Monday, September 23, 2013
CHOMBEZO : FACEBOOK CHATTIN'
Najisikia nimechoka sana, nimechoka kupita kawaida kwa sababu nilikuwa nimetoka kucheza mpira uwanjani huku nikiwa nimechafuka kupita kawaida. Ninapofika nyumbani, ninaoga na kisha kuchukua simu yangu kwa ajili ya kuangalia updates za facebook, sikukuta hata meseji moja zaidi ya notification tu, tena wala hazikuwa nyingi. Nilichokifanya ni kuanza kuzugazuga hapa na pale na kisha kutulia. Mara ghafla nikaona namba moja nyekundu kwenye sehemu ya meseji, kulikuwa na meseji imeingia, nilichokifanya, nikaifungua na kuanza kuchati na mtu huyo huyo.
EDUADO: Mambo vipi Shahruk Khan.
MIMI: Hahahha! Poa. Inakuwaje wewe mtu.
EDUADO: Kama kawa. Nilikuwa nakusubiri sana online. Nilikuwa na mzuka na wewe ile mbaya.
MIMI: Duh! Mzuka na mimi! Kuna nini tena?
EDUADO: Kuna bonge la kazi hapa. Unataka?
MIMI: Kwa nini nisitake? Nipe mawasiliano yao niandike barua ya kuomba kazi fasta.
EDUADO: Hahahaha! Kaka unakosea. Niliposema kazi sikumaanisha hiyo.
MIMI: Wewe ulimaanisha ipi sasa?
EDUADO: Kazi moja hivi. Kazi ambayo watu wengi wameishindwa hasa masharobaro.
MIMI: Hahahaha! Itakuwa kubeba zege hiyo watoto wa mama hawaiwezi. Mimi naiweza, hebu niambie ni jengo gani.
EDUADO: Sio kazi ya kubeba zege. Kuna mtu nataka umfanyie kazi.
MIMI: Mtu gani?
EDUADO: Kuna demu fulani nipo nae hapa UDSM ni mkali ile mbaya. Yaani mkali mpaka nashindwa kusema ukali wake unafanana na nini.
MIMI: Hebu acha masihala kaka. Kwa hiyo kama mkali mimi nifanyeje nini?
EDUADO: Huyu demu anaringa mbaya. Yaani demu ananata utafikiri akanyagi ardhi hii tunayochimbia vyoo.
MIMI: Ok! Wazuri wapo wengi na hata wenye maringo wapo wengi pia. Hebu niambie kuhusu huyo. Kwanza anaitwa nani. Nipe maelezo ya kujitosheleza na sio naanza kumtengeneza demu mkali kichwani mwangu ikawa ndivyo sivyo.
EDUADO: Huyu demu anaitwa Aziza Moody, anaishi Msasani, baba yake ni mfanyabiashara mkubwa sana aisee. Ni demu fulani pini…yaani ni pini sana.
MIMI: Hebu acha masihala. Sasa inakuwaje watoto wa kisharobaro wamemshindwa.
EDUADO: Huyu demu hafagilii muonekano, ni demu fulani ambaye anapenda mtu anamfuate kama jinsi alivyo. Yaani kama wewe ni mtu wa chini, mfuate hivyo hivyo ila tatizo watoto wa hapa chuo wanapenda kumfuata kisharobaro kaka.
MIMI: Dah! Kwa hiyo kazi unayotaka kunipa ni ipi?
EDUADO: Umchukue huyu mtoto. Yaani ukifanikiwa, moyo wangu utakuwa mweupeeeeeee kama theluji.
MIMI: Hahaha! Usitake kunichekesha EDUADO, hivi unamkumbuka Sikitu?
EDUADO: Sikitu yupi?
MIMI: Si yule demu wa mwaka jana ambaye ulikuwa unamsifia sanaaaaa kwamba mkali kumbe wala hakuwa mkali kama ulivyokuwa ukimsifia, mbaya zaidi alikuwa anakaa Musoma.
EDUADO: Acha na hayo, yule msahau kwani mimi mwenyewe alinitumia picha ambayo sio yake. Ila kaka kiukweli Aziza ni demu mmoja mkali sana. Hapa chuo amekuwa gumzo kila kona, vijana wengi wamechemka.
MIMI: Sasa kama wengine wamechemka mimi nitaweza vipi?
EDUADO: Hahahaha! Kaka ninakuamini sanaaaa, wewe mtu unaweza sana kuongea, unaweza sana kuandika. Endapo kazi nikakupa na kisha ukashindwa, haki ya Mungu nitajua kweli duniani kuna wasichana wagumu.
MIMI: Kwa hiyo kazi yako ina malipo au?
EDUADO: Ikitokea umempata, nitakupa zawadi kaka. Yaani ninachokitaka huyu demu umchukue tu, basiiiiiiii. Anaringa sana, ananata sana, yaani sijui niseme vipi.
MIMI: Ila si anaringa kwa sababu mzuri?
EDUADO: Ndio. Ila yeye kazidi.
MIMI: Ila kwa sasa aisee nahisi nimepoteza kumbukumbu zangu za kuongea na hawa watoto wa kike, sijui kama nitaweza.
EDUADO: Acha kunitania kaka. Nakuamini sana kwamba unaweza kuliko mtu yeyote na ndio maana nikakufuata wewe. Hivi haujiulizi kwa nini sikumfuata Thomas? Thomas kwenye kuongea mkali sana ila kwenye kuandika hakuna kitu, ila wewe, aisee una kipaji kila kona, nafikiri hata ukimtokea kiziwi, hachomoiiiiiiiiii.
MIMI: Hahaha! Hebu acha kunipamba. Hebu niambie, huyo demu yupo Facebook?
EDUADO: Amejaa teleeee…yaani kajaa teleeee. Anajiita Aziza M Aziza. Ni demu mkali sana. Hebu mcheki kwanza.
MIMI: Sawa.
Sikutaka kuchelewa, tayari kichwa changu kikaanza kujazwa na sura nyingi za wasichana wazuri huku nikianza kuzigawanya kimakundi kwamba huyu alikuwa Aziza mwenyewe huyu hakuwa mwenyewe. Nilikuwa namfahamu EDUADO toka tupo katika shule ya sekondari ya Mbezi High School, alipokuwa akisema msichana fulani ni mzuri, mzuri kweli japokuwa kwa Sikitu alikuwa ameniingiza choo cha kike. Sikutaka kuremba, mara baada ya kuona majina kadhaa, nikamfuata EDUADO inbox.
MIMI: Oyaa Akshey.
EDUADO: Vipi ushampata?
MIMI: Wamekuja wakina Aziza wengi hao, mpaka wengine wanakaa India.
EDUADO: Hebu subiri.
Sikujua alikuwa akifanya nini, kwa sababu aliniambia kwamba nisubiri, wala sikuwa na presha, nikamsubiri nione angeniambia kitu gani baada ya hapo. Nilimsubiri kwa kipindi kama cha dakika moja hivi, akanijia tena inbox.
EDUADO: Umeiona hiyo picha yenye mdoli wa Barbie?
MIMI: Yeah!
EDUADO: Ndiye yeye huyo. Nyemo huyo ni demu mkali ambaye sijawahi kuona.
MIMI: Acha utani.
EDUADO: Sure. Unamkumbuka Silvia wa Mbezi High, sasa Silvia haingii kwa Aziza.
MIMI: Acha utani kaka. Silvia haingii?
EDUADO: Kweli tena. Tena hagusi hata robo.
MIMI: Sasa mbona hajaweka picha yake, nitamjua vipi kama ni mkali. Hebu nipe sifa kwanza manake naona picha zake kazipiga pini watu wasio marafiki zake wasizione.
EDUADO: Kwanza demu ni pini sana, demu kwao wana mahela ya kumwaga, chuo anakuja na gari, Verrosa moja nyeusi, mtoto anamiliki laptop aina ya Apple ile inaayouzwa milioni tatu, mtoto anamiliki anamiliki iPhone 5 huku akisema kwamba mwezi ujao iPhone 6 ikianza kuuzwa atataka kuanza kuitumia kwani anapenda kwenda na wakati.
MIMI: Kaka utakuwa unanitania tu.
EDUADO: Kweli tena.Halafu kuna cha zaidi.
MIMI: Kipi?
EDUADO: Otea.
MIMI: Hebu niambie kipi?
EDUADO: Ugonjwa wako.
MIMI:Unamaanisha nini?
EDUADO: Mtoto Mpemba.
MIMI: Hahahaha! Kaka acha utani, utanifanya nimfuate sasa hivi.
EDUADO: Ndio hivyo. Mtoto ni pini sana, pini ile iliyosimama.
MIMI: Hahaha! Pini kama ya Blackberry vile.
EDUADO: Acha kaka. Mtoto ni pini zaidi ya zile za Blackberry. Kwanza ukimuona tu, mtoto utampenda. Mavazi yake sasa…weeeeeee.
MIMI: Hebu nipe sifa zake kwa ujumla.
EDUADO: Nisikilize. Mtoto ni wa kipemba. Ana nywele ndefu zinazomfikia chini ya mabega yake, mtoto ana hipsi zilizopangika, hapa mashavuni mwake ana vijishimo viwili, lipsi lainiiiii kila wakati zinang’aaaaa.
MIMI: Kingine?
EDUADO: Mtoto ana sura zile nyembamba zile, masikio hayaonekani sana, kifuani hapa kumesimama vizuri sana, mavazi yake huwa ni suruali za jinsi kwa sana.
MIMI: Umesema anaishi wapi?
EDUADO: Anaishi Masaki.
MIMI: Halafu mimi naishi uswahilini Tandale. Umesema anamiliki simu gani?
EDUADO: Anamiliki iPhone 5.
MIMI: Halafu mimi namiliki Huawei. Umesema baba yake ana gari?
EDUADO: Yeah! Yeye mwenyewe analo.
MIMI: Mimi sina gari na baba yangu hana hata gari.
EDUADO: Acha kujizarau Nyemo. Mtoto unang’oa huyu.
MIMI: Usijali. Ushawahi kufika kwao?
EDUADO: Yeah kaka. Kwanza hiyo nyumba yao….duh! Kuna watu wanakufuru. Kwanza bonge la nyumba. Limezungushiwa ukuta, jumba lina fensi kwa juu, ndani kuna kamera, nyumba vigae, ukiingia ndani unakutana na bwawa la kuogelea. Kuna ungo wa Dstv, kuna bustani kali ya maua mbalimbali, kuna walinzi wawili ambao wanalinda kwa bunduki kutoka Knight. Yaani wapo full.
MIMI: Ok! Mimi naishi Tandale. Nyumba yetu ndogo, haina ukuta wala fensi, haina mlinzi na kama kuogea, tunaogea bafuni na si kwenye bwawa. Mpaka hapo, nimeshamkosa.
EDUADO: Nyemo. Usiniangushe. Yaani mimi lengo langu umchukue huyu mtoto tu.
MIMI: Una namba zake za simu?
EDUADO: Hapana.
MIMI: Basi ngoja nifanye mishe halafu nione itakuwaje. Ila wasiwasi wangu ule ule tu, itakuwa kama Sikitu.
EDUADO: Usijali kaka. Huyu sio kama Sikitu. Kwanza yule demu mwenyewe alinitaka nikaamua kukurushia wewe. Mimi na demu wa mkoa wapi na wapi. Ishi Dar tuwe tunamalizana, mambo ya mikoani haya, tigo pesa zinatumika sanaaaa. Hapa hapa Bongo ndio kuzuri, ukimtaka tu, nauli yako sh 400 kwenda, 400 kurudi. 600 soda yako, 600 soda yake. Mwisho wa siku kwa gharama zote ukitoa buku tano, michenji inarudi mingi mpaka mfuko unaomba poo kwa kuzidiwa uzito.
MIMI: Hahaha! Umeonaeeeee. Hakuna gharama kabisa. Ila poa, usijali. Ngoja nimtumie friend request halafu nianze kumfanyia uninja. Ila niandalie zawadi yangu.
EDUADO: Usijali kaka. Wewe fanya yako, ukimaliza, niache nami nifanye yangu. Au sio?
MIMI: Poa. Mia mia. Ngoja nianze kazi.
EDUADO: Shwari. Ngoja nifanye yangu. Nataka nimfuate mtoto Magreth hapa.
MIMI: Ndio yupi huyo?
EDUADO: Si yule wa facebook wa kipindi kileeeee.
MIMI: Kwani ushang’oa?
EDUADO: Chezea mimi wewe. Mimi noma…kama ni wembe basi Topaz.
MIMI: Sasa mbona hujamkata Aziza kama ni Topaz.
EDUADO: Aziza ana chembechembe za chuma. Ningemkataje? Huyo nakuachia kama wewe mwenye yale maji ya kuyeyushia vyuma ndio utakwenda nae sawa.
MIMI: Basi poa. Acha nikufanyie kazi yako mkurugenzi. Kazi hii niliachana nayo zamani sana ila kwa ajili yako, navaa gwanda nikukamilishie halafu nisepetue.
EDUADO: Mia mia.
Hapo nikatulia kwanza. Nikaanza kujifikiria ni kwa jinsi gani nilitakiwa kuanza kumfuata msichana Aziza. Kitu ambacho kilikuwa kikiniumiza kichwa changu kwa wakati huo ni kwamba hata Aziza mwenyewe sikuwahi kumuona kwa hiyo niliogopa kuuziwa mbuzi kwenye kiroba kama ilivyokuwa kwa Sikitu. Ngoja nikupe kijistori changu na huyu Sikitu.
Eduado alinifuata inbox na kuniambia kuhusu Sikitu, alimsifia na kumpamba sana, alinifanya nivutiwe nae sana na yeye alitaka nimchukue, nikasema poa. Mzee nikaanza mishemishe zangu kama Michael Scotfield wa Prison Breaak na kweli ndani ya wiki mbili, mtoto akawa mikononi mwangu. Unajua jinsi mtu anavyokwambia kwamba msichana mzuri hata kama wewe mwenyewe haujamuona unaanza kumtengeneza msichana wako kichwani, hivyo ndivyo nilivyofanya kwa Sikitu. Nikamtengeneza Sikitu wangu kichwani, kumbe nilikuwa namuumba Sikitu wangu bila kujua. Siku aliponitumia picha yake inbox niione mara baada ya kumlazimisha sanaaa, akanitumia. Alikuwa mrembo lakini hakuwa na urembo kama ambao Eduado aliniambia. Nikaachana nae.
Sikitu hakukoma, chating zangu nzuri za inbox za maneno ya hapa na pale alikuwa akizipenda sana, hivyo alitaka tuendelee kuchati. Haikuwezekana tena, nilimkatia maguu mara baada ya kuniambia kwamba anaishi Musoma, mbaya zaidi huku Dar hakuwa hata na ndugu kwa hiyo hakuwa na ndoto za kuja Dar, sasa mimi ningeonania nae wapi? Yaani nisafiri mpaka Musoma kwa ajili yake? Niliona kuwa suala gumu sana kufanyika. Basi ndio hivyo, tukapotezana potezana na hatimae mapenzi kutoweka, siku hizi simuoni, bila shaka, kaniblock.
Baada ya miezi miwili, leo Eduado kaja na mpya, kaja na demu mpya ambaye wala sijawahi kumuona, huyu anaitwa Aziza. Sikutaka kufanya vitu kwa presha sana, nilichokifanya ni kumtumia friend request na kisha nikianza kusubiria majibu. Kila siku nilipokuwa naingia facebook, hakuwa ameconfirm, sikuwa na shaka, niliendelea kusubiria zaidi na zaidi na baada ya siku mbili, akaikubali, furaha iliyoje? Hapo ndipo nilipoamua kuuanza mchezo wangu, mchezo ule ule ambao ulimfanya Sikitu kuchanganyikiwa kwangu, ila kwa hapa, kutokana na sifa ambazo niliambiwa na Eduado, ilinipasa nitumie mbinu kubwa zaidi, mbinu ambazo zingeendana na uzuri wake, mtoto wa kipemba bwana, hakutakiwa kufuatwa kikawaida, nami nikaanza kumfuata kipemba kipemba na mapenzi ya Kihindi….mtu mzima nikawa najiona kama Shahruk Khan vile.
Nimepewa kazi moja kubwa, kazi ya kumpata mtoto wa Kipemba, mtoto wa tajiri mwenye mapozi mengi.
Je nitafanikiwa kumpata mtoto huyu?
Je Eduado atanipa zawadi nikimpata au atanizunguka?
Hiki ni kijihadithi ambacho kitakuwa kinatoka kila siku hapa kwenye blogi yetu.
Itaendelea . . .
MTUNZI : NYEMO CHILONGANI