Mkurugenzi alipotazama CV ya Yule kijana aligundua kijana alifaulu vizuri sana shuleni kutokana na alama zake kuwa kubwa hivyo akamuuliza swali yule kijana ,
“JE uliwahi kupata udhamini wowote ule shuleni?
Kijana akajibu, “HAPANA”
Je ni baba yako aliyelipia karo zako za shule? “
Baba yangu alifariki nikiwa na umri wa mwaka mmoja hivyo mama ndiye aliyenilipia kila kitu” Kijana akajibu,
" Mama yako anafanya kazi wapi?”
“Mama yangu ni dobi.” Kijana akajibu tena.
Mkurugenzi akamwambia kijana amwoneshe mikono yake, na kijana akaonesha mikono yake miwili ikiwa milaini na isiyo na tatizo.
. ” Je umewahi kumsaidia mama yako kufua nguo ? “
HAPANA,mama alitaka mimi nisome hivyo muda wangu niliutumia kusoma vitabu vingi.
Lakini pia , mama anaweza kufua nguo haraka zaidi kuliko mimi. Mkurugenzi akasema ninaomba nikuombe kitu, ukirudi nyumbani leo naomba umwombe mama umwoshe mikono yake kasha uje kesho asubuhi.
Kijana akaona nafasi ya kupata kazi ile ilikuwa na matumaini akarudi nyumbani na kumwomba mama yake kuosha mikono yake .Mama alipatwa na mshangao wa furaha ila hakutaka mwanae ajue akiwa na mawazo pia akampa mwanae mikono aioshe.
Kijana akaiosha mikono ya mama yake taratibu na machozi yakaanza kumtoka kila alipoendelea kuiosha mikono ya mama yake. Ilikuwa ni mara ya kwanza kugundua kuwa mikono ya mama yake iliharibika ina magamba na pia imechubuka baadhi ya sehemu huku ikimpa mama maumivu kwa baadhi ya vidonda kila alipojaribu kushika maeneo hayo.
Kiukweli pia ilikuwa ni mara ya kwanza kugundua ni mikono hiyo hiyo yenye maumivu hayohayo iliyofua nguo pamoja na maumivu hayo ili kijana asome shule, na kuwa michubuko ile kwenye mikono yalikuwa ni malipo aliyopata mama ili kijana apate elimu bora, maisha mazuri na kuwa na malengo bora ya baadae..
Baada ya kuosha mikono ile akamalizia kufua nguo zilizosalia pia .Usiku ule mama na mwanae waliongea kwa muda mrefu sana na siku ya pili kijana akaenda kwa Yule mkurugenzi.Mkurugenzi akagundua kijana alikuwa katoka kufuta machozi, “ Unaweza
kuniambia jana umefanya nini na kujifunza kutoka kwa mama?”
Kijana akajibu, “Niliiosha mikono ya mama na kasha nikamalizia kufua nguo zilizosalia”
“Sasa natambua nini maana ya shukrani mbele ya mama yangu, nisingeweza kuwa hapa au kuwa hivi nilivyo nilipo bila ya yeye.
Kwa kumsaidia mama jana nimegundua jinsi ilivyokuwa ngumu na ilivyo vigumu kupata kile ukitakacho ukiwa peke yako ".
Mkurugenzi akasema, “ Na hicho ndio ninachokitafuta kwa meneja wa hii ofisi.Nataka kumtafuta meneja atakayeshukuru na kuihamini michango ya wengine, mtu atakayetambua maumivu na machungu yaw engine wanao au waliojitoa ili kufanya mambo yawe hivi yalivyo, na mtu ambaye hataweka fedha kama mpango wa peke yake katika maisha…..” “Hongera sana kijana UMEAJIRIWA KMENEJA”
Kijana huyu alijituma kila siku katika majukumu yake na alipokea heshima kutoka kwa wafanyakazi wenzake na alifanya kazi kwa kushirikiana na wenzake kama timu moja na ufanisi wa kampuni ukaongezeka mara dufu.kampuni na kukubalika na wateja wengi
KUMBUKA
Mtoto ambaye analelewa kwa kudekezwa na kupewa kila atakacho atatengeneza tabia kichwani mwake ya kujiweka yeye wa kwanza katika maisha yake kwa kuona kila kitu ni halali yake.Atakuwa mjinga wa kutotambua nguvu na jitihada za wazazi wake katika kumkuza. Akiwa kazini atataka kila mtu amsikilize yeye na hatokubali kubadilika misimamo yake. Na akiwa meneja hatajua wala kuithamini michango na maumivu ya wafanyakazi wake katika kuipa kampuni yake faida na atakuwa mtu wa kuwalaumu tuu.
Unaweza kumfanya mwanao aishi katika nyumba kubwa, ajifunze kucheza kila aina ya gemu, kula chakula kizuri, kutyazama TV kubwa lakini ukiwa nje unakata nyasi, safisha nyumba palilia maua au bustani hebu jaribu kuwafundisha.
Baada ya chakula hebu nao nwasafishe meza na vyombo pamoja na kaka na dada zao sio kwa sababu huna fedha ya kuajiri wasaidizi au wasaidizi ndio wafanye tuu ila kwa sababu unataka kuwapenda katika njia za kweli kwani kuna siku nao watahitaji kuwa na majukumu kama hayo na familia zao.
Cha msingi zaidi, je wanao wanajifunza kuthamini na kushukuru na kupitia magumu na uwezo wa kujifunza kufanya kazi na wenzao ili kufanikisha kazi zako?