TETESI ZA SOKA ULAYA
Boss wa Manchester City Manuel Pellegrini
anapanga kumchukua Didier Drogba, 36, ambaye
pia anasakwa na klabu yake ya zamani Chelsea
(Daily Star), meneja wa Manchester United Louis
van Gaal anataka kutoa pauni milioni 17
kumchukua beki mkabaji wa Ajax Daley Blind, 24
(Daily Express), United pia wameripotiwa kuwa
karibu kumsajili beki wa kati wa Borussia
Dortmund Mats Hummels, 25, kwa pauni milioni
16 (Daily Mail), Tottenham wameambiwa watoe
pauni milioni 25 kama wanamtaka kiungo wa
Real Sociedad Antoine Griezmann, 23, ambaye
pia anafuatiliwa na Chelsea na Monaco (Daily
Telegraph), boss wa Arsenal, Arsene Wenger
amesema hatosajili mshambuliaji msimu huu na
hivyo kufuta tetesi zinazomhusisha na Mario
Balotelli wa AC Milan (Daily Mirror), kiungo wa
Ureno Thiago Mendes, 23, ametupilia mbali
uwezekano wa kurejea Chelsea na angependa
kusalia Atletico Madrid miaka miaka mingine
miwili (Daily Express), PSG watakwepa sheria za
Fifa za fedha kwa kumchukua Angel Di Maria,
kwa mkopo kwa mwaka mmoja kutoka Real
Madrid. Di Maria anasakwa pia na Man United
(Daily Express), Arsenal, Chelsea na Man United
wanamtaka beki Reece Oxford, 15, baada ya
kinda huyo kuonesha kipaji msimu uliopita akiwa
na West Ham ya vijana (Daily Star), Arsene
Wenger atamruhusu Thomas Vermaelen kwenda
Manchester United, ikiwa tu atarhusiwa
kumchukua Phil Jones au Chris Smalling (Daily
Mirror), Chelsea watampa Didier Drogba mkataba
wa miezi 12 wa kucheza ambao hautakuwa na
kipengele cha kuwa kocha, ingawa Chelsea wapo
tayari kuzungumzia hilo (Daily Telegraph),
mshambuliaji wa Lille Divock Origi anakwenda
Boston Marekani kuungana na Liverpool ambao
wapo katika ziara ya mechi za kabla ya msimu.
Atafanyika vipimo kabla ya kukamilisha uhamisho
wake wa pauni milioni 10. Huenda pia
akarejeshwa Lille kwa mkopo (Daily Star).
NA. KIKEKE SALIM