Headlines News :

Tuesday, February 18, 2014

"SASA TUNAKUJA" - JUAN MATA

JUAN_MATA-AON_JERSEY
JUAN MATA anaamini kuwa Manchester United itamaliza Ligi Kuu England Msimu huu ilikwemo 4 Bora na hivyo kufuzu kucheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Kwa sasa, Man United, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa England, wapo Nafasi ya 7 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Liverpool ambao wapo Nafasi ya 4 ambayo ndio ya mwisho kwa Timu kuchezea UCL Msimu ujao.
Lakini Juan Mata, Mchezaji wa Kimataifa wa Mabingwa wa Dunia Spain aliehamia Man United kutoka Chelsea Mwezi Januari kwa Dau la Rekodi ya Klabu la Pauni Milioni 37.1,
amesisitiza Kikosi chao kinachocheza chini ya Meneja David Moyes ni kizuri kushindana na Klabu yeyote huko England.

MAN UNITED-Mechi hadi mwisho wa Msimu:
[Zote Ligi Kuu England isipokuwa inapotajwa]
Feb 22: Crystal Palace v Man United
Feb 25: Olympiakos v Man United [UCL]
Machi 8: West Brom v Man United
Machi 16: Man United v Liverpool
Machi 19: Man United v Olympiakos [UCL]
Machi 22: West Ham v Man United
Machi 25: Man United v Man City
Machi 29: Man United v Aston Villa
Apr 5: Newcastle v Man United
Apr 12: Man United v Hull
Apr 19: Everton v Man United
Apr 26: Man United v Norwich
Mei 3: Man United v Sunderland
Mei 11: Southampton v Man United
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Mata amesema: “Sasa tunakuja na nadhani tunaweza lakini inabidi tushinde Gemu nyingi! Lengo ni kufikia nafasi za UEFA CHAMPIONZ LIGI!”
Mata aliongeza: “Ni ngumu kwa sababu Liverpool wanafanya vyema, pia Arsenal, pamoja na Tottenham na Everton, wote wanapigania nafasi hizo lakini tunayo Timu ambayo inaweza kufanya hilo! Hii ni Manchester United. Klabu hii ikishinda Mechi mbili, tatu au nne ni kwa sababu ina fikra za ushindi!”
Akiongea kuhusu David Moyes, Mata, mwenye Miaka 25 na ambae yeye pamoja na Kikosi chote cha Man United walikuwa huko Dubai kwa Mazoezi ya Siku 5 kwenye Hali ya Joto, amesema: “Uhusiano wangu na yeye ni mzuri na wa kirafiki. Tangu Siku ya kwanza alionyesha ni Mtu mwema. Alinifanya nijisikie muhimu. Nilijisikia vyema aliponambia: ‘Juan, wewe ni muhimu kwa Timu na tunataka umiliki Mpira kila mara!’ na hilo ndio najaribu kufanya!”
Vile vile, Mata alisema Moyes ataleta Wachezaji wengine wakubwa mwishoni mwa Msimu ili kuiibua upya Klabu.
Mata ameeleza: “Meneja amesema kuwa atasaini Wachezaji. Klabu hii sasa ipo kwenye hatua ya mpito, ya mabadiliko, na Klabu hii lazima Wachezaji bora watakuja!”
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger