Headlines News :

Sunday, April 21, 2013

UREMBO - JINSI YA KUTUNZA NYWELE KWA VITU ASILI

Leo katika somo letu la urembo ningependa kuangalia katika utunzaji wa nywele bila ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kemikali ambayo yamesababisha kwa kiwango kikubwa matatizo katika ukuaji wa nywele kama nywele kukatika,kunyonyoka,kupooza katika ukuaji n.k
Hina ni moja kati ya mimea ambayo watu wengi hasa wanawake huitumia katika kujiremba hasa kujichora maungoni bila kutambua kuwa mmea huo huweza kusaidia katika utunzaji wa nywele zao pia kwa kiasi kikubwa.

Hebu tuanze maandalizi ya Hina.

 MAHITAJI:-

  • Hina vijiko vitatu vya chakula.
  •  Kipande cha ndimu au limao.
  • Maji ya chai kiasi kidogo.
  • Glavu mbili mpya.







NAMNA YA KUFANYA:- 
  • Vaa glavu ili mikono yako isiharibiwe na hina.
  • Changanya hina na viungo vyake hakikisha haiwi nyepesi sana wala nzito sana.
  • Gawa nywele zako katika mafungu manne,kisha paka hina yako kwa uangalifu ili isichafue uso  wako.
  • Hakikisha unakaa nayo kwa muda usiopungua lisaa limoja.
  • Zikiwa tayari,hakikisha unaosha vizuri na kukausha nywele zako kwa taulo lililo safi.
Unaweza kuziweka nywele zako katika mtindo wowote baada ya kupaka Mafuta.




Ningependa kukushauri kutumia mafuta yasiyo na kemikali yatokanayo na vitu asili kama mimea, matunda nk.








UMEIPENDA POST HII???   SHARE NA MARAFIKI KWENYE FB & TWITTER ili nao waone!!
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger