Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini
unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.
Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una
furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .
Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile
utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri
Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu
wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.
Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo
cha maisha yako, atakulinda daima.
Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya
shinikizo fulani (pesa au mali)
Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini
nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine,hafichi hisia zake mbele za
watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.
Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na
atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.
Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba
katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .
Atakuwa tayari kuvumilia,hatak uwa mwepesi wa hasira
wala kutumia lugha chafu na ubabe.
♥♥♥♥♥