Headlines News :

Friday, September 27, 2013

JINI MAHABA!



Majini ni nini?

Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa Moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita.

Viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;
Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.
Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vile vile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.
Taifa la Majini limegawanyika katika makabila Milioni Sabini na mbili (72,000,000) na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka.


Idadi ya Majini ni kila Binadamu mmoja kuna Majini 300 na wanaishi katika Majumba yetu, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa.



Majini wako katika aina Mbili (2); Maruhani na Mashetani.

Maruhani ni Majini wema ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na wanawasaidia Binadamu katika mambo mengi.
Mashetani ni Majini Waovu ambao ni wakorofi na wanawaletea Watu madhara na Matatizo mara kwa mara.
Baba wa Majini anaitwa JANN ambaye kimaumbile yeye ana tofauti ndogo na wenzie kwamba yeye ameumbwa kwa ulimi wa Moto.
Pamoja na mambo mengi wanayoyafanya Majini na kujihusisha na binadamu, Majini vilevile wanafanya kazi za Malaika hasa zile za mambo ya kupeleka Habari na kuwalinda Binadamu, mambo ya doria za Angani. Kazi hizi siyo zao lakini kwa vile wanapenda kuiga mambo basi huiga hata kazi ambazo siyo zao.
Majini na Binadamu wana sifa zinazofanana kwani wote wana akili na wote watahesabiwa siku ya Kiama na watazawadiwa kwa mema yao na maovu yao, wote wanakula na kuzaa.
Kama ilivyo, kuna wataalamu wa Kijini wenye fani sawa na Wataalamu wa Kibinadamu wenye kufanya kazi zinazofanana.
Tofauti kubwa iliyopo kati ya Majini na Binadamu ni kwamba; Majini hawana maumbile maalum na wana uwezo wa kujibadilisha katika maumbile mbalimbali ingawa wengi wa Majini wapo katika maumbile ya paka, nyoka na ndege.
Binadamu wao wana umbile maalum ambalo halibadiliki.

Majini wana uwezo wa kuwaingia Binadamu wakati Binadamu hawana uwezo wa kuwaona Majini isipokuwa kwa ufundi maalum.


Namna Majini wanavyowaingia Binadamu iko katika njia tatu:-
1.      Njia ya kwanza (1): ni kama Remote Control; Hii inamfanya yule aliyedhibitiwa kuweza kuelewa au kuwa na fahamu zake lakini anakuwa hawezi yeye mwenyewe kuudhibiti mwili wake na anasema yale anayotaka yule Jini.
2.      Njia ya Pili (2); Jini humwingia Binadamu ndani ya utosi na kuingia katika Mfumo wa Damu. Hii inamfanya yule Binadamu kupoteza fahamu na anakuwa haelewi kabisa kinachoendlea na anafanya yote anayotaka yule Jini.
3.      Njia ya Tatu (3) ni ile ya Jini kukaa nyuma ya Binadamu. Njia hii humfanya yule Binadamu anakuwa hapotezi fahamu ila anakuwa hawezi kufanya lolote na mwili wake.

{mospagebreak}
Majini vilevile wana uwezo wa Kusafiri kwa kasi ya upepo bila kutumia chombo chochote; Binadamu hana uwezo huo isipokuwa kwa msaada wa Majini.

Hiyo ni kusema kwamba mambo yote yanayofanywa na Wachawi na Wanga hayawezekani isipokuwa kwa msaada wa Kijini.

Jambo la muhimu ni kwamba pamoja na uwezo mkubwa walionao Majini, Wanadamu wana uwezo wa Kumtawala na Kumdhibiti Jini na vivyo hivyo Majini nao wanaweza kumtawala na kumdhibiti Binadamu wote kwa kutumia utaalamu maalum.

Wako Majini wa kila Dini na kila Kabila, na kuna watu wanaofuga Majini kwa kujikinga, na kwa kuboresha kazi zao au kujipatia utajiri. Pia kuna watu wanaofunga ndoa na Majini kwa kutumia utaalamu au kwa hiari za Majini hao.

Wabaya wa Majini ni Mashetani ambao wengi hawana Dini na ndio wanaoharibu mimba za Wazazi na kufanya mapenzi na watu usingizini bila hiari zao.
Kuepuka usichafuliwe kimapenzi, kabla ya kulala piga Bismillahi kwa Muislamu au taja jina la Yesu mara tatu kwa Mkristo.

MAUMBILE YAO YAKOJE?
·          
·         Majini wana maumbile makuu manne (4);
·         Wanakuwa katika maumbile ya Nyoka.
·         Wanakuwa katika maumbile ya Nge.
·         Wanakuwa katika maumbile ya Mbwa.
·         Wanakuwa katika maumbile ya Paka (Mweusi).
·         Kuna Majini wengine hawana maumbile yeyote na hawa shughuli yao ni kuruka hewani kuzunguka huku na kule na husafiri mbali kwa mara moja yaani kufumba na kufumbua.


SURA ZA MAJINI NA MASHETANI:


Majini sura zao ni za kutisha na mfano wake ni kama Matunda ya Mti wa Zaqum ambao unatoa matunda yenye sura mbaya na yanayofanana na mawe.

Majini wanakuwa na mkutano kila siku nyakati za kuchomoza na kuzama Jua na nyakati hizo ndizo ambazo wanafanya maasi yao.
Fitna na Maasi yao mengi wanafanyia upande wa Mashariki.
Majini vilevile wanaweza kujigeuza kama mbwa mweusi au paka mweusi kwa sababu Majini wanapenda Rangi Nyeusi kwa sababu ya kiza.

WANAKULA NINI?

Majini wao wanakula mifupa na mavi ya farasi. Hivyo ni vyaluka vyao vikuu pamoja na kwamba wengine wanakula Moshi (Ubani) na wengine wanapenda kunywa damu.
Wanapokula au kunywa, wao hutumia mkono wa kushoto na Majini wazuri ndio ambao wanakula mifupa mizuri na kuwaachia mifupa mibaya na uchafu Majini wabaya au Mashetani.

JE MAJINI WANAZAA?


Majini wanaoa na kuongezeka kama tulivyo Binadamu na huzaana kwa wingi sana.

Katika wao kuna wale wanaokula na kuoana na kuna wale ambao hawafanyi hayo.
Binadamu Mwanamume ana uwezo wa kumuoa Jini Mwanamke na Jini wa Kiume ana uwezo wa kumuoa Binadamu Mwanamke pamoja na kwamba ndoa inayotambulika na Mwenyezi Mungu ni ya kiumbe kwa kiumbe yaani Binadamu kwa Binadamu na Jini kwa Jini.
Huyu ni JINI MAHABA wa Kike anaitwa SUCCUBI huwajia wanaume na kufanya nao Mapenzi






Jini Mahaba wa kiume akiwa Kazini ni hatari sana hawa






  •  
    Support : Blog designer | Blogger | Developer | | KakyteeMedia.InC
    Copyright © 2011. Kakytee.com - All Rights Reserved
    Template Modified by KakyteeMedia
    Proudly powered by Blogger