Headlines News :

Thursday, February 20, 2014

CHOMBEZO : "ALAZWE PEMA"



Juhudi zangu za hapa na pale za kumlaghai binti huyu aingie kwenye himaya yangu ni kama zilikuwa zimegonga mwamba, niliamini kwamba kila neno tayari nimetumia katika kamusi yangu ya longolongo nilizojifunza jijini. Ulikuwa mfadhaiko mkubwa sana yani nilipokuwa mjini haikunichukua muda mrefu sana kumhangaikia msichana sasa hapa kjijini inakuwaje? “Nina mchumba wangu mjini” ndio lilikuwa jibu lake siku zote binti huyu aliyeitwa Ashura bint Zahor, hakuwa na uzuri wa kutisha hata kidogo lakini kwa pale kijijini aliongoza. “Eti ana mchumba mjini kha! mbona hata mi mjini nimefika, tena mie hadi Zenji nimeenda  japo kwa kula skukuu tu nimewaona akina Makomboa,Halikuniki, Asu, Munah, Baby J, na wengineo ambao yeye anaishia kuwaona kwenye tivii tu, huyo mchumba huenda mwisho wake hapo Chake Chake tu mh! Chake  napo mjini huyu mjinga nini??” ndivyo niliwaza, sikuamini likizo yangu ya mwezi mzima nimeambulia patupu yaani naondoka bila kumfaidi mtoto huyu wa kijijini. Alikuwa mwembamba sana wa umbo lakini kifua kilikuwa kipana siju kwa nini, miguu yake ilikuwa na dizaini flani ya ‘matege tusijuane’au kwa wa;e wachezaji wa mpira kuyaita ‘vigoli vidogo’ nywele ndefu zilizosukwa siku nyiingi zilizopita zilishikilia mamlaka ya kichwa chake, mkanzu wake mrefu huku akiwa amejifunga mkanga mmoja mkuu kuu alioshindia kutwa nzima ukiwa amejifunga kiunoni, kiasi flani alifanana na misukule bandia tunayodanganywa kwenye magazeti ya udaku huko bara  kuwa imetolewa na wachungaji mashuhuri wanaojipa majina ya mitume na manabii huku wengine wakifikia hatua ya kujiita Miungu watu.Lakini kutokana na hali yake ya siku hiyo usingeweza kumsema kwa lolote lile maana kila mtu aliijua. Licha ya yote hayo huyu mtoto kama akipata mtu wa kumtunza haki ya nani ni mzuri wewe, hivi unafahamu ladha ya binti mwenye ‘matege tusijuane’, achana na wale wenye ‘matege mbinuko’ hao hawana ladha sana kama hawa ninaozungumzia. Kweli Ashura  apate mtu wa kumtunza mbona asingejutia sema kwenye kile kifua ndio sielewi kama palikuwa na ujanja.
* * * *
Msiba wa babu yake Ashura  haukuwa wa kusikitisha sana kama misiba mengine kwani alikuwa anakaribia kutimiza miaka 95 umri ambao ni wachache sana kuufikia hivyo tuliamini ahadi yake ilikuwa imefika. Mimi pamoja na vijana wengine pale kijijini tuliungana katika shughuli nzima ya kuchimba kaburi hadi maziko kwa ujumla. Baada ya maziko, wengne walirudi makwao, lakini mimi na kundi jingine tulirudi kwenye msiba nyumbani kwao Ashura . Kwa ajili ya kuendelea kutoa mchango wa hapa na pale ikiwa kuna tatizo litaweza kujitokeza. Majira ya saa nne usiku nilikuwa chumbani kwa Ashura  nikimfariji “Jamani mi ngoja nikacheze karata nje” dada yake Ashura  aliyeitwa Faida aliaga na kutoka nje, pale ndani nikabaki mimi na Ashura , roho ikaniambia hiyo, kama ni mpira wa miguu basi ilikuwa ni penalt dakika ya tisini, goli la pekee la ushindi, hiyo ndio nafasi iliyobaki kujaribu bahati kama kweli Ashura  amenizidi ujanja ama inawezekana. “Kibatali kimeisha mafuta” Ashura  alisema baada ya kuona inafifia aliichukua akaitikisa kweli haikuwa na mafuta akawa ameirudisha mahali pake. “Ngoja tuizime eti!” nilizuga kuuliza wakati tayari nimeipiga pua. “Mjini ZECO huku mafuta safi sana!!!” nilijisemea baada ya giza kuchukua hatamu. Giza likachukua nafasi yake na ujasiri ukaongezeka maradufu aibu ikajificha hakika hiyo ndio ilikuwa nafasi ya kufanya uzinzi na Ashura . Ashura  alikuwa amelala na mimi nimekaa, taratibu mkono wangu ukapata kishawishi nikapapasa hadi nikatua kwenye mikono yake migumu, hata hakushtuka basi nikausogeza hadi kifuani pake nikasalimiana na mzigo wa titi moja nikalinganisha na matiti ya vitoto vya Kiunguja viwili. Nikaguna kisha nikendelea si unajua tamaa tena!!! “Jamani Shaibu kuna watu nje watatusikia, acha!!” alilalamika Ashura  nikacheka gizani kicheko cha kimya kimya nikayakariri maneno yake ‘watatusikia’ “Kumbe na yeye anajua kinachoendelea”, mi wala sikumjali nikapeleka na mkono wa pili weweeee! kifua kikubwa kama dari ya udongo, raha jamani dah! nikashangaa msimamo wangu wa kupenda chuchu ndogo ukianza kuyumbishwa na joto lililotoka pale ndani. Ulaini wake ukaitesa mikono yangu, uzito wake haukunisumbua!!! Ashura  akawa anahema kwa kasi nikatamani kupanda pale kitandani lakini nikahofia aibu ya kuporomoka kutoka katika kitanda kile cha kamba. Sikukiamini kabisa japo alikuwa amenambia awali kuwa kitanda kile walikuwa wanalala watu watatu wakati mwingine. Kwa jitihada nikamshusha hadi chini kwa kumbeba. Alikuwa mzito wewe!! Si alikuwa keshalegea!! Akiwa bado hoi nikaupeleka ulimi wangu masikioni mwake bila kujalisha ameyasafisha au la Ashura  akatoa milio ya mtu mwenye kifafa ambaye yupo katika hatua za mwisho kupoteza fahamu, nikautoa ulimi sikioni nikauhamishia kwenye shingo yake iliyokuwa na ladha ya chumvichumvi kutokana na jasho la kutwa nzima katika harakati za mazishi, hata sikuhofia chumvi hiyo kwani nimeshazamia chumvi kali kuliko hiyo tena si mara moja wala mbili, watoto wa Zenji si ndio burudani yao. Wamenifundisha tabia mbaya hao!!! “Mamaaaa mamaaaa” alipiga mayowe kwa nguvu, nikakurupuka pale lakini sikuweza kutoka alikuwa amenishikilia bila shaka alikuwa anataka huduma yangu. Nilijivuta ili nitoke lakini wapi Ashura  sijui hata alikuwa amezitoa wapi nguvu zile. “Acha kulia Ashura  eeh” nilibembeleza kwa uoga, lakini Ashura  aliendelea kulalamika kwa sauti ya juu, kelele zilifika hadi nje, hofu ikanitawala sana nilikuwa naenda kuaibika msibani sasa mtoto wa kiume mie. Watu wakaanza kulia huko nje wakiamini Ashura  anamlilia marehemu babu yake. Laiti kama wangejua chanzo cha ya kilio chake nadhani pangekuwa hapatoshi. “Jamani Ashura  ukilia utakuwa unakufuru sasa imetosha tumwombee marehemu ALAZWE PEMA PEPONI” nilizungumza hayo kwa sauti ya juu huku nikitoka nje nikimuacha Ashura  akiwa ndani analia kwa uhitaji tayari alikuwa ameiondoa kanga yake akabakia na mchupi mkubwa uliokuwa umelegea kiunoni au puru kama ambavyo tuzoeya kuyaita machupi ya kushona, watu wakaingia kumbembeleza baada ya kuwa wamesikia maneno yangu yaliyowachoma. Mimi tayari nilikuwa nje, hamu zote zikiwa zimeniisha. Sikuamini nimekwepa aibu hiyo japokuwa nilishindwa kutimiza lengo langu la kumfaidi Ashura .Kesho yake nikaondoka asubuhi na mapema kurudi zangu mjini na kurudi tena hapo kijijini sikutamani tena kwa kipindi hichi. Maana waliyoyakuta huko ndani walijua wao wenyewe mie sitaki kujua.
MWISHO
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger