KATIKA MAPENZI ZINGATIA CHAGUO, SI KILA MFAA MACHO ATAKUFAA
Mathalan,
mwenzi wako anatimiza kila kitu unachohitaji. Anageuka mtu wa ndiyo na
kutekeleza kila ombi lako. Wewe unajiona unatisha kwa kuona kwamba
mwenzi wako anakunyenyekea unavyotaka. Kumbe mwenzako ana malengo yake,
mkishaingia faragha na kukidhi haja zake, ule unyenyekevu wake wote
unaondoka, anarudi kuwa yuleyule.
Mwenzi wako ana asili ya kiburi,
mara nyingi ombi lako la kukutana naye faragha hulitolea nje kwa maelezo
kwamba eti huwa hajisikii. Lakini anapokuwa na shida ya pesa, anakuwa
mpole, kiburi chake chote kinapotea. Hakawii kukwambia ana hamu na wewe.
Akili ikae kichwani kwako.
Mfano: Msomaji wangu ambaye naomba
nimtaje kwa jina moja la Bryson, aliwahi kunilalamikia kwa njia ya simu,
kuhusu tabia ya mke wake. Akadai kuwa wakati mwingine hafikirii kama
aliyemuoa ni mke wake, ila changudoa anayetaka kuvuna kwake. Akaenda
mbali zaidi kwa kusema anahisi mkewe ana kidumu nje ya ndoa yake.
Akaeleza
kwamba yeye na mkewe tofauti yao kubwa huwa ni usiku wakati wa kulala.
Kila anapomhitaji mkewe hukutana na vizingiti visivyokwisha. Visingizio
ni vingi, mara ooh, leo nilifanya kazi nyingi, nimechoka sana, siku
nyingine ooh, leo nimezunguka sana, hapa mapaja yote yamechubuka.
Kwa
mujibu wa Bryson, visingizio vya mkewe huwa haviishi. Pale ambapo
husisitiza, hutokea ugomvi mkubwa kiasi kwamba hata majirani hutambua
kwamba kuna kimbembe chumbani kwao. Hii ndiyo inamfanya Brayson ahisi
kwamba mkewe ana kidumu pembeni ambacho hutimiza haja zake.
Bryson
akae-ndelea kueleza kuwa inapotokea mkewe ana shida ya pesa, siku hiyo
ataanza kumtumia SMS za mapenzi siku nzima. Atamsisitiza awahi kurudi
nyumbani kwamba ana hamu naye, wakati mwingine hudanganya analia kwa
madai eti, ‘amemmisi’ kupitiliza.
Anaweza kuandika SMS yenye sura
hii: “Mume wangu leo uje na shilingi 100,000, kuna nguo nataka ninunue,
ukija nayo usiku nitakupa.” Wakati Bryson anatafakari jinsi ya kujibu,
mkewe anatuma SMS nyingine: “Yaani tuache utani, ukweli nimekumisi. Leo
jiandae kabisa, lazima tukeshe.”
Bryson akichelewa kujibu, mkewe
ataandika SMS nyingine: “Nakupenda sana mume wangu. Usichelewe kurudi,
leo nina mzuka wa ajabu na wewe, si unajua ni wewe ndiye unayenipatia?”
Punde tena, SMS nyingine: “Mbona hunijibu, najisikia vibaya mpaka nalia
peke yangu, hiyo tabia gani ya kunichunia?”
Msomaji wangu huyo
akaeleza kwamba kimbembe hujiri pale anapofika nyumbani. Hukuta kila
kitu kimebadilika. Mandhari huwa ni nzuri, mkewe huwa mchangafu kupita
siku zote. Hata huduma za nyumbani, huwa zipo juu kupita maelezo.
Akifika atafunguliwa vifungo vya shati na kuvuliwa shati kwa
unyenyekevu.
Atafunguliwa kamba za viatu na kuvuliwa viatu kwa
madaha. Atapelekwa mezani kula, baadaye bafuni kuoga, huko ataogeshwa
naye atabaki amesimama tu kama mlingoti. Atatolewa huko na kupandishwa
kitandani, wakati wa kulala atafanyiwa ‘masaji’ na kubembelezwa kwa
sauti tamu, iliyonakshiwa na tundu za pua.
Ikifika wakati wa tendo, katikati ‘romansi’, mke huulizia ile shilingi 100,000 aliyoomba.
Itaendelea