Kwenye miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na matumizi ya wanyama na
viumbe wengine kwenye kutabiri matokeo ya mechi za soka hasa kwenye
michuano mikubwa kama kombe la dunia.
Mwaka 2010 wakati wa WOZA, nchini Ujerumani kulikuwa na Pweza
‘Octopus Paul’ ambaye alitabiri mechi zote na akapatia kila utabiri,
mwaka huu amekuja Ngamia aitwaye Shakeeen kutoka Dubai ambaye nae
alianza kutabiri tangu siku ya kwanza.
Shakeen ambaye anamilikiwa na shabiki mmoja wa timu ya soka ya Al
Wasry ya Dubai, alitabiri mechi zote za ufunguzi na akapatia, akatabiri
ushindi wa Italy dhidi ya England akapatia, jana akaitabidi ushindi
Ufaransa na Argentina akapatia tena.
Pia ameitabiria Ureno kushinda mechi ya leo dhidi ya Ujerumani.