliza
aliko.
“Aaaa..nipo Makutano bar hapa napata moja baridi moja moto.Vipi mume bwege yupo?”
“Yupo
anakusalimia”Getruda alisema na kunitupia jicho ,akacheka kidogo na
kuendelea, “Utakuja kutusalimia?”Getruda aliongea akiniongoa wasi wasi.
“Ninani huyo unaongea naye?”Nilijikuta nikisema wakati Getruda anaongea na simu.
“Wivu
umekuzidi mume wangu.Kila kitu unataka kujua hebu chukua basi uongee
naye”Getruda aliibadilikia kwa ghafla,alinyoosha mkono wake
akitakakunikabidhi simu.
“Sihitaji kuongea nae,nimekuuliza kwani vibaya?.Nilifikiri ni mama amekupigia simu”
“Hapana.Nirafiki yangu”Kisha akaendelea kuongea nae.
“Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.Mume wangu anwivu ilembaya”
“Sasa wivu wanini wakati hayawezi?”Sauti nzito upande wa pli ilisikika ikisema.
“Hata mimi nashangaa!”Getruda alidakia na kuangua kicheko kikubwa.
“Mpenzi sikia…..naomba ufike sasa hivi hapa Makutano bar”
“Mama
anaumwa sana!.Ehhe mmempeleka hospitali?”Getruda aliongea maneno hayo
akiwa tayari kesha kata simu.Aliendelea kuongea simu ikiwa imekatika
ilimradi anipumbaze “Ana umwa na nini hasa?” alitulia sekunde mbili hivi
akaendelea, “Ooo! My god .Kuna uwezekana wa kupona?”
alitulia tena sekunde kadhaa hivi, “Sawa.Ninakuja sasa hivi huko”Akajidai kukata simu.
“Vipi mbona jasho linakutoka?.Mama anaumwa na nini?”
Nilimwuliza
sekunde chache alipokata simu. “Mama alidondoka ngazi akiingia
kanisani”Getruda aliongea kiupole kabisa, akionekana kujizuia kulia.
“Kanisani?”
“Ndio.Na hivi sasa yupo amepelekwa hospitali ya Kcmc kwa matibabu” Safari hii alifura na alifanya kulalamika chini chini.
“Ooo! Pole sana mke wangu.Unaonaje nikaoga tukaenda wote?”
“Utanichelewesha sana”
“Basi siogi tena. Ngoja nivae twende,tena nina siku nyingi sijaenda kumsalimu”Niliongea nikiamka kitini, tayari kwa safari.
“Hapana.Nitakuletea taarifa ya hali yake.Nyumba tutamuachia nani?”
“Hilo halina shida.Nisubiri”
“Sitaki
bwana. Wee kila mahali unataka kuongozana na mimi.Nimeshachoka, ngoja
niende kisha kesho nikirudi nitakuja kukuchukua kwani hata kupajua
hupajui.Unapafahamu pale tulipokuwa tukiishi zamani” Nilisimama kama
mlingoti ,nikavuta pumzi na kuzishusha kwa nguvu.Nikatikisa kichwa na
kusema “Sawa.Kama hutaki nikapajua kwenu leo ….hata kesho nitapajua”
Niliona
Getruda akitoa tabasamu kubwa ,hakuishia hapo alinifuata nakunibusu
shavuni “Mwaaaa”Kisha akaokota kipima joto chake,na kutoka kwa haraka
akionekana mwenye wasi wasi mkubwa.Alipofika mlangoni aligeuka na
kunitizama kama akinihurumia vile,sikugundua kitu ,nilibaki
nimeduwaa.Akanipungia mkono na kusema “Bye bye”Nami nikapunga kono langu zito kigoigoi bila tabasamu.
Getruda
alimpigia simu mteja wetu wa kila siku katika usafi,si mwingine bali
Jangala. “HalloJangala tafadhali naomba unichukue hapa nyumbani”alisema
baada ya simu kupokelewa.
“Sawa.Namshusha abiria hapa mjini nakuja”
“Ok”Alijibu na kukata simu.
Kama kawaida yake Jangala huwa hakaidi na hana tamaa.Aliingia na kusimama mbele ya Getruda binti Kimario.
“Shem vipi.Wapi leo pa kula kuku.Si unaelewa wiki end”Jangala alimtania Getruda.
“Ndio.
Wiki end lakini kwangu imenijia vibaya .Nimepata taarifa mama yangu
mgonjwa.Naomba unifikishe karibu na Makutano bar nikampe taarifa
shangazi yangu.Kisha utaendelea na safari yako.Mimi nitakupigia kama
nitakuhitaji tena”Getruda alidanganya.
“Sawa.Riziki ndogo ndogo hizi usininyime shem.Pole sana kwa kuuguliwa na mama yako”
“Nishapoa shem”Alimjibu kiunyonge.Getruda hakuuguliwa wala nini.Alipokuwa akienda ni Makutano bar kukutana na Mzee Jophu Kundy.
Katika mazungumzo yao walijikuta kufika Makutano bar, “Tafadhali nishushe hapa.Kuna uchochoro gari haliwezi kuingia huko.Shilingi ngapi?”
“Elfu nne zinatosha shem”Jangala alisema akimtizama Getruda.
“Punguza shem.Hujui mimi mteja wako?”
“Petroli imepanda bei sana shem. ‘Any way’ nipe tatu unusu”Jangala alisema .
Getruda alimpatia Jangala elfu tatu na mia tano,akashuka garini.
“Usihaike shem.Nitafunga mwenyewe mlango.Mteja kwangu ni
mtukufu”Jangala alisema baada ya kumuona Getruda anataka kufunga mlango.
Getruda alijidai kama anaingia uchochoroni ili Jangala aondoke
zake.Alipogeuka aliona gari la Jangala likiishia bali kabisa.Aligeuka na
kurudim kuelekea kule Makutano bar.
*****************
Ndani
ya makutano bar,alionekana mwanaume wa makamo.Kwa kumtizama ungeweza
kukisia anamiaka hamsini ama hamsini na tano.Kichwa chake kilikuwa na
mvi za kuhesabika.Uso wake ulisha anza kuwa na makunyanzi ya uzee.Alivaa
suti ya kahawia,na viatu vya pembe nne ‘Four angile’.Shingoni alinyonga
tai ya bluu iliyozidi kumfanya maridadi.Mkononi alivaa saa ya seiko 5
ya dhahabu.Meza aliyoketi ilijaa vyakula na vinywaji.
Mara
kwa mara aliinua mkono wake wa kushoto akitizama muda,alipomaliza
aligugubia glasi ya bia mdomoni na kuirudishia glasimezani.Pia muda wa
kuiacha pombe ishuke vema tumboni alitupa macho yake lako la kuingilia
wateja.Safari hii ilikuwa mara ya kumi kutizama lango hilo,alipohamisha
macho aliyapeleka kwenye glasi ya kinywaji,akaona kama bia ilishaisha
glasini,alikamata chupa ya bia na kumimina kiasi kwenye glasi ya
bia.Hakuchelea aligugubia kama mikupuo miwili bila kuishusha
mezani,alipomaliza akacheua kama mara tatu hivi,alihisi kilevi kikipanda
vema ndani ya ubongo.Akajikuta akicheka mwenyewe
“Mimi ndiye.Mwingine hakuna”Alisema nakutizama simu yake.Aliiokota nakujaribu kupiga,simu aliyopiga iliita bila kupokelewa.
“Shiit.Kwanini hapokei?”alipayuka kwa ghadhabu.
Hakuchoka akapiga mara ya pli,iliita tena,akasikia ikipokelewa “Hallo Prety girl.Uko wapi mbona hupokei simu yangu?”
“Nakaribia jengo la Makutano hapa”
“Sawa.
Nakusubiri kwa hamu wa moyo”Walikata simu.Mzee Jophu akawa habandui
macho lango la kuingilia,alitaka kumwona Getruda akiingia kwa
madaha.Ghafla aliona mlimbwende akiingia kwa mapana na kumfanya kila
aliyeko mle ndani kumtupia jicho.Getruda hakuwa mzuri sana wa
sura,lakini umbo lake na makalio ndio kichochezi kwa wanaume rijali.Kila
alipovuta hatua ,makalio yake yalitikisika mithili ya mawimbi
baharini.Nafiki jambo hilo ndilo lililomfanya Mzee Jophu ammezee mate
mke wangu.Si kwamba na msifia kwa vile ni mke wangu,hapana.Njoo kwangu
Arusha ushuhudie, ukweli wangu.Lakini kwa sasa ni mzee sana.
“Kaaaa,
kakaka!”alionekana kijana mmja aliyeko nyuma ya mzee Jophu
akihamaki,mfdomo ukiwa wazi kwa mshangao na mkono ukiwa umeshika mdomo wa chini,Jicho likiwa limemtoka kama ndulele iliyoiva.
“Mkindu wavona ilo ibora ledha aho”Kijana huyu alimwambia mwenzake kwa kilugha.
Akimaanisha “Mkindu umeona lisichana hilo linalo kuja hapo?”
“Nikirumo ilo!”Mkindu alijibu.
“Hilo ni balaa!” Wakacheka.
Mzee Jophu alimsindikiza Getruda kwa macho ya matamanio hadi alipomkaribia kabisa.
“Vipi.Mbona umechelewa ?”
“Mume bwege alikuwa akinichelewesha”Getruda aliongea akivuta kiti kilicho wazi.
“Achana nae.Ukisha mkabidhi fisi bucha unamatarajio gani?”
“Kuokota mifupa”Getruda alidakia.
“Hakuna kinachobaki.Fisi gani anakuachia mfupa!”Wakacheka na kupigana mabusu.Kisha akagonga meza.
“Muhudumuuu”aliita.
“Nakuja”sauti ilisikika kwa mbali kidogo.
“Kuja
haraka.Watu wanapesa zao hazina pakwenda”Alisema akijiamini
kabisa.Getruda alimtizama akagundua mzee Jophu alishaanza kulewa.
“Mpati wa moyo wangu kinywaji chochote anachotaka upesi”Muhudumu akaitikia sawa.
“Dada nikupatie kinywaji gani?”
“Henken ya kopo.Usisahau mrija tafadhali”
“Ya baridi au moto?”
“Aaaa! Vuguvugu.Nitapata?”
“Usihofu,utapata”Muhudumu aliondoka.
“Mpenzi
nimekuita nina jambo muhimu la kukueleza,hivyo basi naomba
uwemsikivu”Alitulia kidogo na kuokota glasi ya bia,hakuchelewa alimimina
bia yote na kurudisha glasi tupu.Akacheua mara mbili nakuendelea
“Kwanza kabla ya yote. Napenda unihakikishie kwamba unanipenda”
“Nakupenda sana mpenzi inamaana hujagundua bado?”
“Ninyi wanawake mnabadilika sana.Lazima kila tunapokutana tuulizane jambo hili”
“Si
wote bwana.Unajua ninyi wanaume mkionyeshewa kama mnapendwa sana vichwa
huvimba na kujiona mna matilaba ya kufanya lolote juu ya mwanamke”
“Ni
baadhi ,si mimi Jophu”Akasema na kusogeza kiti jirani na Getruda.Kabla
hajaendelea tayari vinywaji vililetwa,Henken ya Getruda na safari ya
Mzee Jophu.
“Karibuni”Muhudumu alisema.
“Ahsante”Getruda akajibu.
“Wee binti mwite mchoma nyama tafadhali”Hakukawia kufika mchoma nyama. “Kata nyama ya kidari,ile laini…umeelewa?”
“Ndio,bosi”
“Haya futikaa”Alisema kiulevi ulevi.Akamgeukia Getruda, “Wife,sasa tuendelee na mazungumzo yetu”
“Kama umenidhihirishia unanipenda utakuwa upande wangu kwa lolote lile,si ndivyo”
“Ndivyo”
“Nikisema kitu kwa manufaa yetu lazima tusaidiane,sivyo?”
“Ndivyo”alijibu
kiupole hakujua ni jambo gani anataka kuelezwa wakati huo.Kwa sasa Mzee
Jophu akapunguza sauti akamweleza Getruda kwa sauti ya chini
kabisa.Nafikiri alihofu watu kung’amua maneno yake.
“Getruda naomba iwe siri kubwa sana.Nataka tumuondoe Sweedy Duniani”Getruda alishituka sana kama aliyeamshwa usingizini. “Heee!”
“Usishituke
laazizi wangu.Nimeamua hivyo kwa manufaa yetu pia.Kila siku kujiiba
iiba ,tutajiiba mpaka lini?.Heri afe tupate uhuru….”
“Haiwezekani Jophu.Unajua dhambi ya kuua lakini?”Getruda aliuliza.
“Acha ujinga, nani kakuambia kuna dhambi.Nani aliyeenda akarudi akasema kuna adhabu kali?.Niambie”
“Kwenye maandiko takatifu,maneno hayo yapo.”Getruda alijibu akimtizama Jophu.
“Kumbe nimaandiko yaliyotungwa kama hadithi tu.Nitajie nani alikufa akafufuka na kutuonyeshea adhabu alizopata ahera?”
“Bwana acha mizengwe yako.Uhusiano wetu hauwezi kuzuilika kwa sababu ya Sweedy”
“Nitakupa
chochote lakini tumuue Sweedy.Uko tayari?”Getruda alikaa kimya,safari
hii alishindwa kijibu. “Nijibu basi?”Mzee Jophu alimhimiza.
“Nikujibu nini?”
“Kwani
hujui.Sina jibu lolote.”Akamtizama Mzee Jophu ,na kuvutakumbukumbu ya
siku ya kwanza tulipokuwa kanisani,alikumbuka maneno mengi ya
mchungaji.Akanikumbuka nilipompiga busu la kwanza nikiwa namvisha pete
ya ndoa.Pia akakumbuka maneno ya mama yake akimweleza juu ya unyumba
wetu.Machozi yakamtiririka mashavuni bila kujijua.Akapandisha mkono wa
kuume ulioshika leso na kujifuta. Mzee Jophu alinyoosha mkono na
kumpatia funguo Getruda.
“Kuanzia dakika hii.Land cruiser iliyoko nje ni mali yako.”Getruda alishangaa hakuamini kile alichokuwa akikiona wakati huo.
“Mpenzi ni kweli ama ni mipombe inakusumbua akili?”
“Sijalewa
wa moyo.Ninachohitaji sasa hivi, ni kutoa uhai wa huyu hanithi”Akatulia
kama nukta tano hivi ,kisha akasema,“Sawa sawa?”
“Sawa”Getruda
alijibu mapigo ya moyo yakimwenda mbio.Alifikiri na kuona kwanza
alishachoka kukodi teksi kila siku.Naye alitaka kutembelea gari la
kifahari.Alitamani akawatambishie mabinti wenziye aliosoma nao pale Mkuu
Rombo.Watajuaje kwamba naye nitajiri pasipo kutembea na gari la
kifahari?.Aliamini mtu akiwa na pesa huheshimika kuliko hata kitu
chochote duniani.Akajikuta moyo ukipamba na furaha kali, “Acha afe bwana
kwani nini bwana. Mtu kama furushi la nguo, heri afe , wangapi wameuawa
na kuwaacha wake zao na mapesa kibao.Mungu nisamehe”aliwaza akilini.
Waliendelea kunywa na kula nyama choma pale.Getruda alimaliza bia
yake na kuongezwa zingine mbili,tayari ubongo ukafa ganzi.Alianza
kuongea sana,tena bila kujali kwamba alisikiwa na watu. “Mpenzi wangu
nasema hivi…nitamuua kwa mikono yangu mwenyewe.Haina haja ya kuishi
wakati hana sifa ya kumfanya hai. Eti mume, mume gani bwege kilasiku
hapandi kitandani mpaka nishikwe na usingizi ndio nae apande!!!!”
“Hatakama ingelikuwa mimi.Ningetumia akili hiyo hiyo.Unafikiri ni kazi ndogo hiyo…fedheha bwana!”
Mzee
Jophu na Getruda alikunjwa na kuondoka zao.Walielekea nyumba moja ya
wageni ambako waliingiza gari la Gertuda na kujipumzisha.
**************
Katika maisha yangu nina kijitabia fulani cha kutotoka siku za mwisho wa wiki,isipokuwa jioni
tena nikiwa na mke wangu ,Getruda. Huwa natoka katika matembezi mafupi
na kurudi nyumbani.Juma pili hii ilikuwa ngumu kwangu.Kwanza mke wangu
hakuwepo,usishangae nikimuita mke wangu japo sikufanikiwa kufanya tendo
la ndoa.Ni mke wangu kwa sababu nimefunga ndoa kanisani.
Mawazo
bado yalinizonga sana akilini,niliwaza safari ya ghafla ya mke
wangu.Nilitamani sana nijue maendeleo ya wazazi wake huko mkuu
Rombo.Kingine ni tatizo linaloniletea utata ndani ya ndoa yangu.Nilizidi
kuwaza ,kwanini ugonjwa huo uwe kwangu tu.Kwanini usiwe kwa
fulani?.Nilitamani kunywa bia lakini lakini nikaona si kutatua tatizo
zaidi ya kuliongeza.
Nikiwa
kwenye dimbi la mawazo,nilisikia simu ikiita,nilishituka sana.Kwa
haraka nikaiendea simu ambayo niliiacha Varandani juu ya meza.Nilifikiri
mambo mengi ,nikahisi aliyepiga simu alikuwa mke wangu akinipa habari
za mama yake,nilitegemea kupata habari mbaya kutokana na maneno
aliyoniacha nayo Getruda jana alipokurupuka akionekana wazi kuchanganywa
na hali ya mama yake.Nilipofika nikaiokota simu upesi na kuipokea ,
“Hallo mume wangu.Umzima ?”
“Ndio.Vipi kuhusu hali ya mama.Anaendeleaje?”Nilimwuliza.
“Kidogo amepata ahueni.Kuna uvimbe gotini unamsumbua”
“Utakuja lini?”
“Aaa kesho jioni.Namsaidia kumuuguza hospitalini”
“Sawa.Nimebaki mwenyewe kama mkiwa”
“Usijali mpenzi.Upo nyumbani, na hutoki leo?”
“Ndio,nipo sitoki bila wewe.Kwanza najisikia vibaya kabisa sijui ni kwanini mpenzi”
“Pole sana mume wangu,bye”
Getruda akakata simu.
*********************
Kulikuwa na kundi la patao watu watano,aliyekuwa
msemaji mkuu akiwa mzee Jophu.Pembeni aliketi Getruda na kushoto kwake
mwanaume mmoja mwanye umbo kubwa,unaweza ukamfananisha na mcheza
mweleka.Mikono yake minene iliyojaa na kujengeka misuli.Kushoto kwa
mwanaume yule alikuwepo kijana mwingine,mrefu mwembamba lakini anasura
ya kukatili.Ukimuona lazima ungemtambua kama ni muuaji.Huyu aliweka
bastola kibindoni,bastola aina ya Revolver.Aliyebaki alionekana mdogo
sana,ukitadhimini umri wake ni miaka kumi na tano,alionekana alikulia
mitaani.Huyu ni kibaka mzoefu ,achilia mbali bangi ,sigara na dawa za
kulevya, kuvuta petroli na gundi ya viatu kwake si tatizo.Mtoto huyu
walimtumia sana katika matukio ya ujambazi na upelelezi wa wapi kuna
pesa ,wapi tukaibe leo.
Walicheka
muda mfupi tu baada ya Getruda kukata simu, “Anasemaje huyo maiti”Mzee
Jophu aliuliza akiwa anamtizama Getruda kwa udadisi.
“Anasema leo yupo nyumbani hatoki,ni jambo ambalo liko wazi bila mimi habandui mguu wake.Hivyo kazi yake imeisha”
“Patamu
sana hapo.Naomba vijana wangu waingie kazini.Kama nilivyo waelekeza na
mfanye kwa tahadhari sana msije kubainika kama ninyi ndio
mlioua.Mmenisikia?”
“Mzee usitufundishe hii ndio kazi yetu kama kazi nyingine.Tumeua sana na tutaendelea kuua.Pesa ya
kazi mbele”Alisema jambazi mmoja nene lenye kifua kama
pipa,lilitambulika kwa jina moja tu ‘Man Kaugo’Man Kaugo ana kasumba
moja hataki kufundisha kazi ya uuaji,nasema anaielewa vema na ujuzi huo kwake ume komaa.
“Naona mchukue lita arobaini za petroli.Mzungushie nyumba yake yote na muitie kiberiti”
“Eeee!kuna vitu vyangu vya muhimu.Kwanini msimuue bilakuchoma nyumba”
“Vitu vyako nitakulipa.Tatizo ni nini?”
“Nyumba yamgu.Nilitaka mumuue nibaki na nyumba”
“Nyumba nitakununulia njiro”
“Haya, usinidanganye mpenzi”
“Sikudanganyi.Mimi na wewe kwani wa tani?”
“Hapana”
“Sasa kumbe…” akatulia kidogo kisha akasema, “Nafikiri tumemaliza makomando wangu”
“Pesa zetu bado.”
“Kiasi gani ?”
“Milioni tatu kwa kichwa kimoja”
“Ok,subirini kidogo nakuja.”
Mzee
jophu alitia gari moto na kuondoka zake.alielekea benki ambako
alichukua milioni tano na kuzihifadhi.Hakuchelewa alirudi. “Kamata
milioni tatu hizi.Naomba mharakishe tafadhali”
“Sawa mzee.Utasikia mwenyewe mambo yakijibu”Wale vijana waliondoka zao.
Nilisikia
kama watu wakiongea nje ya jengo langu,kila nilipojaribu kutega sikio
kwa makini,nilishindwa kun’gamua mazungumzo yao.Nilitunguza redio kabisa
,japo nilikuwa macho lakini nilihisi bado kiko usingizini,watu hao
walinikaribia dirishani ,kwambali nikasikia mmoja wapo akisema “Hili
ndilo dirisha lake”
Mwingine
akasema “Basi hapa tumwage petroli nyingi iliafe haraka”kilikuwa
kitendo cha haraka nilisikia petroli ikimwagwa dirishani,nilikurupuka na
kushituka ,nilipofungua macho kumbe nilikuwa nikiota njozi mabaya
kabisa.Kukurupuka kwangu hata mke wangu Suzan ambaye tulibahatika kupata
mtoto wa kiume aitwaye Samji ,alinisikia nikipiga kelele, “Nakufaaaaa”
“Nini
mume wangu?”Suzan, mke wangu aliniuliza akiwa na masalio ya
usingizi.Nilihisi mapigo ya moyo yakinienda mbio utadhani nilikimbia umbali mrefu bila kupumzika.
“Baba samji,ni nini mbona umepiga kelele kiasi hicho?”
“Ndoa yangu inanitesa”Niliropoka nikipikicha macho, sikuamini yale niliyoyaona nikiwa usingizini.
“Ndoa yako inakutesa kivipi?”
“Nafikiri nilikuwa nikiota ndoto ya mateso kabisa”
“Ndoto?.Nilikusikia
hata wakati mwingine ukilia ukiwa usingizini.Nilikutingisha lakini huku
shituika, ulikuwa ukisema Getruda Getruda .Getruda ninani?”Nilitulia
kidogo nikajaribu kumkumbuka, “Getruda ni huyo mwanamke niliyemuoa,
akawa ananitesa”
“Usinidanganye mume wangu.Madhambi unayofanya na mahawara wako ,ndio unayaota usiku?”
“Basi
nisamehe mke wangu,ni ndoto tu.Sina mtu nimpendaye zaidi yako.Sijui
njozi ya ajabu namna hii imetokea wapi.Yote niliyoota hakuna hata kimoja
kilichowahi kunitokea”
Ilikuwa usiku ,majira ya saa kumi na moja.Suzan, mke wangu alinisamehe na tukaanza kusali.
MWISHO