skip to main |
skip to sidebar
JEE UNAFAHAMU KUWA 70% YA WAAJIRIWA MAOFISINI HUTONGOZANA WAO KWA WAO? UTAFITI UNAONESHA HIVYO, SOMA HAPA KUFAHAMU HILO !
Utafiti huu unaweza kuleta taharuki kwa wanaume au wanAwake ambao wenzi
wao wanafanya kazi maofisini, yaani ambao wameajiriwa. Hii inatokana na
madai kwamba, katika kila waajiriwa kumi, saba wanatongozana na wenzao
wa ofisi wanamofanyia kazi.
Utafiti huu ambao ulifanyika hivi karibuni unakuwa kama vile ni msumari
wa moto kwa walio na wapenzi walioajiriwa, ambapo umebainisha kwamba,
saba kati ya kumi miongoni mwa waajiriwa wanatongozana, kutomasana au
kufanya mapenzi na wenzao wa ofisi moja, moja kati ya tatu ya hao
wanaotomasana, kutongozana au kufanya mapenzi , hufanya hivyo na
waajiriwa wenzao ambao nao wameoa au kuolewa.
Utafiti huo unazidi kubainisha kwamba, wanaopata hasara kwenye uhusiano
huu wa maofisini ni wanawake zaidi kuliko wanaume. Mtaalamu Geoff
Carter ambaye naye amewahi kufanya utafiti wa aina hii anasema kwamba,
wanawake ambao mara nyingi huangukia kwenye mikono ya wapenzi wa nje
ambao tayari wameoa, ndiyo ambao mara nyingi huumia kutokana na mapenzi
haya ya kiofisi.
Carter alifanya utafiti wake kwa kuwahoji mameneja wapatao 400, katika
utafiti wake huo alibaini kwamba wale walio kwenye umri wa miaka 18 hadi
30 ndio ambao wanafanikiwa kwenye uhusiano huu wa kiofisi. Lakini wale
ambao wana umri mkubwa zaidi wawe wanawake au wanaume, mara nyingi
huumia sana.
Ushauri uliotolewa a watafiti hao unawaasa wanawake kuacha kujiingiza
kwenye mapenzi na watumishi wenzao kwenye ofisi moja kwani madhara
yanayotajwa ni ule ukweli kwamba, mapenzi kwa watumishi wa ofisi moja
huzaa wivu, fadhaa, kujifunga na wasiwasi mwingi.