Headlines News :

Thursday, July 16, 2015

CHELSEA NEW KIT SEASON 2015/16 :

Tukiwa tunasubiri kuanza kwa Ligi Kuu Uingereza msimu ujao vilabu kadhaa vimekuwa vikitangaza jezi za mechi za nyumbani na ugenini… Mara nyingi jezi zao huwa hazibadiliki rangi kinachobadilika ni muundo tu wa jezi na wakati mwingine nembo ya mdhamini kutegemeana na Mkataba ambao Klabu wanao.

Sababu mojwapo inayofanya vilabu vingi vikubwa duniani kubadili muundo wa jezi kila msimu, ni kusaidia klabu iweze kufanya biashara ya mauzo ya jezi kwani mashabiki wengi wa soka barani Ulaya huwa wanajivunia kuvaa na kumiliki jezi orijino ya klabu anayoipenda.

Shabiki wa klabu husika anaona fahari kuvaa jezi orijino na anajivunia pia, kuna vilabu ambavyo vimeshatangaza aina ya jezi watakazotumia msimu ujao ikiwemo Arsenal na sasa ni zamu ya Chelsea mtu wangu, nimekuwekea video ya jezi za Chelsea watakazotumia msimu ujao kwa mechi za nyumbani.

  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger