Headlines News :

Friday, July 25, 2014

TETESI ZA SOKA ULAYA

Kiungo wa Juventus Arturo Vidal ameipa pigo
Manchester United kwa kudai hatokwenda Old
Trafford (Daily Mail), Liverpool watatumia madai
hayo kumfuatilia kwa makini Vidal kwa kutoa
pauni milioni 42.5 (Metro), Atlètico Madrid
wameanza kumfuatilia mshambuliaji wa
Manchester United Javier Hernandez, 26 (Times),
kiungo wa Chelsea Marko Marin, 25,
anazungumza na Besitkas kwenda kwa mkopo
(Sun), meneja wa Aston Villa,, Paul Lambert
amesema nahodha wake Ron Vlaar, 29,
anayefuatiliwa na Tottenham, hauzwi (Sun), beki
wa Spurs Vlad Chiriches huenda akaenda Roma
(Sun), Jose Mourinho anakaribia kukamilisha
uhamisho wa Didier Drogba, 36, huku kipa Petr
Cech, 32, akimuonya Mourinho kutomkalisha
bench msimu ujao (Sun), Arsenal wanamfuatilia
kipa wa Real Madrid Iker Casillas, 33, na
wamempa mkataba wa miaka mitano kwa
mshahara wa pauni milioni 1.4 kwa mwaka (Daily
Express), Manchester United wanapanga
kumfuatilia Memphis Depay, 20 wa Uholanzi
(Sun), Per Mertesacker, 29, Mesut Ozil, 25 na
Lukas Podolski, 29, watakosa mwanzo wa msimu
baada ya kuongezewa likizo kufuatia kushinda
Kombe la Dunia (Daily Mirror), Ryan Giggs
amemuelezea meneja mpya wa Manchester
United Louis van Gaal, kama "Alex Ferguson
Mpya" (Telegraph), nahodha wa Liverpool Steven
Gerrard, 34, anajiandaa kusaini mkataba wa
mwaka moja zaidi (Liverpool Echo), Inter Milan
imedai inakaribia kumsajili beki Gary Medel wa
Cardiff City (Wales Online), Sunderland wana
matumaini ya kumsajili beki wa Chelsea Patrick
van Aanhold (Metro), Arsenal wanamtazama kwa
karibu Douglas Costa ambaye amekataa kurudi
Shakhtar Donetsk kutokana na matatizo ya
kisiasa. Mchezaji huyo anafuatiliwa pia na AC
Milan na Spurs (Sky Sport Italia), Arsenal
wanajiandaa kuwasilisha maombi yao kwa
Hoffenheim kumsajili Roberto Firmino.
Mshambuliaji huyo kutoka Brazil anatakiwa pia
na Inter Milan (Tuttomercatoweb.com) matumaini
ya Manchester United kumsajili Juan Cuadrado
yameongezeka baada ya Bayern Munich kuacha
kumfuatilia mchezaji huyo wa Fiorentina
(talkSPORT).

NA. KIKEKE SALIM

  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger