JOHNNY alikuwa analala darasani wakati mwalimu anafundisha!
MWALIMU: We John kwanini unalala wakati mi nafundisha?
JOHNNY: Unajua mwalimu sauti yako nzuri ndio maana nikalala!
MWALIMU: Sasa mbona wenzako hawajalala?
JOHNNY: Kwa sababu wao hawakusikilizi!!
MWALIMU: Haya nitajie mifano ya wanyama kumi wa pori...
JOHNNY: Aaaah! uliza swali lingine bhana hilo siwezi kujibu ni rahisi mno!
MWALIMU: Jibu kwanza hilo kama ni rahisi!
JOHNNY: Simba saba na Chui watatu...!!!