Jamaa mmoja kijasho kikimtoka na panga kali mkononi akaingia msikitini, akaanza
kuwauliza, "hapa nani muislam?" wote wakawa kimya, akauliza tena, jamani hapa
nani muislamu? " watu wakaendelea kuuchuna, akamchukua mmoja wao aliyekuwa
amekaa mlangoni akatoka nae nje, kufika nje akamwambia, samahani mkuu
wangu kwa kukusumbua, naomba unichinjie mbuzi wangu, jamaa akakubali
akamchinja yule mbuzi, kisha akamwambia mie kuchuna siwezi (alikua mzee kidogo) labda urudi tena
msikitini, Jamaa akaingia tena msikitini huku panga likiwa limejaa damu , Akaenda kuwauliza tena" jamani
nani muislam hapa? " wakamuonyeshea kwa Imamu, Imamu akaanza kujitetea," Aah
jamani yaani mie kuswalisha leo tuu ndo nimeshakuwa muislamu!!!?"
HAHAHA!!!