Headlines News :

Wednesday, July 9, 2014

BRAZIL YAGARAGAZWA 7 BILA NI UJERUMANI WOLD CUP 2014 USIKU HUU

Brazil imebwagwa vibaya kwenye nusu fainali ya
Kombe la Dunia kwa ushindi wa kihistoria wa
Ujerumani. Ujerumani imeitwanga Brazil mabao
7-1 yakiwa magoli mengi zaidi kuwahi kufungwa
na timu moja kwenye nusu fainali ya Kombe la
Dunia. Mvua hiyo ya magoli ilianza kwenye
dakika ya 11 paleThomas Thomas Müller alipotia
kimiani goli lake la tano kwenye michezo ya
mara hii ya Kombe la Dunia. Baadaye yalifuata
magoli 2 ya Toni Kroos na 1 la Sami Khedira .
Brazil iliyocheza bila ya nyota wake, Neymar Jr. ,
ambaye amevunjika mgongo, ilionekana kupata
uhai kwenye kipindi cha pili, lakini goli la sita na
saba pia likaenda kwa Ujerumani, pale André
Schürrle alipoongeza chumvi kwenye kidonda
kibichi cha Brazil. Oscar alitia kimiani goli la
pekee la Brazil katika dakika za mwisho, kikiwa
ni kifuta machozi kisicholeta faraja.

  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger