Headlines News :

Sunday, March 9, 2014

IMANI YAKO NDIO ITAKAYOKUPONZA

Photo: Salome alifunga ofisi yake na kwenda benki kuchukua fedha kwa ajili ya ada ya mwanae aliyekuwa akisafiri siku ya pili kwenda shuleni.

Mita chache baada ya kuchukua fedha akiwa anaelekea kupanda gari akakutana na mama mmoja aliyekuwa akiomba msaada wa fedha ya kula yeye na familia yake.

Kwa huruma ya kumwona mama mwenzie akitia huruma kuomba msaada wa chakula cha yeye na familia yake akafungua mkoba wake na kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpa.

Alipofika nyumbani akashangaa kuona fedha zote kwenye mkoba zimetoweka na hakuwa na jinsi zaidi ya kulia kwa huzuni kwani hata alipofika ule mtaa alikomsaidia yule mama hakukua na dalili zozote za yule mama.

Suphiani yeye alitembelewa na baba mmoja dukani kwake na kumwomba msaada wa chenji ya shilingi elfu kumi.

Saa moja baada ya yule baba kuondoka suphiani hakuamini kuona droo yake ya fedha ikiwa tupu kwani hela zote zimetoweka.

Sara alibahatika kuwa dada mjasilia mali na alijiimarisha sana katika shughuli zake.

Akabahatika kukutana na rafiki mmoja wa kike walioshibana sana na kushauriana sana katika biashara.

Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa sara yule rafiki alimpa zawadi ya mkufu mzuri sana ambao kamwe sara hakutamani kuutoa mwilini mwake kwa jinsi ulivyompendeza.

Siku hadi siku sara akashangaa kuona biashara yake ikizidi kushuka na kuporomoka kwa kasi kabla ya kwenda kanisani na kuombewa na kwa mshangao ule mkufu ukabadilika na kuwa kamba ya ajabu mfano wa hirizi.

Hirizi ile ikaongea kuwa alipewa sara na rafiki yake ili impotezee mafanikio yake na kumwacha maskini wa kutupwa atakaye hangaika maishani.

Ndugu kumbuka sio kila mtu unayemsaidia ana mpango mzuri kwako na sio kila zawadi unayopewa ina maana ya kukupa furaha.

Kila utakachokipokea kumbuka kukikabidhi mikoni mwa Mungu na kuomba ulinzi wake.

Sala yangu kwako

Kila msaada utakao utoa na uende kwa mhusika na Mungu akupe mara kumi ya kila utakachokitoa na kukubarikia furaha.

Kila zawadi utakayoipokea daima ikupe furaha na kukuongezea mafanikio na sio kukuibia mafanikio.

Comment AMEN na kisha share ujumbe huu kama nawe waamini ulinzi wa Mungu kwa kila unachokitoa na kukipokea.
Mikasa zaidi tembelea ... http://dlvr.it/52bxnxSalome alifunga ofisi yake na kwenda benki kuchukua fedha kwa ajili ya ada ya mwanae aliyekuwa akisafiri siku ya pili kwenda shuleni.

Mita chache baada ya kuchukua fedha akiwa anaelekea kupanda gari akakutana na mama mmoja aliyekuwa akiomba msaada wa fedha ya kula yeye na familia yake.

Kwa huruma ya kumwona mama mwenzie akitia huruma kuomba msaada wa chakula cha yeye na familia yake akafungua mkoba wake na kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpa.

Alipofika nyumbani akashangaa kuona fedha zote kwenye mkoba zimetoweka na hakuwa na jinsi zaidi ya kulia kwa huzuni kwani hata alipofika ule mtaa alikomsaidia yule mama hakukua na dalili zozote za yule mama.

Suphiani yeye alitembelewa na baba mmoja dukani kwake na kumwomba msaada wa chenji ya shilingi elfu kumi.

Saa moja baada ya yule baba kuondoka suphiani hakuamini kuona droo yake ya fedha ikiwa tupu kwani hela zote zimetoweka.

Sara alibahatika kuwa dada mjasilia mali na alijiimarisha sana katika shughuli zake.

Akabahatika kukutana na rafiki mmoja wa kike walioshibana sana na kushauriana sana katika biashara.

Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa sara yule rafiki alimpa zawadi ya mkufu mzuri sana ambao kamwe sara hakutamani kuutoa mwilini mwake kwa jinsi ulivyompendeza.

Siku hadi siku sara akashangaa kuona biashara yake ikizidi kushuka na kuporomoka kwa kasi kabla ya kwenda kanisani na kuombewa na kwa mshangao ule mkufu ukabadilika na kuwa kamba ya ajabu mfano wa hirizi.

Hirizi ile ikaongea kuwa alipewa sara na rafiki yake ili impotezee mafanikio yake na kumwacha maskini wa kutupwa atakaye hangaika maishani.

Ndugu kumbuka sio kila mtu unayemsaidia ana mpango mzuri kwako na sio kila zawadi unayopewa ina maana ya kukupa furaha.

Kila utakachokipokea kumbuka kukikabidhi mikoni mwa Mungu na kuomba ulinzi wake.

Sala yangu kwako

Kila msaada utakao utoa na uende kwa mhusika na Mungu akupe mara kumi ya kila utakachokitoa na kukubarikia furaha.

Kila zawadi utakayoipokea daima ikupe furaha na kukuongezea mafanikio na sio kukuibia mafanikio.

Comment AMEN na kisha share ujumbe huu kama nawe waamini ulinzi wa Mungu kwa kila unachokitoa na kukipokea.

MAMBO HAYA HUTAKIWI KUYAKOSA KAMA MWANAMKE KATIKA MTOKO WAKO

Mwanamke hatakiwi kukosa, Kitambaa, kipande cha kanga au kitenge au japo mtandio, Anti Bacteria Wet Tissue, Body Spray, HandLotion, kioo, lip bum or lip shine, Pafyum, kitana,Ped, Pesa kidogo, simu of course, diary, Pen, mouth Spray au Chewing gum nadhani hivyo ni vya muhimu vingine ni ziada tu.



HIZI NI SABABU SITA NA MUHIMU ZA KUMILIKI AKAUNTI YA TWITTER

Sina uhakika sana ila naanza kuandika hiki kipande nikiamini kwamba unajua nini maana ya mitandao ya kijamii(social networks). Siku hizi makampuni makubwa makubwa duniani yanaajiri wataalamu wa kitu kinachoitwa New Media/Social Networks.Wengi wao ni vijana wadogo tu ambao aidha ndio wametoka vyuoni au wamejiari kwa kutumia mitandao jamii.
Leo naomba nigusie kidogo mtandao wa Twitter na kwanini nashauri ujiunge nao.Endapo unatumia e-mail hivi leo basi ni wazi kwamba kama bado hujajiunga au kufungua akaunti yako ya Twitter,basi hivi karibuni itakubidi. Mimi binafsi ni mtumiaji wa Twitter japokuwa siwezi kujiita mtumiaji mkubwa kwani bado sijafikia spidi ya kupost zaidi ya mara kumi kwa siku.Spidi zangu zinatofautiana
Sababu ya Kwanza: Ni vizuri mapema kabisa ukachukua username yako. Kila siku majina ya watu yanazidi kuchukuliwa.Hakikisha umechukua lako mapema kwani tofauti na mitandao inayotoa huduma za barua pepe(e-mail),mtandao wa twitter.com ni mmoja tu. Kwa hiyo ukikuta jina lako limechukuliwa  utakuja kuishia au kupaswa kuchukua jina kama jumapachu76654256 kwa sababu tu twitter.com/jumapachu itakuwa imechukuliwa
Sababu Ya Pili: Nenda na wakati kwa kuelewa kinachoendelea katika ulimwengu wa tekinolojia ya mawasiliano.Hili ni muhimu zaidi kama una watoto au unatarajia kuwa na watoto. Mimi nina watoto.Ni muhimu kujua kinachoendelea mtandaoni kwani watoto wa siku hizi,tofauti na enzi zetu,wao ni watumiaji wazuri zaidi wa mitandao.Na huko,kwa bahati mbaya,wapo watu wasio na utu wala maadili.Usiposimamia usalama wao,utakuwa unafanya makosa kama mzazi.Chukua hatua,nenda na wakati.
Sababu Ya Tatu: Ni jambo la hakika kwamba ukianza kutumia Twitter au mitandao jamii mingine,utajifunza mambo kadhaa na bila shaka utafurahia. Kama unapenda kusikia “umbea” au udaku utaukuta katika Twitter.Kama unapenda kujua mambo kadhaa kuhusu maendeleo ya ulimwengu wa mtandao,habari za papo kwa papo(breaking news),habari za masoko ya hisa,nk.Yote hayo unaweza kuyapata kwa haraka sana kupitia mtandao wa Twitter.
Sababu Ya Nne: Kama una wasiwasi au uoga kwamba mtandao wa Twitter pengine ni mgumu sana kuuzoea au kuutumia,naomba nikuhakikishie kwamba ni rahisi sana kuutumia.Lugha inayotumika,ujuzi au ufundi wa kuingia na kutoka,kutuma vitu,nk ni jambo rahisi sana kulielewa.Ukishaanza tu kuutumia,utaona jinsi wengine wanavyofanya na utaelewa ilivyo rahisi.Kwa hiyo ni rahisi kuutumia,shaka ondoa.
Sababu Ya Tano: Baadhi ya watu wamewahi kuniambia kwamba wanahofia kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter kwa kuhofia usalama wa habari zao au kupunguza uwezo wako wa kufikiri(zimewahi kutolewa hoja za namna hiyo kwa wanaopinga matumizi ya Twitter na mitandao jamii mingine).Kama ilivyo rahisi katika kujiunga ni rahisi pia kujiunga bila kujulikana na kila mtu(labda wewe mwenyewe na watu wako wa karibu sana) na pia ni rahisi kujitoa.Usalama upo.Habari kwamba Twitter wanachofanya ni kuisaidia serikali ya Marekani katika kukusanya taarifa za watu,nchi nk hazina msingi wala utafiti wa hakika wa kiinteligencia.
Sababu Ya Sita: Twitter na mitandao mingine ya kijamii sio sehemu tu ya “wateja” au “walevi” wa masuala ya mitandao au jamii, ni sehemu ya watu wote wanaopenda kujifunza jambo moja au jingine kutoka kwa watu au kubadilishana maarifa. Kwa mfano,mojawapo ya mambo ambayo mimi binafsi nayafurahia sana katika utumiaji wangu wa mtandao wa Twitter ni pamoja na kusoma au kupata habari.Kwa sababu takribani vyombo vyote vya habari duniani vinazo akaunt zao maalumu za Twitter,basi upatikanaji wa habari zote muhimu kupitia mtandao huo ni rahisi. Utasoma na kujifunza mengi kutoka kwa watu,vyombo vya habari nk.Jiunge na Twitter leo. Bonyeza hapa kufanya hivyo.
Je,kama wewe unayesoma habari hii tayari unatumia mtandao wa Twitter,nini maoni yako kuhusu Twitter.Unakubaliana na sababu hizo hapo juu? Unazo za nyongeza au za kupunguza? Account yako ya Twitter ni ipi ili “tukufuate”?

Friday, March 7, 2014

KIPI KINACHO 7BISHA MWANAMKE KUKOSA HEDHI (AMENORRHEA)


Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).

Primary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au nywele za kinena; au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.

Secondary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.
Mwanamke hupataje hedhi?

Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus napituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.

Amenorrhea husababishwa na nini?
Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.

1. Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.

1. Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na
-Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary
-Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi. Ugonjwa huu hujulikana kama Kallmann syndrome
-Lishe duni na utapia mlo
-Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza)

2. Matatizo katika tezi ya Pituitary: Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na
- Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamuProlactinemia. Prolactin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.
-Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.
-Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
-Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
-Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

3. Matatizo katika ovary: Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na
-Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)
-Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia)
-Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa
-Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake
-Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao humbatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida. Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease)
-Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji
-Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili
-Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary
-Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu

2. Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi: Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na

1. Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke, shingo ya uzazi au mji wa mimba (uterus)

2. Kuta za uterus zinazotazamana kujishikiza pamoja

3. Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen)

4. Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka

3. Mabadiliko katika mwili wa mwanamke: Mambo yanayoweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na

1. Kula kiasi kidogo sana cha chakula kuliko kawaida au kula kupita kiasi
2. Unene uliopitiliza au kupungua uzito/kukonda isivyo kawaida
3. Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu
4. Utapiamlo
5. Msongo wa mawazo
6. Matumizi ya madawa ya kulevya
7. Matumizi ya baadhi ya madawa hususani baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili
8. Kuwa na hofu iliyopitiliza
9. Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi

Dalili za Amenorrhea ni zipi?
Kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na
• Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo
• Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen
• Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovary
• Kuongezeka uzito kupita kiasi au kupungua kwa uzito isivyo kawaida
• Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida yaweza kuashiria kuwepo kwa matatizo ya kiakili na kisaikolojia

Je kukosa hedhi kunaweza kusababisha nisipate mtoto?
Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo halitashughulikiwa.
  • World News

     
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger