Katika mapenzi zingatia chaguo, si kila mfaa macho atakufaa
Mpenzi
msomaji, bado naendelea kukudadavulia makala haya ambayo ukiyafuatilia
hadi mwisho utapata darasa tosha la mapenzi. Endelea...
Kila anapomhitaji mkewe hukutana na vizingiti visivyokwisha. Visingizio ni vingi, mara ooh, leo nilifanya kazi nyingi, nimechoka sana, siku nyingine ooh, leo nimezunguka sana, hapa mapaja yote yamechubuka.
Kwa mujibu wa Bryson, visingizio vya mkewe huwa haviishi. Pale ambapo husisitiza, hutokea ugomvi mkubwa kiasi kwamba hata majirani hutambua kwamba kuna kimbembe chumbani kwao. Hii ndiyo inamfanya Brayson ahisi kwamba mkewe ana kidumu pembeni ambacho hutimiza haja zake.
Bryson akaendelea kueleza kuwa inapotokea mkewe ana shida ya pesa, siku hiyo ataanza kumtumia SMS za mapenzi siku nzima. Atamsisitiza awahi kurudi nyumbani kwamba ana hamu naye, wakati mwingine hudanganya analia kwa madai eti, ‘amemmisi’ kupitiliza.
Anaweza kuandika SMS yenye sura hii: “Mume wangu leo uje na shilingi 100,000, kuna nguo nataka ninunue, ukija nayo usiku nitakupa.” Wakati Bryson anatafakari jinsi ya kujibu, mkewe anatuma SMS nyingine: “Yaani tuache utani, ukweli nimekumisi. Leo jiandae kabisa, lazima tukeshe.”
Bryson akichelewa kujibu, mkewe ataandika SMS nyingine: “Nakupenda sana mume wangu. Usichelewe kurudi, leo nina mzuka wa ajabu na wewe, si unajua ni wewe ndiye unayenipatia?” Punde tena, SMS nyingine: “Mbona hunijibu, najisikia vibaya mpaka nalia peke yangu, hiyo tabia gani ya kunichunia?”
Msomaji wangu huyo akaeleza kwamba kimbembe hujiri pale anapofika nyumbani. Hukuta kila kitu kimebadilika. Mandhari huwa ni nzuri, mkewe huwa mchangafu kupita siku zote. Hata huduma za nyumbani, huwa zipo juu kupita maelezo. Akifika atafunguliwa vifungo vya shati na kuvuliwa shati kwa unyenyekevu.
Atafunguliwa kamba za viatu na kuvuliwa viatu kwa madaha. Atapelekwa mezani kula, baadaye bafuni kuoga, huko ataogeshwa naye atabaki amesimama tu kama mlingoti. Atatolewa huko na kupandishwa kitandani, wakati wa kulala atafanyiwa ‘masaji’ na kubembelezwa kwa sauti tamu, iliyonakshiwa na tundu za pua.
Ikifika wakati wa tendo, katikati ‘romansi’, mke huulizia ile shilingi 100,000 aliyoomba. Bryson akijibu ipo, mke hutaka aoneshwe kabisa, akishawekewa mezani, basi hujituma kweli. Bryson hupewa ladha na mitindo ambayo hajawahi kupata. Endapo atasema fedha hana, mchezo huishia hapo, tena wakati mwingine mke huwa mkali kweli.
“Kipindi kingine mke wangu hulazimisha usiku huohuo twende kwenye ATM nikamtolee hiyo pesa. Nikisema benki sina akiba, mipango yote ya mapenzi inaishia hapo. Atanisimanga, mwisho tunalala mzungu wa nne. Nikifikiria hapa ndiyo maana huwa nasema mke wangu ni kama changudoa, hafanyi nami tendo la ndoa mpaka pesa,” anasema Bryson.
Inawezekana picha iliyopo kwako siyo sawa na ile ya Bryson lakini hebu fikiria upande wako, kama mwenzi wako anakuwa nawe kwa masharti, hebu jichenge. Upendo unaotakiwa hapa ni ule usiozingatia hali wala masharti. Ukipuuza hili, kaa ukijua kuwa ukiyumba katika kile ambacho anakupendea lazima atakuacha.

MWISHO.