Headlines News :

Friday, November 27, 2015

ZANZIBAR HEROES YAIGARAGAZA HARAMBEE STARS



Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup 2015, yameendelea tena leo November 27 Ethiopia, michezo iliyochezwa leo November 27 baada ya mapumziko ya siku moja ni mechi kati ya Zanzibar Heroes dhidi ya bingwa mtetezi wa Kombe hilo timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars.
Timu ya Zanzibar Heroes ambayo nafasi yake ya kuendelea katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kuwa ndogo, baada ya kukubali kufungwa mechi zake mbili za awali lakini leo November 27 haijakubali kuingia katika rekodi ya kumaliza mechi zake tatu za makundi kwa kipigo kama mechi zake mbili za awali.
Wachezaji-wa-Zanzibar-na-baadhi-ya-viongozi-wakimpongeza-Abdallah-Othman-katikati-aliyesujudu
Kenya wamekubali kupokea kipigo cha goli 3-1 kutoka kwa Zanzibar Heroes ambayo kuendelea katika hatua inayofuta kunategemea nafasi ya best looser kama watafanikiwa kupata nafasi hiyo, magoli ya Zanzibar Heroes yalifungwa na Kassim Suleiman dakika ya 45 na dakika ya 74 na Khamis dakika ya 57 wakati goli pekee la Kenya lilifungwa na Jacob Keli dakika ya 90. Kwa matokeo hayo Zanzibar ipo nafasi ya mwisho katika msimamo wa Kundi B wakiwa na point tatu.
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger