Headlines News :

Wednesday, February 26, 2014

Mapenzi ya dhati si lazima mwenza wako akununulie vitu vya thamani na kukupatia pesa kila unapozihitaji.

Daima mwenza anayekupenda huonyesha upendo wake wa dhati kwa vitendo na hakuna kitabu wala mtaalamu ambaye anaweza kukufundisha namna ya kuonyesha upendo wa dhati kwa mwenza wako kwasababu kitendo hicho pekee hutokea kwa muhusika kiasili wanachofanya wataalamu ni kufundisha mambo mazuri katika mapenzi lakini ni muhimu wewe binafsi kujitambua na kukubali kile unachokifanya Mapenzi au upendo ni hisia ambazo hazitabiriki , na kumbuka upendo siyo kwa watu wenye fedha ambao wanadhani kwa kutumia pesa zao wataupata mapenzi hayaangalii kipato ila kipato ni sehemu ya maisha.




Unaweza kumuandalia mwenza wako zawadi yeyote kulingana na uwezo wako usijilazimishe kufanya mambo yaliyo nje ya uwezo wako

Zawadi kama Gari na vitu vingine vya thamani havikatazwi ila kuwa makini wakati unatoa zawadi hii angalia uwezo wako na je unayemnunulia ana mapenzi ya dhati kwako au anakupenda kutokana na zawadi za thamani unazompa. Mapenzi hayatabiriki hivyo ni muhimu kuwa makini wakati wote.

Use Facebook to Comment on this Post

  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger