Headlines News :

Thursday, October 24, 2013

MAPENZI NA KAZI ( Office Romance ) 2

Mapenzi mahali pa kazi au maofisini ni kitu cha kawaida sana kusikia siku hizi, hii ni kwa sababu kushuka kwa nidhamu makazini na kwamba tunatumia muda mwingi sana kuwa ofisini kuliko nyumbani hivyo wafanyakazi huwa na muda wa pamoja kuliko hata familia.

Urafiki wa mapenzi ofisini kama hujaoa au kuolewa unaweza kukusaidia kuoa au kuolewa au unaweza kukusababishia madhara makubwa kiasi cha kufukuzwa kazi au kufungwa jela na kupata magonjwa kama UKIMWI, kuharibu taaluma yako na sifa zako, pia kuvunja ndoa za wengine kitu ambacho ni hatari zaidi.

Pia suala la mapenzi kazini huweza kusababisha kuzorota kwa utendaji na ufanisi binafsi wa mtu kazini.
Mapenzi na kazi ni vitu viwili tofauti sana ndiyo maana waajiri wengi hawaruhusu watu kujihusisha ma masuala ya mapenzi kati ya wafanyakazi.

Pia kuna utafiti unaonesha kwamba (Vault.com) nusu ya watu wanaofanya kazi maofisini huvutiwa kimapenzi na mtu mwingine wa jinsia tofauti katika ofisi moja na wengine hupelekea hata kuoana kabisa.

"Si vema kuchanganya biashara, kazi na mapenzi ofisini"

Wapo watu wamejitoa muhanga kuwaridhisha mabosi wao kwa mapenzi ili kujihakikishia kupata kazi nzuri au kuongezewa mshahara, au marupurupu au kupewa visafari kikazi au kupelekwa kusoma nje ya nchi, hata hivyo matokeo yake ni kudhalilika na wakati mwingine kujipatia bonus ya magonjwa kama HIV/AIDS.
Pia wapo mabosi au waajiri ambao bila kutembea (sex) na mtu anayemwajiri bado hajakamilisha taratibu zake za kuajiri, hii ni tabia mbaya sana na si ya kistaarabu.

Je, hali ipoje katika ofisi yako kuhusiana na suala la mapenzi kazini au ofisini?
Je, katika ofisi zetu za serikali hali ipoje?
Na huko kwenye sekta binafsi hali ikoje?

Naamini kila mmoja wetu ana jibu kwa haya maswali
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger