Headlines News :

Thursday, December 26, 2013

UMEWAHI ONA HII?


Nilikutana na mdada mmoja mtandaoni; siku tulipopanga kuonana alinifanyia surprise. Kwanza alinambia nimuelekeze ofisini ndo aanzie (alitoka mbali na nilikokuwa). Alifika ofisini tukasalimiana, then akaniaga na kunambia anatafuta hotel apumzike then atanicall ili tukae sehemu tuongee mawili matatu. Kwa namna nilivyomwona alivyokuwa classic ilinibidi niende benk kuongeza unene wa wallet.

Ilikua ni jumapili, hivyo kazi ilikuwa nusu siku. Muda wa saa 8 mchana wakati natoka kazini nilimpigia sm kumuuliza alipo - alinielekeza. Nilifika na kuuliza kama wana huduma ya msosi, bahati mbaya chakula alichokitaka yeye hakikuwepo (samaki wa kuchoma + ndizi za kukaanga) Ilitubidi tuondoke pale hadi Villar - Kirumba.

Mhudumu alikuja tukaagiza vinywaji na msosi kama kawaida; tuliendelea na maongezi huku tukitumia; ilipofika mida ya saa 2 hivi; nilimuita mhudumu ili nipewe bill nilipe tuendelee na mambo mengine; sauti toka kwa mrembo huyo ilisikika ikisema hivi "Sweetie naomba hiyo bill tuigawane kwani nami nafanya kazi kama wewe unavyofanya kazi na isitoshe una familia wakati mi bado niko single" Nilimwambia hakuna kabaya. Alilipia vinywaji mi nikalipia misosi.

Tuliondoka hadi hotelini na kuburudika kama kawaida. (Kumbuka chumba kalipa mwenyewe). Baada ya mechi niliondoka kwenda kujimwagia maji ili nisepe; nilirudi na kumpa kile nilichojisikia kumpa lakini alikataa kabisa kupokea hicho (pesa) basi tuliagana. Wakati niko njiani alinitumia sms na kunieleza kwamba kwenye mfuko wa koti wa ndani kuna bahasha niangalie then nimjibu.
Nilifungua hiyo bahasha nilikuta laki moja na cheni ya silver. Nilipomuuliza pesa ni za nini alicheka na kukata simu na kunitakia safari njema.
UMEWAHI ONA HII… (Endelea kutukana watu ovyo kwenye mitandao bila kuwajua ni akina nani uone kama utapata kama nilivyopata mimi)
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger