Headlines News :

Wednesday, July 23, 2014

KAPTEN DUNGA AWA KOCHA MPYA BRAZIL

Brazil imemtangaza mchezaji wa zamani Dunga
kuwa kocha wa timu ya taifa, kwa mara ya pili.
Dunga alikuwa nahodha wa Brazil mwaka 1994
waliposhinda Kombe la Dunia, na alikuwa kocha
kuanzia mwaka 2006 hadi 2011.
"Nimefurahi sana kurudi," amesema Dunga, 50,
ambaye alikuwa akitajwa sana kuchukua nafasi hiyo.
Dunga anachukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari,
aliyejiuzulu baada ya Brazil kufika nusu fainali ya
Kombe la Dunia 2014, lakini alipata kipigo kizito
katika historia ya taifa hilo kwa kufungwa 7-1 na
Ujerumani. Dunga aliifikisha Brazil katika robo fainali
Afrika Kusini mwaka 2010.

  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger