Headlines News :

Saturday, July 26, 2014

JINI NAMIZI ( JINAMIZI )

Kukabwa na Jinamizi katika ndoto kama
tunavyoita ni kitendo ambacho kinawatokea watu
wengi sana.
Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni Jini
lakini Tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama
“Mwili kupooza katika usingizi” (Sleeping
Paralysis)
Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa
sekunde 20 lakini wewe unayehusika
utahisi kama dakika 5 au dakika 10.
Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na
yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na
nusu macho.
Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila
yanakupa khofu kwa muda fulani.
Unapokabwa unakuwa na fahamu nusu. Unaweza
kufungua macho, na utahisi kupiga kelele lakini
watu hawakusikii, Mwili wako unakuwa hauwezi
kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa
havifanyi kazi,
Inapokutokea unakuwa huwezi kunyanyua mguu
wala mkono wala kichwa. Kwa ujumla unakuwa
kama uliyepata
“ugonjwa wa Kupooza”.
Hali hii ya kukabwa inapotokea unaweza
ukamuona mtu anayetisha akiingia ndani
chumbani kwako, wengine wanaona kama
wanatekwa nyara au kuchukuliwa, wengine
wanahisi wanabakwa, wengine wanaona
wakipigwa au kukimbizwa na matukio mbali mbali
ya kutisha.
Kukabwa na Jinamizi kama tunavyoiita
kunatokana na sababu nyingi, ya kwanza kabisa
ni jinsi wewe mwenyewe ulivyolala, mara nyingi
unapolala chali mambo hayo yanakutokea, au
ukiwa na jambo linalokusumbua kimaisha ambalo
huwezi kulitatua linaweza kukuletea kukabwa na
Jinamizi.
Sababu nyingine ni mazingira unayoishi au eneo
ulilopo kama kuna makelele, au chumba kisicho
na hewa ya kutosha au kuwa na mawazo kuhusu
jambo fulani, au kulala na njaa au ukiwa umelala
umekasirika au ndoto unazoota.
Njia ya kwanza ya kupambana na tatizo hili ni
kujaribu sana lisikutokee, unatakiwa ujaribu kujua
kitu gani kinakusababashia wewe kupata matatizo
hayo, mfano ukijua kwamba kila ukilala chali
unakabwa basi badilisha ulalaji wako, lala upande
au lalia tumbo.
Ikiwa unakabwa ukiwa umelala usiku sana, au
umefanya kazi ngumu, Jaribu kubadili muda wako
wa kulala au punguza kufanya kazi mpaka
ukachoka.
Njia nyingine ni kuhakikisha unapata muda mrefu
wa kulala na umepunzika kabla ya usingizi
haujakuja.
NJIA ZA HARAKA ZA KUEPUKANA NA KUKABWA
NA JINAMIZI
1.Ikikutokea hali hiyo jaribu kuvuta pumzi nyingi
ndani kwa sababu pumzi peke yake ndio
unayoweza kuidhibiti ukiwa umekabwa.
2.Jiepushe kulala chali.
3.Punguza mawazo mengi.
4.Lala katika muda mzuri na jaribu kupata muda
mrefu wa usingizi masaa 8 mpaka 10.
5.Jaribu kuwa na muda maalum wa kulala ikiwa ni
saa 3 basi iwe muda huo wakati wote.
6.Jaribu kula vizuri kabla hujalala.
7.Kumbuka kwamba pamoja ya kuwa hali hii
inatisha lakini haina hatari yoyote.
8.Ukihisi unakabwa jaribu sana kujitingisha, hali
ya kukabwa itakwisha.
9.Ukiona kama unataka kukabwa amka kaa chini
kwa dakika 5 halafu lala tena.

  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger