MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI
FACEBOOK CHATTING 4
0718 069 269
Maisha yalikuwa yakiendelea kama kawaida, kuhusu Aziza, wala sikuwa na wasiwasi kwa kuamini kwamba piga ua huyu mtoto ni lazima ningemchukua bila tatizo lolote lile. Kila siku nilikuwa nikiwasiliana nae, alikuwa akionekana kunikubali sana, chatting zangu zilizokuwa zikitabasamu zikaonekana kuuteka moyo wake. Nilikuwa na marafiki wengi facebook lakini nikikaa bila kuchati na Aziza sikuwa nikijisikia furaha kabisa.
Japokuwa Eduado alikuwa amenipa ishu ya kumfuatilia Aziza kama mchezo fulani lakini kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo nami nikazidi kufall inlove. Nilikuwa nikipenda sana Aziza, kila nilipokuwa nikiingia facebook na kumkosa, sikuwa nikijisikia raha kabisa.
Kuna nyakati za shida zikaingia, nyakati ambazo sikuweza kumuona Aziza online. Katika nyakati hizo maisha yalikuwa ya tabu sana, nilikuwa nikikosa furaha hata katika maisha ya kawaida. Nilimzoea sana Aziza, nilimpenda sana Aziza kwa hiyo kutokuuona uwepo wake machoni mwangu kilikuwa ni kitu ambacho kiliniumiza sana.
MIMI: Eduado vipi?
EDUADO: Poa. Inakuwaje?
MIMI: Kama kawa. Mbona Aziza simuoni siku hizi?
EDUADO: Tupo kwenye mitihani kaks.
MIMI: Sasa mkiwa kwenye mitihani ndio haruhusiwi kuwa online? Mbona wewe upo?
EDUADO: Mimi si unajua mbishi kaka.
MIMI: Dah! Nimemmisi sana Aziza. Nimemmisi ile mbaya kaka.
EDUADO: Usijali kaka. Mitihani ikiisha atakurudi online tu.
MIMI: Poa. Ila mnamaliza lini?
EDUADO: Wiki ijayo.
MIMI: Duh!
EDUADO: Nini tena kaka?
MIMI: Nahisi kama nitakufa kwa mawazo. Nahisi nitaweza kufa kaka.
EDUADO: Usijali kaka. Wewe vumilia tu utakula mbivu.
MIMI: Poa kaka.
Katika kipindi hicho ndicho nikajua kwamba moyo wangu ulikuwa ukimpenda sana Aziza. Huyu Aziza ndiye ambaye alinifanya niwaone wasichana wote kuwa wa kawaida sana, yeye ndiye aliyenifanya nimuone kuwa msichana mzuri kuliko wasichana wote duniani. Uwepo wake katika mtandao wa facebook bado nilikuwa nauhitaji sana, nilikuwa nikijisikia mpweke kupita kawaida. Aziza...Aziza...Aziza...up
Siku zikaendelea kukatika nahatimae siku ambayo ilionekana kunifurahisha ikawadia. Siku hiyo nikawa kama nimepigwa na mshtuko mkubwa moyoni, sikuamini kile ambacho kilikuwa kikionekana machoni mwangu, Aziza alikuwa online. Sikutaka kupoteza muda, sikutaka kuleta pozi, kwa haraka sana nikamtumia meseji.
MIMI: Mungu wangu!
AZIZA: Nini tena.
MIMI: Umekuja at last.
AZIZA: Yeah! Nilipotea kwa kipindi fulani hivi, si unajua mitihani wangu.
MIMI: Pole sana. Mmekwishamaliza?
AZIZA: Yeah! Tumekwishamaliza. Ila nami nilikumisi sana.
MIMI: Nashukuru kwa kunimis, ila ulimiss nini kutoka kwangu?
AZIZA: Chatting zako, meseji zako zimekaa kitofauti sana na watu wengine.
MIMI: Kivipi?
AZIZA: Zipo kitofauti sana. Katika maisha yangu nimewahi kuchati na watu wengi sana, ila zako...dah!
MIMI: Bado haujaniambia kivipi.
AZIZA: Kwanza hauandiki kimkato kama neno ‘sijui kuliandika cjui’, yaani maneno ya mikato huwa hauitumii kabisa.
MIMI: Kwani hiyo nayo ni sababu?
AZIZA: Ngoja nikwambie kitu Nyemo. Hii ni siri ambayo wanaume wengi wamekuwa hawaielewi na ndipo wanapofanya makosa kila siku.
MIMI: Siri gani?
AZIZA: Unajua unapochati na msichana yeyote ambaye haujawahi kuonana nae, unatakiwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, hiyo ndio sifa moja kubwa ya kumteka msichana kwa sababu hisia zetu hazitekwi na mambo makubwaaa, hapana, hivi vitu vidogo vidogo ambavyo wavulana wanavipuuzia ndio vinatuteka.
MIMI: Kama vitu gani.
AZIZA: Cha kwanza salamu Nyemo. Hivi unajua kwa sababu gani meseji yako ya kwanza kabisa uliyowahi kunitumia sijakujibu?
MIMI: Hapana. Sijajua kwa nini.
AZIZA: Salamu. Wanawake wengi wanalichukulia tofauti neno ‘mambo’. Unapomsalimia msichana kwa mara ya kwanza kwa kumwambia ‘Mambo’, wanaojibu ni wachache sana.
MIMI: Kwa nini sasa?
AZIZA: Kwa sababu mwanamke anapenda kufuatwa kinidhamu.
MIMI: Sasa nilitakiwa kukusalimia vipi ili ujibu?
AZIZA: Unapomfuata msichana yeyote duniani, anza kwa kumsalimia ‘Habari yako’ au salamu yoyote iliyokaa kinidhamu. Kidogo ukisalimia hivyo, kuna asilimia kubwa sana ya msichana kukujibu.
MIMI: Duh! Kumbeee!
AZIZA: Yeah! Hiyo ni siri ya kwanza Nyemo, wavulana wengi huwa wanafeli hapo tu kitu ambacho kinawafanya kila siku kulalamika kwamba wasichana tuna mapozi kujibu salamu zao, hapana, hatuna mapozi bali wanakosea kusalimia, wanakosa nidhamu katika kusalimia.
MIMI: Nimekuelewa. Naomba siri nyingine.
AZIZA: Chattin. Unajua usipende kuchati na msichana kifupi kama nilivyokueleza toka mwanzo. Andika neno lote kwa ujumla, unajua unapoandika kifupi, unaupa kazi ubongo wa mtu kulifikiria neno na matokeo yake akili yake inachoka na kukatisha chatting na wewe.
MIMI: Ila mimi sijawahi kuchati namna hiyo Aziza.
AZIZA: Najua. Ila ninakumegea siri juu ya vitu ambavyo msichana anavipenda na vile asivyovipenda.
MIMI: Dah! Umeifungua akili yangu.
AZIZA: Ila wewe..dah! Wewe mtu noma.
MIMI: Kwa nini?
AZIZA: Kama kuna msichana ulichati nae halafu akaonekana kuchoka na chatting zako, basi hakika hatoweza kuridhika na chatting za mtu yeyote yule duniani.
MIMI: Hahaha! Kwa nini?
AZIZA: Unaandika maneno kwa ujumla, hauandiki vifupi, cha kushangaza sasa
MIMI: Kipi?
AZIZA: Unafuatilia mpaka alama za maandishi. Penye kiulizo, unaweka, penye nukta, unaweka, penye mkato, unaweka, penye alama ya mshangao, unaweka. Nimekuvulia kofia.
MIMI: Hahaha! Ni kawaida sana Aziza. Napenda kuchati na mtu katika staili ya kuandika hadithi.
AZIZA: Hongera yako. Naomba nikuulize swali.
MIMI: Uliza tu.
AZIZA: Ulinimis?
MIMI: Sana tu.
AZIZA: Ulimiss nini kutoka kwangu?
MIMI: Chatting na mambo mengine.
AZIZA: Kama yapi?
MIMI: Uzuri...koh koh koh
AZIZA: Hahaha! Hebu acha kunitania, umewahi kuniona mpaka useme mimi mzuri?
MIMI: Unajua unapoongea na msichana usiyemfahamu simuni halafu ukasikia sauti yake, unajua tu kwamba huyu mzuri na huyu mbaya.
AZIZA: Sasa kwani mimi umeisikia sauti yangu?
MIMI: Hata unapochati na mtu, mwandiko wake unajionyesha kwamba huyu mzuri na huyu mbaya. Ila kuna kingine pia.
AZIZA: Kipi?
MIMI: Nilichogundua ni kitu kimoja. Wasichana wengi wanaoweka profile picha zao picha za wanawake maarufu wazuri, huwa wabaya. Ila walioweka picha za profile zao kama maua au midoli, huwa ni wanawake wazuri.
AZIZA: Hahaha!
MIMI: Yeah! Hii ni kwa sababu yule msichana mbaya kamuweka Rihanna kwa sababu anataka kutuonyesha kwamba yeye ni mzuri ila yule aliyoweka picha ya ua anataka kutuonyesha kwamba yeye ni mtu wa thamani, mzuri na ananukia kama ua au mdoli. Nililifuatilia hilo kwa marafiki zangu wengi na nikaligundua.
AZIZA: Kweli wewe mfuatiliaji. Kwa hiyo ukagundua mimi kuwa ni mzuri?
MIMI: Yeah! Nimegundua hilo kiasi ambacho kama nitaambiwa niombe kitu kimoja duniani nacho kitafanikiwa, basi ningeomba kuwa na wewe, basi.
AZIZA: Hahah! Acha utani Nyemo.
MIMI: Kwani naonekana kutania?
AZIZA: Yeah!
MIMI: Huwa sifurahii pale ninapokuwa serious halafu mtu ananiona natania. Nipo serius Aziza.
AZIZA: Sasa umenipendea nini? Hujawahi kuniona wala nini.
MIMI: Ngoja nikwambie kitu Aziza. Mapenzi ni hisia, mapenzi hayajalishi uwe umemuona mtu au haujamuona, vyote hutokea moyoni. Unapotumia kipindi kirefu kuchati na msichana fulani, automatical moyoni unafall inlove, hicho ni kitu ambacho hutokea kwa binadamu wengi wenye moyo wa nyama kama wa Nyemo.
AZIZA: Duuh! Hivi naomba nikuulize kitu.
MIMI: Uliza.
AZIZA: Unaongea mambo mengi sana mazuri Nyemo. Unaonekana kuwa una kitu cha ziada kichwani mwako.
MIMI: Hapana, sina kitu cha ziada. Akili nilizonazo mimi ndizo ambazo hata mtu mwingine anazo, tofauti kwenye kuzitumia hizo akili tu.
AZIZA: Unaonaaa. Kila unachoongea point. Nyemo una kitu cha ziada akilini mwako. Matumizi ya akili yako nayaona kuwa tofauti sana. Wewe genious.
MIMI: Genious! Acha utani. Niwe vipi Genious na wakati shuleni sijawahi kuingia hata kumi bora?
AZIZA: Sikiliza Nyemo. Kuna wale genious wa darasani. Haimaanishi ukiwa genious darasani basi hata kwenye kuongea na kuandika utakuwa genious, haiko hivyo. Kwa magenious wamegawanyika. Kuna wale wa darasani na wale wa sehemu nyingine kwenye maisha. Unaweza ukawa genious darasani lakini katika maisha ukawa mbumbumbu. Unakubaliana nami?
MIMI: Kiasi.
AZIZA: Hahaha! Usijali. Utanielewa tu. Turudi kwenye mada yetu.
MIMI: Kwa hiyo hivyo ndivyo mapenzi yalivyo Aziza.
AZIZA: Nimekuelewa Nyemo.
MIMI: Naomba nikuulize swali moja tu.
AZIZA: Uliza.
MIMI: Ushawahi kujisikia kitu chochote romantic moyoni mwako juu yangu?
AZIZA: Swali gumu kujibika Nyemo.
MIMI: Najua. Hata mwalimu anapoamua kutoa mtihani mgumu, kuna wengine wanafaulu japokuwa ni mgumu. Najua swali langu gumu lakini naona linaweza kujibika kirahisi sana.
AZIZAl Swali gumu Nyemo.
MIMI: OK! Ngoja nibadilishe swali. Unanipenda?
AZIZA: Ninakupenda sana Nyemo. Nahisi katika marafiki zangu wote facebook. U are the best.
MIMI: Dah! Ushatoka nje ya mada.
AZIZA: Kivipi?
MIMI: Hebu turudi ndani ya mada. Unanipenda?
Itaendelea.