Headlines News :

Friday, July 10, 2015

TAIFA STARS YAZIDI KUSHUKA VIWANGO VYA FIFA

info-560x270

Tumeshuhudia timu ya Taifa Stars ikiwa na matokeo mabovu mfululizo ikiwemo kushindwa kufuzu michuano  ya  CHAN 2016 na kutolewa na Uganda kwa jumla ya mabao 4-1 katika mechi za kufuzu.
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeporomoka katika viwango vya FIFA kwa nafasi 12 hadi nafasi ya 139… Taifa Stars imepata matokeo mabovu mfululizo  katika mashindano ya COSAFA ambayo ilishiriki kama nchi mgeni mwalikwa, ilifungwa mechi zote tatu za kundi B,mechi ya kwanza kufuzu AFCON 2016 ilifungwa 3-0 Misri.
Kufuatia matokeo hayo shirikisho la soka Tanzania TFF liliamua kumfukuza kazi kocha Mholanzi Mart Nooij na nafasi yake kupewa kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye amepewa miezi mitatu ya majaribio.
KOCHA-TAIFASTARS1
Kocha aliyetimuliwa baada ya Stars kuwa na Matokeo mabaya, Mart Nooij
Mkwasa ameanza vizuri kibarua chake hicho baada ya kupata sare 1-1 ugenini dhidi ya Uganda, katika orodha iliyotolewa jana makao makuu ya FIFA mjini Zurich Uswis  inaonyesha baadhi ya nchi wanachama wa CECAFA pia kuporomoka Uganda imeshuka kwa nafasi mbili hadi 73, Rwanda imeporomoka kwa nafasi 16 hadi nafasi ya 78, Sudan imeporomoka kwa nafasi 18 hadi nafasi ya 90.
MKWASA
Kocha aliyekabidhiwa kuifundisha Stars Charles Boniface Mkwasa pamoja na msaidizi wake Hemed Moroco
Story nimekusogezea toka >>>BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger