Headlines News :

Saturday, June 20, 2015

LIONEL MESSI ATIMIZA MECHI 100 BILA TAJI LOLOTE


Jumamosi huko Nchini Chile, Supastaa Lionel Mechi ataichezea Nchi yake Argentina Mechi yake ya 100 dhidi ya Jamaica lakini Karne hiyo ya Mechi itafikiwa bila ya yeye kutwaa Taji lolote akiwa na Nchi yake.
Mechi hii na Jamaica ni Mechi yao ya mwisho ya Kundi B la Copa America ambalo kwa Argentina ndio lilikuwa Kombe lao la mwisho kulitwaa Mwaka 1993 na imepita Miaka 22 bila Nchi hiyo kutwaa Taji jingine lolote.
Messi amepata mafanikio makubwa na Klabu yake Barcelona ya Spain  kwa kuweza kuzoa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani mara 4, kutwaa Klabu Bingwa Ulaya mara 4, Ubingwa wa Spain mara 7 na Copa del Rey mara 3.
Lakini kwenye Timu ya Taifa ya Argentina hali ni tofauti na tena alianza kuichezea vibaya kwani katika Mechi ya kwanza tu, hapo 17 Agosti 2005 akiwa na Miaka 18, aliingizwa KIpindi cha Pili na kudumu Dakika 1 tu na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada kumpiga kipepsi Mchezaji wa Hungary Vilmos Vanczak.
Mechi hiyo ilipokwisha Wachezaji wenzake wa Argentina walimkuta Messi yuko ndani ya Chumba cha Kubadili Jezi akilia.
Katika Mechi zake 99 hadi sasa, Messi ameshafunga Bao 46 na kucheza Fainali za Kombe la Dunia mara 3, 2006, 2010 na 2014, na kuishia kwa machozi tu.
Messi, atakaetimiza Miaka 28 Juni 24, anatarajiwa kuvunja Rekodi za Argentina za Javier Zanetti za kucheza Mechi 145 na ile ya Gabriel Batistuta ya kufunga Bao 56.
 
Pia hii, huko Chile, Kepteni Lionel Messi ana nafasi poa kuiongoza Argentina kutwaa Taji lake la kwanza kwa kulibeba Copa America.
 
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger