Utafiti huu unaweza kuleta taharuki kwa wanaume au wanAwake ambao wenzi wao wanafanya kazi maofisini, yaani ambao wameajiriwa. Hii inatokana na madai kwamba, katika kila waajiriwa kumi, saba wanatongozana na wenzao wa ofisi wanamofanyia kazi.

Utafiti huu ambao ulifanyika hivi karibuni unakuwa kama vile ni msumari wa moto kwa walio na wapenzi walioajiriwa, ambapo umebainisha kwamba, saba kati ya kumi miongoni mwa waajiriwa wanatongozana, kutomasana au kufanya mapenzi na wenzao wa ofisi moja, moja kati ya tatu ya hao wanaotomasana, kutongozana au kufanya mapenzi , hufanya hivyo na waajiriwa wenzao ambao nao wameoa au kuolewa.

Utafiti huo unazidi kubainisha kwamba, wanaopata hasara kwenye uhusiano huu wa maofisini ni wanawake zaidi kuliko wanaume. Mtaalamu Geoff Carter ambaye naye amewahi kufanya utafiti wa aina hii anasema kwamba, wanawake ambao mara nyingi huangukia kwenye mikono ya wapenzi wa nje ambao tayari wameoa, ndiyo ambao mara nyingi huumia kutokana na mapenzi haya ya kiofisi.

Carter alifanya utafiti wake kwa kuwahoji mameneja wapatao 400, katika utafiti wake huo alibaini kwamba wale walio kwenye umri wa miaka 18 hadi 30 ndio ambao wanafanikiwa kwenye uhusiano huu wa kiofisi. Lakini wale ambao wana umri mkubwa zaidi wawe wanawake au wanaume, mara nyingi huumia sana.

Ushauri uliotolewa a watafiti hao unawaasa wanawake kuacha kujiingiza kwenye mapenzi na watumishi wenzao kwenye ofisi moja kwani madhara yanayotajwa ni ule ukweli kwamba, mapenzi kwa watumishi wa ofisi moja huzaa wivu, fadhaa, kujifunga na wasiwasi mwingi.