
Kilichonitatiza sasa ni hiki: Miezi kadhaa iliyopita, binti amekuja kutuambia kuwa amepata mwanaume anayempenda wa kumuoa na kwa kuwa vijana wa siku hizi ni wasumbufu kwenye mapenzi wakiwa na vijana wenzao, amemkubali mwanaume huyo japo ni mtu mzima sana (anakaribia miaka 60). Kwa kuangalia hali yetu (mimi ni kijana na mama yake anaelekea uzee), tulishindwa kumkatalia.
Basi siku ikapangwa mwanaume aje kujitambulisha ili process nyingine zifuatwe. Kilichonishtusha sana siku ilipofika: Mwanaume huyo ni baba yangu mzazi ambaye kwa sasa anaishi mwenyewe kwa kuwa mama yetu alifariki miaka 10 hivi iliyopita. Baba yangu amekuwa akiishi mwenyewe tu, na kwa kuwa kipato chake kwa muda mrefu kilikuwa ni cha chini, hatukuwa na ukaribu sana kwani kila mmoja alikuwa anatafuta kivyake. Hata huyu mama (mke wangu) hajawahi kukutana naye.
Najiuliza: Niipinge hii ndoa? Kwa kuwa kama wakikubaliana kufunga ndoa, basi nitakuwa baba mkwe wa baba yangu mzazi. Na pia huyu binti mbali ya kuwa ni binti yangu (kwa huyu mama yake), pia atakuwa mama yangu (kwa baba yangu mzazi). Vipi wakizaa mtoto, nitamuitaje, mdogo wangu au mjukuu wangu?
Nimechanganyikiwa sijielewi, tafadhali naomba ushauri wenu!