Headlines News :

Monday, July 13, 2015

SABABU ZA RIBERY NA TEVEZ KUTOFANYA UPASUAJI KUONDOA MAKOVU YAO…FAHAMU KWA NINI WAMEAMUA KUYAACHA

frankriberyscarsKwa kiasi fulani, makovu ni moja ya vitu ambavyo huwafanya watu wakumbuke matukio yaliyopelekea hali hiyo kuwatokea, ni vigumu sana kusahau tukio ama hali iliyokusababishia athari mwilini endapo una kovu katika moja ya sehemu za mwili wako. 
Unapozungumzia wanasoka waliowahi kupatwa na masaibu makubwa katika maisha yao, kiasi cha kusababisha kuacha makovu kwenye miili yao, basi huwezi kuacha kuwazungumzia wanandinga Frank Ribery pamoja na Carlos Tevez.
Frank Ribery ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anakipiga katika klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.
frankriberysoccerRibery ni moja ya wachezaji wanaosifika kwa ubora wake uwanjani kutokana kasi, nguvu, mbinu na uwezo mkubwa wa kupiga pasi pindi awapo uwanjani. Hata hivyo makovu mawili makubwa aliyonayo usoni ndio yanamtofautisha na wachezaji wengine wa kiwango cha aina yake (World class players).
Katika mahojiano yake kadhaa ambayo amewahi kufanya na vyombo vya habari, Ribery ametanabaisha kuwa makovu yake yametokana na ajali ya gari aliyoipta pindi alipokuwa na umri wa miaka miwili.
Ribery anasema, “Tatizo ni kwamba nilikuwa nimekaa siti ya nyuma na wakati ajali ile ilipokuwa inatokea, nilirushwa mpaka upande wa mbele wa gari.” Alipata jeraha kubwa kiasi ya kwamba, mamia ya nyuzi yalitumika kushona jeraha lake ili angalau aweze kurudi katika hali yake ya awali. 
Lakini swali ni kwamba kwa nini mpaka sasa ameendelea kubaki na makovu makubwa wakati, kulingana na utajiri alionao ana uwezo wa kufanya upasuaji ili kuondoa makovu hayo?
Wakati alipowahi kuhojiwa na gazeti la La Gazzetta dello Sport la nchini Italia, Ribery alisema, “Najivunia makovu yangu, yamenipa nguvu na muonekano mpya…Lazima uwe timamu kiakili ili uweze kuvumilia utani kutoka kwa watoto na kejeli za watu wazima”.
 Ribery alihitimisha mahojiano yake kwa kuongeza, “unionavyo hapa, hii ndio sura yangu halisi, tena ambayo watu wanaitambua. Ninaufurahia sana uso wangu. Kwa nini nisiufurahie?”
Carlos Tevez pia ni moja ya wachezaji wa kiwango cha juu kabisa katika ulimwengu wa soka ambaye anajulikana uwanjani kutokana na matumizi yake ya nguvu na uwezo mkubwa wa kufunga pindi awapo uwanjani.
carlostevezscarsHata hivyo kama ilivyo kwa Ribery, Tevez pia ana kovu kubwa ambalo lipo maeneo ya shavu lake la kulia, ambalo alilipata akiwa na takribani miezi kumi tu tangu atoke tumboni mwa mama yake. Kwa upande wake, Carlos Tevez katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya, amelielezea tukio lililopelekea kupata kovu hilo kwa kusema, “Mama yangu akiwa anapata kinywaji na mwenzie (shangazi yangu) huku wakiwa wameniacha nimekaa peke yangu.
Bila ya kujua nilitambaa mpaka kwenye birika ambalo lilikuwa na maji ya moto na ndipo yaliponimwagikia na kuniunguza.”
Hata hivyo alipoulizwa kwa nini mpaka sasa hajaliondoa kovu hilo ambalo lilimpelekea kulazwa hospitali kwa miezi miwili, alijibu kuwa ni sehemu ya maisha yake namna alivyo pindi alipokuwa mtoto mpaka sasa ukubwani.
carlostevez 
Tevez alisema, “ni kumbukumbu kubwa sana kwangu. Kamwe siwezi kufanya upasuaji. Ukinichukulia kama nilivyo au vinginevyo, sawa tu. Vivyo hivyo kwa upande wa meno yangu. Siwezi kujibadilisha namna nilivyo sasa”
Makovu ya Carlos Tevez yanabaki kuwa kumbukumbu yake ya mafanikio kwa mji wa Fuerte Apache huko Buenos Aires ambao uligubikwa na uhalifu wa hali ya juu na ambapo ndipo alipozaliwa. 
Aliongeza, “Pengine ningeweza kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na kuishia kusikojulikana lakini kwa bahati nzuri, nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu na kufikia hapa nilipo. 
Kiukweli maisha yangu ya utotoni niliyafurahia sana. Nilijifunza mengi ambayo yamepelekea leo hii mimi kuwa hapa nilipo: heshima, unyenyekevu na kutoa sadaka”.
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger