Mtoto aliyebebwa ndani ya sanduku kama alivyoonekana kwenye kamera za usalama
Mtoto mmoja
wa miaka minane amesafirishwa hadi nchini Uhispania kutoka Morroco akiwa
ndani ya sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Uhispania.
Mvulana huyo
kwa jina Abou alipatikana ndani ya sanduku hilo lililokuwa limebebwa na
msichana wa miaka 19 kuelekea Cueta,eneo lililo karibu na taifa la
Morrocco siku ya alhamisi.
Wakati
polisi walipolifungua sanduku hilo, mvulana huyo alikuwa katika hali
mbaya sana.Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anahudumiwa na mamlaka
ya Cueta.
Gazeti la
Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa miaka 19 hana
uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba sanduku
hilo.
Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba alitarajia kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.
Chombo cha
habari cha Uhispania Efe kimesema kuwa babaake mvulana huyo ambaye
anajulikana kama Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast kumchukua
mwanawe baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka 2013.
Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.
Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama ambaye hakutaka kupitia mpakani''.
CREDIT: BBC