skip to main |
skip to sidebar
HAWA NDIO WANAWAKE. . . USIULIZE NINI MANAKE NNINI?
Siku
ya kwanza atakuja na chup* mbili, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine
anavaa asubuhi anaondoka... Siku ya pili anakuja na khanga, anaivaa
usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka... Siku ya tatu
anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia 'Honey nitunzie nimesahau
hereni zangu mezani 'Siku ya nne anakuja na nguo mbili na vipedo vya
kubadilisha na viatu pea mbili, anavua high heels anaweka kwenye Shoe
rack, asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo.. Baada ya mwezi chumba
chako kinakuwa na vitu kadha wa kadhaa, na ole wako uvihamishe
alipoviweka, kesi zinaanza... Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima
si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza... Anahamia tartiiibuuu... Mwisho
wa siku dressing table yako iliyokuwa ina perfume na mafuta ya Rays
inakuwa imejaa hereni na 'Foundation' ...My Brother, huna haja ya
kuuliza,Ndo kashahamia huyo....Kifuatacho utaambiwa,''Honey I miss my
days', Zamani nilijua ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed Calls, Siku
hizi kuna Missed days, ukiambiwa hivi tu jua imekula kwako, inawindwa
ndoa....
Wanaumee, Mpoo?? Msiseme sikusema.