Headlines News :

Sunday, September 8, 2013

MAPENZI MHHH!!!

Demu ana-beep, mshikaji wake kapiga
Demu (kalegeza sauti):hello baby,uko wapi?
Boy: niko hapa mwenge,kuna mambo yanilileta huku
Demu: hivi unajua kama mm naumwa?
Boy: unaumwa nini?
Demu: Tumbo linaniuma,kichwa nacho sasa ndo basi,yaani kimekuwa kizito kama nimebeba gunia la mahindi, sijui ni kitu gani? kula siwezi,yaani sina hamu kabisa,
Boy: okay,pole kawaida labda ndo unaingia kwenye siku zak
Demu: hapana kabisa,hii ni too much,njoo nikuone labda ntapona
Boy: sasa mm niko huku mbali,labda baada ya masaa matatu hivi
Demu: wewe hunipendi najua, yaani naumwa sina hamu ya kula afu unasema unakuja baada ya masaa matatu? kama umenchoka nambie
Boy: okay, nakuja sasa hivi, napanda daladala
Demu(kafurahi):kabla hujapanda gari, hapo Mwenge stendi kwenye njia ya kutoa magari,kuna ka-supermarket,ingia humo afu nunua maziwa ya unga Nido lile kopo kubwa,humo humo wanauzaga na juice,nunua kopo mbili,moja ya embe nyingine ya apple,mwambie muuzaji akupe na pakiti kubwa ya soseji basi afu ukitoka tu hapo kuna jamaa wana mkokoteni wanauza matunda,nchukulie parachichi,nanasi hata ndizi pia! nataka nione kama ntarudisha appetite.
Boy:umemaliza?
Demu:  ndio, basi wahi mwenzio nina hali mbaya hujui tu, afu niletee na vocha mwenzio nina deni kwenye line yangu.
Boy: umesahau mzani,na calculator
Demu: hayo ya nini? na ww kwa utani hujambo
Boy: maake naona unataka kufungua supermarket nyingine huko kwenu. Sasa nsikilize wewe mende, siji kama unaumwa hadi unapelekwa ICU haya wasalimie,yaani sijawahi ona mtu anakula kama wewe afu unajiita mgonjwa! Nyambafu zako , mbona sijasikia ukisema unataka dawa? usinipigie simu, kamweleze baba yako hayo mambo
UNAWEZA KU- LIKE HAPO JUU NA PIA KUSHARE NA WATU WAKO WAONE
  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger