Headlines News :

Sunday, March 2, 2014

KITUKO : HOUSE BOY

 


Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.

Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.

Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.

Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss:Bakariiii!
Bakari:Naam boss!
Boss:nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss:Bakariiiii !
Bakari:naam boss!
Boss:nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.

Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari:boss huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno mengine husikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.

Bakari:Boss!
Boss: naam Bakari!
Bakari:Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss kimyaaaa!

Bakari:Bosss!
Boss: ndio Bakari!
Bakari:Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss kimyaaaaaaa!
Bakari:Boss!

Boss: naam Bakari!
Bakari:Nani aliyempachika mimba house girl?
Boss kimyaaaa!

Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!!
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger